Mashaka Mugeta Mimi mtizamo wangu kidogo ni tofauti na huenda mtizamo wa wengi. Na hii inatokana na ukweli kwamba CDM yenyewe ilianzishwa kupambaana na CCM na hili kwaa Waliberali wote wanaona ni sawa. Sasa iweje kitokee chama kingine kiwapinge halafu kwenu isiwe sahihi? Naafikiri kidogo hapo panatia mashaka. Runakuwa na double standards. Demokrasia tunayoihubiri inakuwa na mashaka mbele ya watu wengine wanaoangalia mambo kwa ulinganisho - ina a comparative phenomenal. |
From: Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] CHAMA KIPYA CHA ACT CHASHUSHA BENDERA ZA CHADEMA KIGOMA
Sent: Mon, Mar 3, 2014 8:53:36 AM
Mimi nadhani unapoanzisha chama kipya cha siasa kwa mlengo wa 'kukishughulikia' chama kingine kilichopo, unakuwa unapotoka. Kwa maana ukishakishughulikia hata mwisho wa kushughulikia ukafika, bado kikawa imara, utafanya kazi gani? Ama ukikishughulikia na kikashughulikiwa hata kufikia ukomo wa kutoweka, itachochea nini uhai wa chama kipya? Mtazamo wangu ni kwa ACT wajipande katika mambo yaliyo msingi kwa ujenzi wa chama cha siasa na si kujielekeza zaidi katika kushughulikia chama kingine cha siasa. Watakuwa wanapotea njia. HAYA NI MAWAZO HURU NA SIMO KWA CHAMA CHOCHOTE KATI YA HIVYO AMA KINGINE CHOCHOTE KATIKA TANZANIA On Sunday, March 2, 2014 11:57 PM, Mabadiliko Tanzania <mabadilikotanzania@gmail.com> wrote: Na Magreth Magosso, Kigoma. CHAMA cha Alliance For Change and Transparency Mkoa wa Kigoma,kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Ujiji stendi ya zamani na kupandisha bendera ya (ACT) wakati wa uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji. Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho na hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja. Kabogo aliwataka wanachama wahitaji, wachukue kadi za ACT ili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu ,ikiwa ni jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbele kwa maslahi ya Taifa. "Wananchi nyie ni chachu ya chama kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kukiamini na kukipatia ridhaa kiweze kuleta mabadiliko ya kimaendeleo" alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma. Kwa upande wa Katibu ACT Kanda Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa siasa,ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi. Katika ziara hiyo ya uzinduzi wa matawi ya chama husika,ACT kimefanikiwa kufungua matawi kwenye kata sita kati ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji,huku baadhi ya viongozi kutoka UPD,CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hicho kwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge. Hata hivyo wanachama 3500 wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia chama kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT). Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment