tunachokitaka hapa ni u-nia au utashi wa wana CCM wa kuwa na mwelekeo mpya wa nchi hii ya Tanzania. kimsingi anachokisema Mtatiro ni sahihi, ukiangalia mwenendo wa bunge unaona sura za ugiza kwa baadhi ya wajumbe. suala la katiba ya nchi sio suala la miaka mitano au miaka minne kama baadhi ya wajumbe wanavyofikiria, ni suala la mstakabali wa maisha ya taifa husika ndani na nje ya taifa hilo. Sasa wapo wenzetu ambao ni Machievelians wao wanaangaika kumantain power lakini wanachokosea wanaangaika kumantain temporarly power, na wanasahau kuwa hiyo power pia inaweza kuwa threatened na mataifa ya nje kama mtakuwa na sheria mbovu.
mfano mtu anakazana apate serikali mbili au tatu kwa kuangalia kuwa upande mmoja wa muungano ni mtaji wa kisiasa kwake lakini anashindwa kujua kuwa mkiwa na muungano ambao unatengeneza utupu wa kisiasa kitu chochote cha weza kujaza utupu huo.
Mfano mwingine ni kuhusu kura ya wazi au ya siri, hapa mmeweka mijadala mikubwa kweli bungeni kana kwamba hilo ndilo suala pekee mlilo nalo la kujadili. Unaposema kura ya wazi au ya siri ni lazima ujue athari na faida za kila upande. Unaweza kuchagua upande utakao tengeneza machafuko ya kisiasa kuliko kawaida. mfano umechangua kura ya wazi, kinachotokea ni kupiga kura kwa kuonana nani kapiga wapi. hii sio shida ila ni kwanini fulani kapiga kwa lipi? hii ndio shida. Mambo ya msingi katika hili ni muundo wa bunge maalumu, yapo makundi mabayo kimsingi yakiguswa hata wabunge walioko ndani ya bunge hilo wanaweza kubeba siraha, na njia zozote zile kuyatetea na haya yako juu ya vyama vya siasa na madaraka. Unaposema sema kura la siri pia lipo jambo ambalo Watanzania tungependa kujua misimamo ya viongozi wetu. lakini tukisema tunataka hivyo swali je nchi hii yenye watu zaidi ya 44 millioni nani anaweza kuunganisha matakwa yao.
Nadhani tunahitaji kuwa na umakini Watanzania katika hili, sio jambo la kichama au kikundi fulani bali ni mstakabali wa taifa.
On Thursday, March 27, 2014 3:27 PM, Haidari BENN <benntz@yahoo.co.uk> wrote:
Muungano Na Utanzania Kwenye NjiaPanda.
Sheria Mama Na Mikinzano Kwenye Hotuba za Jaji Warioba Na AmiriJeshi Rais Kikwete.
Yaliyotamkwa Na Vigogo Hivi 2 Yametingisha Taifa Kiasi Ya Kwamba Wananchi Wamejikuta
Wamo Pandani Mwa Njia Iliyojaa Michechele -Wananchi Na Wabunge Wasipotahadhari Wakakanyaga
Kipotenza Njia /Chechele ,basi Sura Ya 6 Ya Rasimu Na Jinsi Ilivyo-sukwa Na Namna Ilivyoandaliwa
Kiuledi Kwa Vifungu Kiasi 67 ,Huenda Wakajikuta Pabaya ,Siko Palipo Kusudiwa Na Waasisi Wa Muungano.
Wananchi Wapo Katika Hali Ya Kupigwa Na Bumbuwazi Na Kujiuliza "Jamani Tumetowa Maoini;Jaji Warioba
Amewasilisha Maoni Yetu Na Fasiri Yake Kuhusu Maoni Yetu; Rais Kikwete ,Nae Ametowa Maoini Yake
Kuhusu Yaliyo Pendekezwa - Sasa Hawa Wabunge Walipelekwa Kule Dodoma Kujadili Na Kuboresha Yale
Yatakayo/Yaliyosemwa Na Jaji Warioba Na Rais Kikwete Au Waijadili Rasimu Ya Katiba Mpya? ".
Au Ndio Tuseme Wabunge Kwa Bahati Mbaya Wamekwisha Kikanyanga Kile Kitu - Chechele ?
Au Ndio Ujanja Wa Kuengeza Posho ? Wakati Ninatafakari Kuchachanua Nipate Siri au Majibu Ya Masuala Hayo
Matatu ; Pakapigwa Simu. Nilichoambiwa "Kinara wa CUF-Zanzibar Amekasirishwa Sana Na Aliyoyasema Rais
Kikwete ,Bungeni Na Kwa Hivyo Ameitisha Mkutano Wa Hadhara ,Ili Afoke Aonyeshe Hasira Zake".
Suala la Nne Likajitokeza ; Kumbe Waliokanyaga Chechele Si Wabunge Tu?.
Katika Kuchunguza -Chunguza Ya Ndani Yaliyo Tamkwa Na Jaji Warioba ,Nikaambuliya haya yafuatayo :
(1)Kasoro na yale yaliyoengezwa kinyume na Kubaliano Mama la Waasisi la 26April 1964.
(2)Walikubaliana Pawepo Bunge Moja Kwa Nchi Moja ,Lakini Upande Wa Visiwani Baraza La Mapinduzi Liwepo
Kidete.Mabunge hivi Sasa Yapo Mawili.Nguvu za Baraza la Mapinduzi Zimeathrika .
(3) Mamlaka Rais na Mahakama Ya Rufani Hayana Ubayana wa Kuridhisha.
(4) Wabunge Wa Visiwani Wana haki Ya Kushiriki katika Kuamua Yanayohusu Tanzania-Bara ,lakini haki hiyo
hawanayo Wabunge wa Bara kuwepo kwenye uamuzi wa mambo ya Visiwani.Hii Ndio ile hali sugu inayoleta zile
sintofahamu baina ya pande mbili na ukaidi wa " Cha Kwetu Chetu ;Cha Kwao Chetu Cha Ushirika ".
(5)Wabunge wa Tanzania Wanazo Kero 11 za Ukosefu wa Usawa baina Wao Na Visiwani.
(6)Wabunge wa Visiwani Nao wanasema Kero zenu mmetuzi kwa moja sisi tunazo 10 kuhusu Usawa.
Nikajiuliza Sasa Hawa ,kazi yao ni kushindania Nani Ni Mbabe Kuzidi Mwengine Katika Kufanyiana Ubabe?
Mimi Nikajiuliza Mbona Jamani wale Waasisi mambo yao yalikua powa ? Walikubaliana Nchi Yao Ni Moja,ila
tu inaserikali Mbili.Mbona Hawaku sema Nchi 2 kwa serikali 2 ?
Nilipofika nikagutuka nikamkumbuka Mzee wetu msema Ukweli mwenye kujuwa hesabu.
Alisema bila kigugumizi na akawauliza wananchi "Hebu Jamani Nisaidieni Hivi 1+1 = Ni 3 ? Mwalimu aliuliza.
Sasa Rais Kikwete , afokewe ,apigiwe makelele ya mchana na usiku,Bungeni na sijui wapi na wapi London
Dubai ,New York ,Kibandamaiti na Kibanda-Chechele gasia hii ya nini?
Rais Kikwete,hakufanya wala hakuwa kipya.Alichokifanya ni kutahadharisha pasikanyagwe chechele au upotoshi
wa kufanya walizozifanya Waasisi kwamba uhakika wa mambo ni kwamba Moja Na Moja Ni Mbili.
Tulipo fika hapa ni kwamba Upo Utata wa baina ya wasemao 1+1+ = 2 Na wale wasemao 1+1+ 3.
Miundo Yote Miwili inazo hatari zake kwa Uhaiwa Muungano.
Nini cha kufanya utakapokabiliwa Na Mbadala 2 Hatarishi ya Ifiriti Au Ibilisi? .Nilijiuliza .
Nikashindwa - Nilikwenda Vichochorinina Mitaani kuuliza huyu na yule kupimisha fikira.
Hitimae Nilimuuliza Bi-Mkwe ,kwa sababu ni Mzee Wa-Kikale,akaniambia ya Ifiriti na Ibilisi yeye hayajui.
Lakini kwa mambo ya kikawaida tu,mtu anapokabiliwa na ulazima wa kuchagua kwa mabadiliko mazito na
ya ghafla mtu akumbuke "Usiwache la Mbwachao,kwa Msaala Upitao ".
Nikamuambia Bi-Mkwe,hayo usemayo,ni rai hasa kwa wale wanao watumikia wananchi .
Viongozi wa Nchi hawawezi kuendesha kwa mitazamo ya ubinafsi au kushauriana na wake au marafiki zao.
Au vipi ? Kwa Si mnakumbuka moja wapo wa zile hekaya za Muasisi ?
Ninayotaka Kuyazungumza hapa ni:
(a)Pendekezo la Tume ya Warioba ,Serikali 3 au 2 kwa ufupi.
(b)Maoni Ya Rais Kikwete,kwa ufupi.
(c)Tamko la Baadhi ya Wabunge wa Kuteuliwa wa Bunge Maalum La Katiba.
(d)Ndimi Tamu Zenye Maneno Hisia na Ushabiki Potoshi.
Pendekezo La Jaji Warioba.
Tarehe 18 march Jaji Warioba amewasilisha pendekezo la Tume yake Kwa Wabunge wa Bunge
Maalum La Katiba Mpya Ya Tanzania.Kwa maneno yake mweyewe nanukua"...tumependekeza serikali 3
kutokana na ufasiri wetu wa yale maoni ya wananchi".Amesema nifasiri yaTume ;na sio kwa mujibu wa
maoni ya moja kwa moja ya wananchi. Hata hivyo,washabiki wa serikalai tatu na wakaidi wa shirikisho la
Muungano kwa nkataba ,wakapiga vigele-gele ,wakajitangazia ushindi kivyao/subjectivelly bila ya kua na
utulivu wa kusikiliza,kuelewa na kufaham kiundani wa mahusiano-pacha na yale aliyoendelea kusema
Jaji Warioba .Hiyo ndiyo shida ya mwanzo ya msingi ya sintofaham ya Ukaidi wa Wapinzani.
Serikali 3.
Cha Msingi Jaji Warioba pawepo Nchi 1+Taifa 1+Uraia 1+Sarafu 1+Dola 1 Na Serikali Tatu.
Na utaratibu huo ufuatiliwe na haki huru za Uhamiaji ,Umiliki ,Ufanyaji Biashara,Kuchagua na Kuchaguliwa
hudumana na elimu kwa wananchi wa pande zote mbili bila ya vikwazo au ubaguzi wa aina yeyote.
Duuh !! Wakaidi wa CUF-Zanzibar ,badala ya kupiga vigele-gele walivimba mashavu wakawaka na maneno
ya ajabu-ajabu "No Cha Kwetu Chetu; Cha Kwenu Kiwe Chetu Shirika Kwa Mkataba ".
Hoja kuu ni kua eti "Nchi Yetu Ndogo,Ardhi Yetu Sio Kubwa Kama Yenu; Mtatumeza.Mambo Hayo ya Ardhi
Yasiwemo ". Mwenzao mmoja akawaambia,"Jamani hizi kelele za nini ; ikiwa kweli mnataka Muungano
ambao tunao sasa ni miaka 50 ,hamuwezi kula vya washirika wenzenu tu,na vyenu viwe marufuku kwa
wenzenu .Hata huo Uisilamu unakukatazeni.Huu Ukaidi wenu khasa mnasema kwa niaba ya NANI ?
Mliwauliza wananchi kuhusu masuala haya au mliharakisha kuwa babaisha na agenda chuki za kero za
Muungano kwa shabaha ya kuvunja Muungano ? Uhalali gani mlio nao kuhusu mada hii?
Isiwe huu ni Ulafi na njama ZENU za uchu wa madaraka "by all means necessary " bora tu Kinara wenu awe Rais
mpate Uwaziri na wingi wa Mabalozi ?.
Na khasa Hii Uzanzibari Kwanza Tanzania Baadae ina shabaha gani,kuvunja Muungano kwanza halafu tuanze
upya Kuujenga ?
Kuhusu Muundo wa Serikali 2 -kiufupi .
Jaji Warioba,alisema nanukua "....Yeye na wenzake wameona kwamba kwa utafiti wao mfumo wa hivi,ingawaje
nihalisi kama walivyotaka waasisi,lakini umeshindwa kutatua kerozilizopo kwa muda mrefu,kwahivyo muundo
huu wa serikali unahitaji marekibisho makubwa".Kimtazamo wao objectivelly ni kwamba muundo wa serikali 2
hauna ubaya ila tu unahitaji marekibisho na uboresho.
Kwa upande huo Rais Kikwete ,hakukinzana na JajiWarioba kwa fikra hiyo .Na inaeleweka kwamba imani ya
ya "the silent majority " inakubalika kwa hilo na inapatikana kutokana na wale wengi ambao kwa mujibu takwimu
ipo bayana kwamba wapo wengi ambao hawaja zungumzia/lalamika kwa suala la muundo wowote maalum wa
Muungano.Inawezekana kwamba hao "the silent majority"hawataki au hawajapendelea kuingizwa katika mambo
mepya wasio yajuwa yatawafikisha wapi ; waliogopa kukanyaga kipoteza njia/chechele wakaingizwa kwa Ifiriti au
kwa Ibilisi - " Mti na Macho ndio Dira Yao au pengine walisikiza yale ya Ma-Babu na Ma-Bibi-Zao wa kale
"Usiawache Mbwachao ;kwa msala upitao".
MaoniYaRais Kikwete -Kwa ufupi.
Siku Ijumaa tarehe 21 March Rais Kikwete,kaenda Dodoma kuhutubia Wabunge.
JK ,ni Kinara wa Nchi,Taifa na Dola ya Tanzania amekula Kiapo - Cha Kuheshimu Katiba ya hivi sasa;yeye kama
Jamadari Mkuu wa Jeshi ni Kulinda na Kuitetea Tanzania Kwa Nguvu Zote Umoja na Usalama wa Nchi
na wananchi wote na Kuulinda Muungano .Hotuba yake yote ilikuwa ikitilia mkazo mambo hayo.
Yeye kama Rais wa Dola,haiwezekani awe "neutral" kwa wakati huu ambapo; Tanzania imo kwenye michakato na
changamoto Ki-historia za mabadiliko msingi ya Uboreshaji wa Katiba/Sheria Mama ya sheria zote za nchi ambazo
zita husu jambo linalohusiana na maisha na uhai wa kila mmoja wetu na kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano.
Ni Political Naivity na udanganyifu kutegemea kwamba Rais awe "neutral" kuhusu Rasimu na mapendekezo ya
Jaji Warioba ,misimamo ya vyama mbali-mbali au matamko hatarishi ya baadhi ya Wajumbe na Viongozi wa
Vyama Vya Siasa nchini . Tanzania si " Kingdom au Nchi Ya Umalkia " ambako vinara wa nchi hua hawana haki
au uhuru wa kujitamka mambo ya Kisiasa kama kwa mfano Uingereza ,Japan na Badhi ya nchi za Scandinavia
Norway,Sweden na Danmark. Tanzania ni Jamhuri .Rais wa Nchi anachaguliwa na Wananchi Kwa Sera za Chama
Cha Siasa . Hivi vyama vya Upinzani wanafanya Ukaidi hata wa kutofaham tofauti baina Taifa lenye Ufalme na
Jamhuri; na dhamana za Vinara wa NCHI ?
Rais alikuwa na haki, kikatiba kusema kila alilolisema .Ikiwa aliyoyasema ,kwa bahati hii au ile yalikuwa ni
samabamba na msimamo wa CCM ,ikiwa ni kusudi au laa ;hiyo ni bahati,lakini hata hivyo ni haki na wajibu
wake kutowa hekma tulivu na busara.
Mlitaka Rais awe bubu,awe kiziwi simsimiki kisiasa wakati wapinzani ,wapinga Mapindinduzi na Muungano
manenokama haya yafuatayo:
(1).Wapinzani wanasema hadharani "Tutakwamisha Bunge kwa kila Tusichokitaka"
(2).Tutafanya ghasia Bungeni "Pakiwepo Mijadala au Mada Tusiyotaka Kuisikia.
(3).Uzalendo wa Ujanachi wa Utanzania - Tutaupinga na Kupendekeza "Uzanzibari Kwanza ".
(4).Kila kitakacho pendekezwa na CCM tutakuwa na pendekezo mbadala kwa vyovyote.
(5).Wakitaka kura wazi sisi tutapendekza kura siri.
(6).Tutahakikisha kwamba haitopatikana 2/3 kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar ikiwa Masilahi
ya Chama Cha CUF-Zanzibar hayakubaliki - Uzanzibari Kwanza Tanzania Shegesha - Yalisemwa
hayo na Jussa ,Magomeni tarehe 17 March kabla ya hotuba ya Rais.
Sasa Jamani Tumbatu,Unguja na Pemba na watu wake ni Milki Ya Chama Cha CUF- Zanzibar?.
Kwani Uzanzibari = U-CUF- Zanzibar au Uzalendo anaousema Lupumba ndio Uzalendo wa watu
wote wa Tanzania Bara ?.
Tatizo jengine na jeuri za baadhi ya Madalali wa Kisiasa wa Upinzani ni kwamba mara nyingi wao
wanaubiri-ubiri kwa kutumia neno "Demokrasia ya uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa ".
Sasa tunawauliza vereje wapige kelele /cryingfaul wakati juzi palipochaguliwa Wenyeviti 12 kati
ya viti 14 kwenda kwa CCM ? Uchaguzi wote kwa misingi hiyo hiyo ya Kidemokrasia wanayo
iubiri usiku na mchana .Wanapokosa ushindi kelele tayari ,kua eti ama wataweka lalamiko la
"Wameonewa-Umepita-Wizi-Wa-Kura". La kuchekesha hivi majuzi wamezusha jengine " Hawa
CCM ni wengi Bungeni". Suala ;Sasa hawa waliteuliwa na Chama au walichaguliwa na Wananchi?.
Badala ya kujibu suala ,na wao eti wakajibu kwakuuliza suala "Kwani Hamuoni wingi wa CCM
inaleta hali yaTyranny ya Majority ?. Sasa ikiwa logical thinking yao ipo kwenye kiwango hicho
sasa hamuoni kuwa mambo ni mazito kujadili nawatu kama hawa . Hivi fasiriya uchaguzi ni
ubiya wa kugawana na kumegeana viti na madaraka ?.
Ikiwa ni hivyo watakavyo , kwa nini wasiseme pakafanyika maridhiano au muwafaka kabla
Uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati Hizo za Bunge ;wangoje wanapo shindwa waanze hizi
kelele-kele ?.Tukumbuke kua Mwalimu alipatakuuliza "Hivi Jamani 1+1 ni Ngapi ?
Kuna waliosema 3. Palipotajwa utaratibu wa serikali na mambo 7 ya Muungano ,kuna wale
walisema "Tuuvunje Huu Kwanza ;Tujadili Shirikisho Jipya ,Kila Nchi Mamlaka Kamili Na Kwa
Nkataba ". Sasa suala Tukivunja huu Muungano tulio nao ,na kila nchi iwe na Mamlaka Kamili
sasa Mkataba wa Nini,na Kwa Mambo Gani ? Cha TanzaniaBara kiwe na Ubiya ,Ardhi za Bara
ziwe za Wazanzibari ,lakini ardhi za Zanzibar ziwe kwa Wazanzibari tu ;Hii vipi?
Jee ,Bado Wapo Viongozi Ambao Wamo Kwenye Ndoto Kurejesha ile ZenjEmpire au Vipi?
Ndimi Zao Kwa Maneno Matamu-Matamu Hayalingani Na Vitendo Vyao.
Kila Mtu Atakula Kile,Alichokipika.
Rais aliendelea kuweka bayana baadhi ya upotoshi na fitina ambazo kwa muda zilikuwa ziki pandikizwa
kwa Wananchi wa Tanzania Bara na wa Visiwani,hasa kuhusu Kero za Muungano na zile ,Hisia za Ubabe
waa Baadhi Ya Viongozi wa Ngazi za Juu ambao ndio wanao sababisha baadhiya hizo kero.
Na ndio maana ili taifa lisitokomee -inabidi Taifa la Muungano lizindikwe,lipakwe Madua Mazuri Mazuri.
Wale Wapotoshi wote itabidi Wazunguuliwe.Na wale Wenye Mashetani ya Kibuki na wenye ya Kipemba
nao Wafanyiwe Kazi Wapone.
Dawa Mbadala ya Kujadidisha Ujananchi Wa Utanzania Ipi ?
Kuboresha KATIBA ambayo ni sambamba na Sheria MAMA kwa nguvu na misingi Iliyowekwa na Waasisi kwa mujibu
wa nguzo zile zile za Mkatabawa tarehe 26 april 1964.Ikiwa Kwa Imani ya dhati Utaratibu huo utakuwa ni Dira ya
Wabunge ,basi chechele atapigwa chenga na taifa halitopotea njia kufuata akina Ifiriti na akina Ibilisi.
Wapinzani walipiga mbiu nyingi potoshi zenye ufinyu wa hisia na ushabiki wa "Ubara na Uvisiwani".
Baadhi ya wananchi Wamefitinika na maoni hayo na ni hatari.Nguvu za kelele za kuwapa Wamamchi tamaa hasa wale
wasio na kazi zimetiya nguvu mno.Ahadi za eti " Muungano wa Mkataba utafuguwa Mmimikliko wa sadaka na
misaada kutoka njee nazo zimejaa vichwani kwa baadhi ya wananchi.Tamaa za kwamba sadaka hizo ndizo weza
kuneemesha kote visiwani,na Uzanzibari utapepeya kwa bendera kwenye Umoja Mataifa na kuweka Mabalozi kote
Duniani .Zanzibar itajaa Waekezaji na wafadhili wa misaada.Kwa masharti gani ; hiyobadohaijulikani.
Makapu ya Misaada na fedha itaifanyakwa muda mfupi tu Zanzibar eti itatiya nuru iwe kama Dubai,Muskati
na Omani au alaao itashaini kama Japani au Ujerumani. Huo ndio uchawi watakao ufanya Wapinzani .
Tujiulize Matokeo ya Mardhiano Ni Nini ? Ni kweli kabisa upo utulivu na Usalama nchini.Lakini jee hii
Mivutano baridi ya kisiasa ya Kuwekeana Miyeraka katika Utekelezaji hitimayeni nini?
Kujeuriana , Kejeli nakupeana majina-majinaya ajabu -ajabu Hadharani mwishowake lini ?
Ukweli wa mambo ni kwamba,Tanzania ni ya Watanzania.Hakuna utata kwa hilo ,lakini si wote ni madalali
wa Itikadi moja;au kila mwenye wingi wa fedha afanye atakavyo kwa hasara na gharama za walio wengi.
Wenye Itikadi za Uleberali ni chaguo lao,na wale wenye itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea chaguo ni lao.
Kwa Busara na Uvumilivu Wabunge wawapatiye wananchi sheria Mama itakayo lingana na Matakwa ya
wengi ,waliojitamka pamoja na wale ambao hawajajitamka kwenye Tume ya Warioba.
Benn Haidari
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826
On Wednesday, 26 March 2014, 9:56, Salim Khatri <skhatri@orcis.com> wrote:
Deogratius,
Hili ni jukwaa la wanazuoni tofauti na kijiwe cha Jamiiforums ama forums zingine zilizojaa mashabiki wa siasa. Tutakuwa hatuufanyii haki ukumbi huu kama tutakuwa tunatoa hoja zenye kuuungwa mkono na hisia zenye kukuzwa na propaganda chafu tu badala ya hali halisi ya mambo yalivyo.
Kwanza naomba unitajie watu wenye busara unaowafahamu wewe waliokuwa wamemzunguka Prof.Lipumba. Naomba usinitajie waakina Hamad Rashid na Lwakatare (yule mwenye kesi ya kupanga kuteka mwandishi wa habari kwa sababu yuko karibu na Zitto).
Maana ya chama cha kishkaji nayoijua mimi ni kile chama kilichojaza ndugu, jamaa na marafiki kwenye ngazi za uongozi. Sasa sina hakika unaweza kuthibitisha kuwepo kwa hiyo sifa kwenye safu ya uongozi wa CUF na ningefurahi kama ungeweza kutoa uthibitisho wa hilo. La kama kuna maana nyingine ya "chama cha kiushkaji" basi ningekuomba utuelimisha kwa kutoa ufafanuzi na mifano hai.
Nafikiri tatizo lako liko kwa Mtatiro na siyo Lipumba kwani unakiri tatizo liko kwa hao waakina Bwege na Mtatiro waliomzunguka Prof. Lipumba. Naomba nikukumbushie tu kuwa kwenye uchaguzi uliopita wa 2010, CUF chini ya uongozi wa Prof. Lipumba na Mtatiro wamefanikiwa kuongeza viti viwili vya ubunge upande wa Zanzibar na viti viwili vya ubunge Tanganyika (call it Tanzania Bara). Ni CUF hiyo hiyo iliiyokuwa na wabunge wengi wa kuchaguliwa baada ya CCM. CUF hiyo hiyo Lipumba na Mtatiro ndiyo yenye madiwani na wenyeviti wa mitaa wengi baada ya CCM.
Ni hayo tu kwa leo.
Salim.
On Mar 26, 2014 12:02 AM, "mruahdeo@yahoo.co.uk" <mruahdeo@yahoo.co.uk> wrote:
Salim,Ilikuwa ni CUF ya Lipumba lakini tofauti na wakati ule alikuwa amezungukwa na watu wenye busara, sio hii KAFU ya akina Lipumba na Mtatiro na akina bwege. Hakuna maana nyingine ya chama cha kishkaji zaidi ya hiyo unayoijua. Kwa miaka mitano tu kundi la CUF ya akina Mtatiro limeitoa kule kwenye chama chenye kuleta ushindani hadi kufikia kuwa wasindikizaji katika kila chaguzi ndogo zaidi wameongeza matamko.
From: Salim Khatri <skhatri@orcis.com>;
To: <Wanazuoni@yahoogroups.com>;
Cc: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [Wanazuoni] BUNGE MAALUM LA KATIBA; TUMETOKA WAPI, TUKO WAPI NA TUNAKWENDA WAPI
Sent: Tue, Mar 25, 2014 5:25:51 PM
Deogratius,Naomba ufafanue maana halisi ya maneno "chama flani cha kishikaji"...Na kilipokuwa chama kikuu cha upinzani "bungeni" kilichokuwa kinashirikisha vyama vingine vya upinzani kuunda upinzani rasmi bungeni (tofauti kabisa na hichi cha sasa), ilikuwa CUF ya nani kama siyo Lipumba? Ama kulikuwa na mwenyekiti mwengine unayemjua wewe ambaye sisi wengine hatumjui?
On Mar 25, 2014 4:17 PM, "deogratius mruah" <mruahdeo@yahoo.co.uk> wrote:Hii tabia ya kutumia lugha za vitisho na kulalamika haijawahi na wala sioni siku za karibuni kama itakuja kuwasaidia hawa wanaojiita wapinzani nchini. Mle sahani moja, mpambane hadi kieleweke na mtumie ukubwa wenu ( as opposed to utoto CCM wanaodhani mnao) bila kuhakikisha mnapata uwakilishi mkubwa mtaendelea kuwa walalamikaji tu. Na kwa mfumo wa demokrasia ya uwakilishi hii inapatikana kwa kuchaguliwa na wananchi kwenye sanduku la kura. Na kwa CUF ya Lipumba na Mtatiro hili ni ndoto maana wanarekodi mbaya sana kwenye uongozi maana ni kipindi chao CUF imeporomoka kutoka chama kikuu cha upinzani hadi kuwa chama flani hivi cha kishikaji.
On Tuesday, 25 March 2014, 15:37, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Na Julius S. MtatiroBUNGE MAALUM LA KATIBA; TUMETOKA WAPI, TUKO WAPI NA TUNAKWENDA WAPI.1. Wajumbe wengi(asilimia 81) kati ya wale 201 walioteuliwa na Rais Kikwete ni viongozi na wanachama waandamizi wa CCM. Tukavumilia na kukaa kimya.2. Kwenye kutengeneza kanuni za Bunge Maalum CCM walipambana kila kukicha kupitisha kanuni zitakazotetea MFUMO wao - tukatumia nguvu kubwa kuwazuia lakini tulifanikiwa kidogo sana -Tukakaa kimya.3. Katika kuanza kuzitumia kanuni, Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa shinikizo la wazi la CCM alikiuka kanuni bila aibu, ikapangwa kuwa hotuba ya Jaji Warioba ianze ili aje Rais wa nchi baadaye, jambo hili ni kinyume kabisa na kanuni. Suala hili likaleta mvutano mkubwa sana tukaamua KUJIFANYA HATUTAKI MAKUU, tukaliacha - Tukakaa kimya.4. Jambo hili lilipokubalika, CCM wakamshinikiza Mwenyekiti wa Bunge Maalum amnyime jaji Warioba muda. Mwenyekiti akatangaza kuwa atampa dkk 60 tu, tukakataa, siku jaji Warioba alipokuja kuwasilisha tukalikwamisha ili aongezewe muda, baada ya mashauriano ya baadaye, ikakubaliwa apewe saa nne.5. Baada ya uwasilishaji wa Rasimu wa Warioba, Rais Kikwete alikuja na kuivunjavunja na kuweka misimamo ya chama chake dhidi ya maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba. Tukamsikiliza Rais kwa nidhamu kubwa na kuvumilia hatua yake ya juu ya kupinga hadharani rasimu ya katiba ambayo imetokana na maoni ya wananchi ambayo ameyakusanya baada ya kuiunda tume ya Warioba. Tukakaa kimya.6. Ikumbukwe kuwa hata kwenye kuchagua Mwenyekiti wa Bunge la Katiba CCM walipigania nafasi hiyo na kushinda. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti pia waliipigania wakachukua. Tukakaa Kimya.7. Jana Mwenyekiti wa Bunge la Katiba aliteua kamati za uandishi na kamati ya Kanuni. Kamati zote hizi mbili, kila moja, mwenyekiti na makamu mwenyekiti walioteuliwa wote ni viongozi wa CCM, Tukakaa kimya. Wenyeviti wa kamati hizi wote wanaingia kwenye kamati ya uongozi ya Bunge Maalum. Tumekaa kimya.8. Juzi CCM walipokutana kwenye kikao cha wajumbe wa CCM waliamua kuteka kamat zote 12 zitakazojadili sura za Rasimu ya Katiba.Jana tulipokwenda kwenye uchaguzi wa viongozi wa kamati, wateuliwa wote wa CCM walishinda akiwemo HAMAD RASHID na Dr. Francis Michael ambao pia wamejivika joho la kusimamia maoni ya wananchi huku ukweli halisi ni kuwa wapo ili kusmamia matwaka na Maslahi ya CCM.Ikumbukwe kuwa, wenyeviti wa kamati hizi 12, wote ni wajumbe wa kamati ya Uongozi ambayo ndiyo dira itakayoongoza kila jambo linaloletwa katika bunge Maalum.9. Leo, Mwenyekiti wa Bunge Maalum ameteua wajumbe watano ili kuingia kwenye kamati ya uongozi kama kanuni zinavyoelekeza. Jambo la ajabu ni kuwa, kati ya nafasi hizo 5, nafasi 4 zote amewateua wajumbe ambao ni viongozi waandamizi wa CCM akiwemo mwakilishi wa walemavu Amon Mpanju.Mjumbe mmoja wa walemavu amesimama na kupinga uteuzi wa mwakilishi wao palepale.Prof Lipumba amesimama na kukataa uteuzi huo, ameeleza si wa haki hata kidogo. Ameeleza alijiunga na siasa ili kutafuta haki za wananchi na umoja wa kitaifa na si vinginevyo. Lipumba amesema kuwa hawezi kutumika kama mhuri.Kama CCM wana nia njema wasingehodhi nafasi zote katika mchakato wa katiba.10. Hoja kubwa ya CCM kuchukua nafasi zote za uongozi wa bunge maalum ni "eti" wao ni wengi. Hoja ya ajabu sana hii! Kama hoja ni nani au kundi gani lina idadi gani basi nafasi hizi zingegawanwa kwa mantiki hiyo. Vyama visivyo CCM peke yake vina wajumbe zaidi ya 130, kama hoja ni wingi vyama hivi peke yake vingepewa nafasi 5 kwenye kamati ya uongozi. Badala yake tumepewa nafasi 1 tu a Prof. Lipumba ambayo ameikataa kwa sababu si nafasi ya haki.11. Tuko hapa kwenye Bunge Maalum kutafuta katiba ya wananchi wa Tanzania, hatuko hapa kutafuta katiba ya chama chenye wabunge wengi kuliko vyama vingine kama anavyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalum Samwel Sitta. Ili tupate katiba ya watanzania wote lazima chama chenye wabunge wengi kitambue wingi wao, na kiutumie wingi huo kuunganisha makundi muhimu yenye idadi ndogo ili kutafuta katiba yenye maridhiano na inayokubalika na makundi madogo na makubwa ndani na nje ya Bunge Maalum.12. Michakato mingi ya kutafuta katiba mpya inaonesha kuwa vyama vilivyoko madarakani huwa ni chanzo kikubwa cha kuvuruga mchakato wa katiba. Na sbb kubwa ya kuvuruga mchakato husika huwa ni chama dola kutaka kuhodhi na kulinda maslahi yake dhidi ya maslahi ya wananchi. Pamoja na uzoefu huu, bado CCM hawataki kujifunza, wanataka kushinda bila kujali wananchi watapata nini.ANGALIZO;Masuala hayo 12 yanaonesha wazi kuwa CCM hawana kabisa nia ya kuona nchi inapata katiba inayokidhi matakwa ya wananchi. CCM wanataka kuchukua kila kitu, wanataka kupata kila kitu, wanataka kuhodhi kila kitu, hawajali wananchi wamesema nini.Wasidhanie kuwa tulioko hapa Dodoma ni watoto wadogo, tutachukua hatua, hatua stahili kwa wakati muafaka. Idadi yao na wingi wao havina maana katika na juu ya maslahi ya taifa na matakwa na maoni ya wananchi.MWISHO;
CCM watambue kuwa TUTAKULA nao sahani moja, hatutatumiwa kuwa mhuri wa Maslahi ya chama chao na kwamba katiba mpya siyo hisani yao, ni matakwa halisi ya watanzania na serikali na chama kinachoongoza dola lazima kitii maoni ya wananchi na matakwa ya misingi ya kdemokrasia, na kwa sababu mchakato huu umeshaanza lazima ufike mwisho. "Jini likitoka kwenye chupa, halirudi"(hadithi za Alfu Lela Ulela).--Yona Fares MaroInstitut d'études de sécurité - SA
.
__,_._,___
0 comments:
Post a Comment