Wednesday 30 April 2014

Re: [wanabidii] Majambazi (wakitumia pikipiki) wapora na kuondoka na Pesa - Airport

Wameua kwa makusudi. halafu ndio tunaongea mtandaoni na ktk jamii kupoinga hukumu ya Kifo? Eti wanahaki ya kuishi, kifungo cha kawaida watajirekebisha. Huyu awe mwanao, baba yako, nduguyo, friend wa katibu, ipo calculated ameuawa, utasema kama wangekamatwa ghapo nao wasife. Mtu anamchinja mwenzake kwa kugombania shamba la mirathi-asinyongwe.

Juzi hapa baba kamwagia maji ya moto mwilini mwanae msichana wa sekondari. Kisha akiwa amelazwa hospitali akampelekea juice yenye sumu anywe afe-akafa na ikagundulika amemuua huyo binti-haki za binadamu asiuawe kwa kunyongwa!! Hawa walipata taarifa ofisini kuwa jamaa atachukua hela nyingi bank-wakamfuatilia au mtu wa bank akala mpango na vibaka kuwa hapa jamaa yupo hivi anatoka nje hapo ana milioni 50 hivi nao wakamfuatilia, anaingia garini mpaka mataa. vingi vinawezekana.

Ndugu, Mke, rafiki msiri wako pia wanaweza kula njama na majambazi kama baba mmoja wa DSM aliletewa milioni 200 na wanawe aanze investment, akastaafu kwa hiyari afanye hivyo. Mke akazichukua kumpa kakake wakala njama wakamtia vumba mume akatembea kwa mguu miaka 6 anazurura DSm-tabora-tanga, Morogoro, Iringa hajui atokee wapi. Mkataba ukaandikwa, kaka na dada waligoma kulipa deni  ulipofika, wakampaisha. Watoto USA wakamsaka baba, eti mama hajui baba alipo si walimpa mihela-kamtoroka na wala mama yao hajakwenda kutoa taarifa polisi hana habari kabisa kwa vile amejua amefanya nini. Baada ya miaka kadhaa (6) akaibukia Morogoro uwanja wa sala wa kanisa linaloita mizukule na watu waliovifungoni wakati wa maombi. Njiani akiuliza watu huko wanakoita ni wapi? Akakutana na mzazi wa mwanafunzi wake wa shule ya msingi akamkumbuka huyo baba, akampa viatu na nguo, maji, akamuelekeza huko wanakosali, akaenda, ndio akafunguka huko. Watu walilia kulikoni.

Miaka sita ya kupishana na wanyama pori, kulala mashimoni na msituni unakokwenda hifiki? Na mke mchawi anasali kanisani daima!! Baba wa watu akajieleza yaliyomkuta, wakaita watoto through facebook alikuwa na address ayo, wakaja bongoland kumchukua. Huyo kama ndio mama yako mzazi utamfanyaje? hawa si watu wa kuwaweka? WAFE!!

On Wednesday, 30 April 2014, 1:18, Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com> wrote:
Nimepita maeneo hayo nikakuta ajali kumbe ndiyo ilisababishwa na hao majambazi? Halafu OCD wa Sitaki Shari ni km 2 au 3 tu.
On Apr 29, 2014 11:18 PM, "Fakhi Karume" <fkarume@gmail.com> wrote:
Watu waliokuwa wanatumia pikipiki wamempiga risasi mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari na kumpora begi lenye pesa na kisha kutokomea na pikipiki yao.
Mtu huyo amepigwa risasi na kufariki papo hapo (maeneo ya mataa ya Uwanja wa Ndege, Dar)
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment