WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR SIO YA VYAMA VYENU VYA SIASA
Hivi sasa tunaingia katika hatua nyengine muhimu ya mchakato huu wa kutafuta Katiba mpya ya nchi yetu. Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshakamilisha kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo imeshatangazwa.
Wale wote waliopata fursa hii ya kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kutokea Zanzibar, kutoka katika chama chetu, katika vyama vyengine na makundi mbali mbali hawana budi kuweka maslahi ya nchi kwanza na kuweka pembeni itikadi zao za kisiasa ili wende katika Bunge la Katika kuyatetea maslahi ya Zanzibar.
Wajumbe hao hawana budi wafahamu kwamba wazanzibari kwa muda mrefu wamekuwa wakililia suala la kutotendewa haki ndani ya Muungano huu, hivyo hii ni fursa pekee adhimu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kupigania hadhi, haki, heshma na usawa baina ya pande mbili za Muungano na hatimae kutoka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliyo bora na yenye kulinda maslahi ya pande zote mbili.
Tunawaomba sana mnaokwenda katika Bunge la Katiba, nendeni mkaitetee Zanzibar na sio vyama vyama vyenu vya siasa. Wala sio kutetea maslahi ya Tanzania kwanza kama inavyosisitizwa na baadhi ya viongozi na wanasiasa wasioitakia mema Zanzibar. Tanzania ni mtoto wa Tanganyika na Zanzibar. Haiwezekani hata siku moja mtoto awe na uwezo na mamlaka ya kuweka misingi na kuwapangia mambo wazee wake, badala yake mtoto apangiwe na wazee wake. Ndio hivyo hivyo Katiba ya Shirikisho la Tanzania, mamlaka yake na mipaka yake ilitazaliwa ikiwa ni mtoto atokanae na maamuzi ya watanganyika na wazanzibari kwa namna ambavyo wanataka, na sio Tanzania ikasimu mamlaka na iweke mipaka kwa Tanganyika na Zanzibar.
Nawatakia kila la kheri na afya njema wajumbe wote wa Bunge la Katiba, wende wakaifanye kazi yao kwa uadilifu na warejee wakiwa na afya njema na Katiba bora kwa watanzania wote.
Amin.
Wasiliana na Maalim Seif: https://www.facebook.com/pages/Maali...63084730502824
-- Hivi sasa tunaingia katika hatua nyengine muhimu ya mchakato huu wa kutafuta Katiba mpya ya nchi yetu. Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshakamilisha kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo imeshatangazwa.
Wale wote waliopata fursa hii ya kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kutokea Zanzibar, kutoka katika chama chetu, katika vyama vyengine na makundi mbali mbali hawana budi kuweka maslahi ya nchi kwanza na kuweka pembeni itikadi zao za kisiasa ili wende katika Bunge la Katika kuyatetea maslahi ya Zanzibar.
Wajumbe hao hawana budi wafahamu kwamba wazanzibari kwa muda mrefu wamekuwa wakililia suala la kutotendewa haki ndani ya Muungano huu, hivyo hii ni fursa pekee adhimu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kupigania hadhi, haki, heshma na usawa baina ya pande mbili za Muungano na hatimae kutoka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliyo bora na yenye kulinda maslahi ya pande zote mbili.
Tunawaomba sana mnaokwenda katika Bunge la Katiba, nendeni mkaitetee Zanzibar na sio vyama vyama vyenu vya siasa. Wala sio kutetea maslahi ya Tanzania kwanza kama inavyosisitizwa na baadhi ya viongozi na wanasiasa wasioitakia mema Zanzibar. Tanzania ni mtoto wa Tanganyika na Zanzibar. Haiwezekani hata siku moja mtoto awe na uwezo na mamlaka ya kuweka misingi na kuwapangia mambo wazee wake, badala yake mtoto apangiwe na wazee wake. Ndio hivyo hivyo Katiba ya Shirikisho la Tanzania, mamlaka yake na mipaka yake ilitazaliwa ikiwa ni mtoto atokanae na maamuzi ya watanganyika na wazanzibari kwa namna ambavyo wanataka, na sio Tanzania ikasimu mamlaka na iweke mipaka kwa Tanganyika na Zanzibar.
Nawatakia kila la kheri na afya njema wajumbe wote wa Bunge la Katiba, wende wakaifanye kazi yao kwa uadilifu na warejee wakiwa na afya njema na Katiba bora kwa watanzania wote.
Amin.
Wasiliana na Maalim Seif: https://www.facebook.com/pages/Maali...63084730502824
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment