Friday 1 November 2013

[wanabidii] Katiba Mpya – Pigo Jengine kwa Wapinzani

Watanzania wengi walidanganywa na Rais Kikwete kuwa amendments za mswada wa mabadiliko ya katiba mpya yaliyoletwa mzozo Bungeni na baadaye yakafanya mpaka Rais Kikwete kukutana na wapinzani, kuwa yatapelekwa bungeni katika kikao kijacho. Mswada haujapelekwa Bungeni

Watanzania wengi waliamini hivyo, na wpainzani nao waliingia katika dema hili na wakavuliwa kama vidagaana mfumo wa CCM.Wameingia kichwa kichwa, na wamezama kichwa kichwa.

Bunge limeanza kikao, na Bunge limethibitisha kuwa waraka huo au document hiyo haimo katika agenda za kujadili katika kikao hichi. Hii bill au hizo amendments hazimo, na maana yake hazitatajwa. That means, wapinzani wamepigwa bao, na wamedanganywa. Na CCM inasonga mebele.

Ina maana pia kuwa sifikiri kama hizo views za wapinzani, na wazanzibari zinaingizwa katika hiyo bill /amendments tena na tena. TUMEPIGWA BAO! na goli la tik tak hilo.

Hii sisemi mimi, Bunge jana limetoa taarifa rasmi kuwa hakuna bill kama hiyo iliyowasilishwa bungeni kwa kujadiliwa.

Inanishangaza sana kuona wapinzani wakiwemo 'maprofessa' wamedanganywa kirahisi kiasi hicho.

Tujue kuwa timeline ya kazi hii ya kupata katiba mpya ni kuwa novemba 2013, inatakiwa liundwe bunge la katiba (constitutional assembly); je bunge hili linaanzishwa vipi wakati mambo muhimu ya kujadiliwa hayatakuwemo?

Rais Kikwete yupo London, au mtaambiwa kuwa ataporudi atakutana tena na wapinzani kwa majadiliano zaidi, au mtaambiwa kuwa bunge la katiba ndilo litajadili hili, kitu ambacho si kazi yake, na haitakiwi kufanya hivyo, na kinyume cha sheria. Au mtaambiwa kuwa 'mambo kidogo kidogo' — hakuna haraka na TZ ni nchi ya amani ya utulivu.

Kikwete yupo London, kuhudhuria mkutano wa mambo ya 'good governance na transperency'. Nchi yake inanuka rushwa (jana kuna report imechapishwa kutoka utafiti uliofanywa na kusema kuwa TZ inaongoza kwa rushwa afrika mashariki na hasa polisi)

Tunachezewa akili, na tunakubali sana.

Hivi kweli wapinzani wlaikuwa hawajui kuwa by the time wanakutana na Kikwete alikuwa ameshainini hiyo bill na kuwa sheria, ingawa waowaliambiwakuwa 'Kikwete hajatia saini' na wapinzani wetu na hasa Zanzibar walikuwa wanasema hivyo.

Hivi Professa Lipumba, Jussa, Maalim Seif, Mbowe nk hawajui kuwa bill ikishapita bungeni, kuna siku 21 lazima rais atie sini ili iwe sheria?

Inasikitisha sana kuwa na viongozi wa aina hii, hawajui hata ABCD ya sheria, kanuni za bunge na mfumo mzima wa utawala katika nchi. Very sad!

Basi akina Lipumba wanshindwa hata kuwa na calendar ofisini mwao na kujua lini bunge limepitisha ile bill, kuanzia hapo hesabu siku 21.

Tumepigwa BAO, tumedaganywa na kwa Zanzibar TUNAZAMAKWA KATIBA MPYA. NCHI INAPOTEA, INATUTOKA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment