Sunday, 2 March 2014

Re: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR

Wnabidii

Naomba kidogo hebu tujadili kidogo hii hoja ya maslahi ya nchi.

Mimi ninavyoona kila mtu au kikundi cha jamii kinayo haki ya kutoa hoja yake na mawazo yake na pia kina haki ya kusikilizwa.

Hoja ninayoiona hapa kila hoja ikitoleww na CCM lazima ipingwe tena kikundi kidogo tu cha watu alimradi inatumia media kwa nguvu ma kwa fedha nyingi ili ionekane inapinga.

Kama ni kwa maslahi ya taifa tusiache wengi waamue hii ndiyo demokrasia tunayotaka ya wengi wape lakini na wachache wasikilizwe.

Binafsi sioni mantiki ya kungagania jambo linaloweza kuamuliwa na wengi hata kama wachache hawattaki. Kichaa kilichomo ndani ya demokrasia ni kuwa wengi wanaweza kuamua jambo baya hata kama wachache wanqona kuwa ni la hatari. Hatari kubwa ni kulazimisha ambako sasa kumeingia kwenye media ambazo sasa kwa nguvu zote wanalazimisha wanavyotaka wao.

Mimi mtizamo wangu ni kwamba jambo liamuliwe kwa uwazi kisha tusonge mbele. Kuna watu wanafiki tu ambao siku zote wanataka kufanya mambo kwa kificho. Hawa ni wabaya sana wanaweza kuuza nchi kwa vile wanapenda mambo ya kisiri.

Kwa nini tuamue jambo kwa siri wakati jambo linalofanyika ni la wazi na kwa maslahi ya nchi. Mimi siono mantiki ya msimamo huu wa kura ya siri.

Nadiriki kuwaita wahuni na wanafiki wanaopenda kujifichaficha. Hawa ndio wanaaoyumbisha nchi. Hata katika maamuzi yao huwa wana kauli mbili hawa. Hawaaminiki.

Hoja nyingine ni kwamba kama hupendi msimamo fulani ni vizuri ukawa wazi tu kwa nini utake kupinga kwa siri? Nani unataka aendelee kukuamini wakati haunae pamoja katika mambo ya msingi?

Kama haukubaliani naye achana naye kuliko kuendelea kumdanganya kuwa mko pamojja wakati wa usiku unamchoma. Nawapenda wazanzibari, wakati ule wa CUF na CCM kabla ya serikali ya umoja wa kitaifa ilijulikanα.



From: Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR
Sent: Sun, Mar 2, 2014 9:20:38 AM

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR SIO YA VYAMA VYENU VYA SIASA

Hivi sasa tunaingia katika hatua nyengine muhimu ya mchakato huu wa kutafuta Katiba mpya ya nchi yetu. Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshakamilisha kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo imeshatangazwa.

Wale wote waliopata fursa hii ya kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kutokea Zanzibar, kutoka katika chama chetu, katika vyama vyengine na makundi mbali mbali hawana budi kuweka maslahi ya nchi kwanza na kuweka pembeni itikadi zao za kisiasa ili wende katika Bunge la Katika kuyatetea maslahi ya Zanzibar. 

Wajumbe hao hawana budi wafahamu kwamba wazanzibari kwa muda mrefu wamekuwa wakililia suala la kutotendewa haki ndani ya Muungano huu, hivyo hii ni fursa pekee adhimu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kupigania hadhi, haki, heshma na usawa baina ya pande mbili za Muungano na hatimae kutoka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliyo bora na yenye kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Tunawaomba sana mnaokwenda katika Bunge la Katiba, nendeni mkaitetee Zanzibar na sio vyama vyama vyenu vya siasa. Wala sio kutetea maslahi ya Tanzania kwanza kama inavyosisitizwa na baadhi ya viongozi na wanasiasa wasioitakia mema Zanzibar. Tanzania ni mtoto wa Tanganyika na Zanzibar. Haiwezekani hata siku moja mtoto awe na uwezo na mamlaka ya kuweka misingi na kuwapangia mambo wazee wake, badala yake mtoto apangiwe na wazee wake. Ndio hivyo hivyo Katiba ya Shirikisho la Tanzania, mamlaka yake na mipaka yake ilitazaliwa ikiwa ni mtoto atokanae na maamuzi ya watanganyika na wazanzibari kwa namna ambavyo wanataka, na sio Tanzania ikasimu mamlaka na iweke mipaka kwa Tanganyika na Zanzibar.

Nawatakia kila la kheri na afya njema wajumbe wote wa Bunge la Katiba, wende wakaifanye kazi yao kwa uadilifu na warejee wakiwa na afya njema na Katiba bora kwa watanzania wote.

Amin.


Wasiliana na Maalim Seif: https://www.facebook.com/pages/Maali...63084730502824

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment