Thursday, 28 November 2013

[wanabidii] Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto

Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto

SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING

"Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake." Baregu  

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba29  2013  saa 8:34 AM

KWA UFUPI

  • Aitaka itafakari madhara yanayoweza kukikumba, asema ni vigumu kuamini kama tuhuma dhidi yake na wenzake zinaweza kuyeyusha mema waliyokitendea.
SHARE THIS STORY
  
 
0
Share

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare alisema chama hicho kipo imara na hakiwezi kuyumba kwa sababu ya uamuzi huo.

Lwakatale ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema: "Mfumo wa ulinzi ndani ya chama upo imara, yakitolewa maelezo na ngazi za juu kinachofuata baada ya hapo ni utekelezaji."

Alisema kilichotokea ni kitu cha kawaida na ni mwanzo wa chama kujiimarisha.

Temeke wapinga

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Chadema hicho Wilaya ya Temeke wamepinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa viongozi hao.

Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Temeke, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, Joseph Patrick aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mgogoro huo haulengi kujenga chama, bali unakibomoa.

"Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia uchaguzi wa ndani. Hii inasababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika kwa lengo la kuwadhoofisha mbele ya wanachama," alisema na kuongheza:

"Tumeona mifano mingi ya namna hii. Wakati Chacha Wangwe akiwa hai alipotangaza kuwania uenyekiti, mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote na hakuwahi kusemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama, bali viongozi wenzake waliotofautiana kimsimamo."

Alisema hali hiyo ilijitokeza pia kwa Zitto alipotangaza kuwania uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa chaguzi za viti maalumu na mabaraza ya chama.

Alisema ni vyema viongozi wakaitisha mkutano mkuu wa dharura na kuwaeleza wanachama mambo mbalimbali ikiwamo ni kwa nini wameamua kusambaza waraka ambao alisema unakidhalilisha chama badala ya waliouandika.

Katibu Chadema ahojiwa

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Herry Kilewo amehojiwa na Polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na madai ya Zitto kutishiwa kuuawa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment