Tuesday, 29 April 2014

Re: [wanabidii] Siungi Mkono Adhabu ya Kifo

Kumhukumu mtu kifo ni ukatili na unyama usio na kifani bila kujali mtu kafanya nini. Hata Mungu amewaacha watenda maovu wanaishi hadi wanakufa wazee akijua kuwa kila mtu anastahili fursa ya kubadilika. Ila sisi tunapenda kuua kwa sababu za chuki na kama namna ya kumaliza shida haraka. Ila hakuna suluhu inayopatikana kwa hukumu ya kifo. Mimi napinga hukumu ya kifo kwa sababu mbili:
 
Kwanza haimpi mtu fursa ya kujutia makosa yake na hata kubadilika. Kama Mkristo ninakumbuka wauaji ambao Mungu hakuwaua. Mfano Musa aliua hata akatoroka na kukaa kama mkimbizi miaka 40. Baada ya hapo akaitwa kuwa Mpigania uhuru wa taifa la Israeli kule Misri. Wa pili ni Sauli au Paulo. Paulo alikuwa serial killer ila Mungu alimbadilisha na kuwa mtume mkubwa sana hata kuandika zaidi ya nusu ya Agano Jipya. Hawa wote walikuwa wauaji lakini walikuwa na uwezo wa kuwa watumishi wakubwa wa Mungu. Kwa hiyo naamini wauaji au wahaini au wahalifu wote wanaweza kuwa watu wazuri na wa kufaa kwenye jamaii kama watapewa fursa ya pili.
 
Pili siungi mkono kwa vile wengine wanaoua wenzao wanapenda kufa zaidi kuliko kuishi. Kwa hiyo kumwua ni kumtimizia maono yake. Mfano ni watu wanaofanya ugaidi hata kujitoa mhanga wakiamini kuna thawabu baada ya kufia wanachokiamini. Kwa hiyo kwanini umsaidie mtu kutimiza nadhiri ya itikadi yake? Atajifunza na kubadilika lini ukimwua?
 
Kwa hiyo mimi nafikiri bora ni adhabu kali na kifungo cha maisha. Namkumbuka dikteta jenerali manuel Noriega  wa Panama aliyenagushwa na Wamarekani na kuongoka gerezani. Hwajamwua ila walimwachia Wafaransa waliomfunga na kumwachia na hatimaye kurudishwa kwao. Kwa hiyo tuwape watu nafasi ya pili. Tusilipe ubaya kwa ubaya bali ubaya kwa wema!
On Monday, 28 April 2014, 22:58, "'lesian mollel <aramakurias@yahoo.com>' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
daaah, hii si haki kabisa.
Cjui hawa wanaoamua kesi kama hizi kama wanaangalia uzito wa kesi,600 si mchezo na kesi ya kisiasa unahukumu kifo? hz nchi zinaongozwa na madikteta
Logically adhabu za vifo zifutwe kote duniani, mungu pekee abakie na mamlaka ya kuamua kumchukua yoyote kwa kua ndio abakie na mamlaka ya kuamua kuchukua roho yake kwakua kaiumba yeye si binaadam yoyote.
Jumuia  kimataifa ziintervene haraka sana kuokoa roho z a wapendwa hawa kabla haziaangamizwa, watawala kama hawa wanasumbuliwa na woga na ulafi tu

On Monday, April 28, 2014 8:32 PM, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
----- Forwarded Message -----

Boxbe This message is eligible for Automatic Cleanup! (dekleinson@gmail.com) Add cleanup rule | More info
Sijui kosa lao, wala sijafuatilia kisa ila nitachangia as sober.
Kwangu mimi hukumu ya kifo naunga mkono 100% ila sio katika mazingira yote.
Hivi mfano mtu amepewa dhamana ya uongozi mahali, kwa tamaa, na ujinga wake baada ya kupokea misaada flani/fungu kuwapelekea wananchi yeye akala na kusababishia baadhi yao kukosa huduma hizo muhimu/chakula hata kupelekea kifo. Au ni mkemia mkuu akaruhusu vyakula vyenye sumu kuingizwa nchini kumbe nyuma ya pazia kaweka mlungula mfukoni.
Mtu wa namna hiyo afanywe nini?? Hayo mataifa ya magharibi yaingilie tuone!!! Mbona walimminya Osama bila kumpa haki ya kujitetea kisheria?? Hawakutangaza atakaemuua kuna dongo nono la fedha?? I know the guy was guilt but not proven mbele ya mahakama!! Kama ndivyo wangeweka sheria kama Rwanda, "everyone is guilty until proven innocent.."
Tuwe makini, weakness ya sheria itatutudisha nyuma kimaendeleo maana watu watachukulia mwanya huo huo kujipigia magoli ya visigino!!!!
Atakaesema nina roho mbaya anisamehe maana ndivyo nilivyo na huwa najiona nimekamilika vizuri sana.
"...by citizenship am a Tanzanian, nationality African..."
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment