Saturday, 30 November 2013

[wanabidii] UJUMBE WANGU KWA SIKU YA UKIMWI DUNIANI 2013

UJUMBE WANGU KWA SIKU YA UKIMWI DUNIANI  2013


Ndugu zangu ,


Kesho ni siku ya ukimwi duniani , kwa wanaofuatilia vyombo vya habari watakuwa wameshapata habari za hapa na pale kuhusu siku hiyo .


Kwa upande wangu wapenda kuwasihi watu haswa vijana wenzangu kujenga utaratibu wa kuangalia afya zao ili kujijua kabla ya kufanya baadhi ya maamuzi ambayo wanaweza kujutia katika maisha yao au kwa watu wengine ambao wanaweza kuathirika kutokana na mmoja kupata maambukizi .


Sio kweli kwamba kila muathirika ameambukizwa kutokana na kushiriki ngono ambazo sio salama , wengine wanafanya ngono salama na wapenzi wao au wanandoa wenzao na wanaambukizana wengine ni kwenye shuguli zao za kila siku kama mahospitalini wengine kwenye ajali .


Pamoja na kuathirika naamini kila mmoja katika jamii kwa kutumia nafasi yake au fursa aliyonayo anauwezo wa kupunguza maambukizi au kushinda vita hii katika maisha yake .


Kwa wale wafanyakazi wajue waajiri wao bado wanawapenda bado wanahitaji mchango wao katika shirika au kampuni husika .


Kwa wale kina baba au mama wajue bado wanahitajika kutunza familia zao haswa watoto wao waliowazaa wenyewe , wajipe muda kuongea na watoto wao kuhusu suala hili .


Kwa wafanyabiashara wajue serikali inahitaji kodi yao kutokana na biashara zao , watu wanahitaji ajira kwa wingi , unapoumwa au kufariki mapema basi ndoto nyingi zinapotea .


Kwa wanafunzi wajue wanahitajika kusoma kwa jitihada ili wawe kwenye kundi bora kati ya hayo hapo juu .


Kwa waathirika wasikate tamaa wanaweza kuendelea kutumia dawa na kufuata ushauri wa madaktari wataweza kuishi muda mrefu zaidi .


Kwa walimu wajue wao ndo wazalishaji wa wote hapo juu , wafanyakazi , wafanyabiashara , wanafunzi  , viopngozi na watu wa aina mbalimbali tunategemea wao wawe na maono zaidi kuhsu suala hili .


Kwa wengine wote , poleni kwa kupoteza ndugu , marafiki na majamaa kutokana na janga hili – tafadhali tuendelee kutoa elimu zaidi , tuendelee kuvumiliana na tuendelee kujenga taifa letu .

 

YONA FARES MARO

0786 806028 


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment