Tuesday 29 April 2014

Re: [wanabidii] Siungi Mkono Adhabu ya Kifo

Unajua,Mungu uhukumu,lkn sio kila mtu uhukumiwa na Mungu mfano,mwanao usipomlea vizuri hatakuwa mtoto mzuri ...sio kama Mungu kashindwa lkn anajua ni jukumu lako wewe kumlea mwanao fresh. Wapo watu ambao lazima wahukumiwe na sis wanadamu,na ndio maana zipo jela .. Mungu alitoa nafasi kwa nyerere kumuhukumu idd amini,akamuacha ..sasa Mungu yeye angefanyaje? Mbona sadam hussein na gaddaffi wao hatukuwaachaa,umesikia Mungu kalalamikaaaa

'Nico Eatlawe' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ngupula,
 
Umenifurahisha kwa hoja zako! Hiyo ndiyo inaitwa nguvu ya hoja. Ila bado hujanijibu hoja zangu mbili. Hawo unaowataja nani kauawa kwa upanga?  Mfano wa Daudi aliyeua wengi mpaka askari wake. Mungu ndiye anayejua nani atakufa kwa upanga. Mfano Amini aliua sana ila kafa kifo cha asili. Walioua na kuuawa ni kama Sadam, Gadafi, Osama, Hilter etc.
On Tuesday, 29 April 2014, 10:34, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Dhambi ni kutenda na kukubaliana na wanaotenda na kukubaliana na wanaotenda . Refer kifo cha stefano...ngoja nikupe list nyingine solomon,samson,joshua....hukumu ni kwa haki na haki ya hukumu ni kwa watoto wa mungu..kuna wakristo wengine wanadhani hata kuua mende ni dhambi.....ngupula

misangocharles via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Musa aliua kwa kutetea haki na paulo aliua kwa kumtetea Mungu. .binafsi sioni haja ya kuthamin maisha ya mtu na mtu huyo hawez thamin maisha ya wengine...auaye kwa upanga atauawa kwa upanga...amwagaye damu naye damu yake itamwagwa. Eliya ,musa,samweli,daud wote waliua...wewe unamjua mungu kuliko waooooo....ngupula

'Nico Eatlawe' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ngupula usitetee hoja yako kwa kusingizia biblia na tena kimakosa. Paulo alimuua nani?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
From: "'Ngupula GW' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 29 Apr 2014 11:26:38 +0300
To: 'Nico Eatlawe' via Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Siungi Mkono Adhabu ya Kifo

Kumhukumu mtu kifo ni ukatili na unyama usio na kifani bila kujali mtu kafanya nini. Hata Mungu amewaacha watenda maovu wanaishi hadi wanakufa wazee akijua kuwa kila mtu anastahili fursa ya kubadilika. Ila sisi tunapenda kuua kwa sababu za chuki na kama namna ya kumaliza shida haraka. Ila hakuna suluhu inayopatikana kwa hukumu ya kifo. Mimi napinga hukumu ya kifo kwa sababu mbili:
 
Kwanza haimpi mtu fursa ya kujutia makosa yake na hata kubadilika. Kama Mkristo ninakumbuka wauaji ambao Mungu hakuwaua. Mfano Musa aliua hata akatoroka na kukaa kama mkimbizi miaka 40. Baada ya hapo akaitwa kuwa Mpigania uhuru wa taifa la Israeli kule Misri. Wa pili ni Sauli au Paulo. Paulo alikuwa serial killer ila Mungu alimbadilisha na kuwa mtume mkubwa sana hata kuandika zaidi ya nusu ya Agano Jipya. Hawa wote walikuwa wauaji lakini walikuwa na uwezo wa kuwa watumishi wakubwa wa Mungu. Kwa hiyo naamini wauaji au wahaini au wahalifu wote wanaweza kuwa watu wazuri na wa kufaa kwenye jamaii kama watapewa fursa ya pili.
 
Pili siungi mkono kwa vile wengine wanaoua wenzao wanapenda kufa zaidi kuliko kuishi. Kwa hiyo kumwua ni kumtimizia maono yake. Mfano ni watu wanaofanya ugaidi hata kujitoa mhanga wakiamini kuna thawabu baada ya kufia wanachokiamini. Kwa hiyo kwanini umsaidie mtu kutimiza nadhiri ya itikadi yake? Atajifunza na kubadilika lini ukimwua?

0 comments:

Post a Comment