Friday 29 November 2013

Re: [wanabidii] Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaongezewa muda ili ikamilishe kazi yake

kwa aliye tayari kujadili maswala mbalimbali yahusuyo mambo ya katiba katika kipindi cha hot mix ya eatv, tuwasiliane kupitia 0715 56 86 53

2013/11/27 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiongezea Tume ya Mabadiliko ya Katiba siku 14 zaidi kuanzia Desemba 16, mwaka huu, 2013, ili kuiwezesha kukamilisha kazi yake.

Rais Kikwete ameiongeza Tume hiyo muda zaidi kufuatia maombi ya Tume yenyewe na kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ameongeza muda wa Tume hiyo kufanya kazi kuanzia Desemba 16 hadi 
Desemba 30, 2013.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi yake. Kufuatia maombi ya kwanza, Rais Kikwete aliiongezea Tume hiyo muda wa siku 45 kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu, 2013.

Chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa miezi 18. Aidha, sheria hiyo inampa Rais mamlaka ya kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi usiozidi siku 60.

Kwa uamuzi wake wa kuiongezea Tume hiyo siku nyingine 14, Rais Kikwete atakuwa ameiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi wa jumla ya siku 59 kati ya 60 ambazo anaruhusiwa kisheria kuiongezea Tume hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

27 Novemba, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment