Saturday 30 November 2013

[wanabidii] Taarifa ya Mabadiliko katika Jeshi la Polisi Tanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema   amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na  wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa Nchini. 

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu  wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake  inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha  kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

 Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa  mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na 
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa  makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona  amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na  nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka  Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging'ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa  Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP  Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa  Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa  wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.  

Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa  mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi. 

Imetolewa na: 
Advera Senso-SSP 
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment