Yona,
Siasa za siku hizi mtu huwa mwakilishi wa nani? Zamani mtu huwa mwakilishi wa wananchi waliomchagua na chama kilichomwingiza madarakani! Siasa za Tz inasukumuwa kwa kiasi kikubwa na motisha wa fursa na maendeleo ya mtu binafsi na familia yake. Hii ni kwa vyama vyote. Wanaochaguliwa kushika nyadhifa katika vyama vyote huwa na vipaumbele vyao binafsi na vya serikali. Ila vyao binafsi hutangulia maana nani ajuaye kama baada ya fursa hii kwisha kama uchaguzi mwingine utapewa hiyo nafasi? Kwa hiyo sera ni chukua chako mapema maana kufa kwaja kesho! Mikataba isainiwe haraka na ifanywe siri maana una chako majuu! Kenya wanaimba nchi ya kitu kidogo lakini sisi ni nchi ya kitu kikubwa maana tulikuwa tumelala enzi za udikteta wa siasa za ujamaa na chama kimoja. Tumeona wenzetu kajirani wakihodhi uchumi wa nchi hasa ardhi! Sasa sisi tunakimbia kulimbikiza wakati wenzetu wamemaliza ardhi yao! Ufisadi hugeuka kuwa mkakati wa kufikia malengo binafsi kwa kushindana kuwekeza katika nyanja zote zenye hela kama hoteli, vipusa, shule binafsi nk! Mungu ibariki Tanzania kwa kuwafungua macho na kutoa matongotongo ya usukule wa ndio mzee! Hata mifumo ya imani inaingia kwenye siasa na mabenki na huko misukule inaangalia? Tunahitaji kufufua misukule hata kama ni kuwakodi akina "Gwajima!" Mwizi akikamatwa lazima atalipa mara saba! Hiyo ndio kanuni!
On Thursday, 28 November 2013, 14:54, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
CHAMA CHA CHADEMA NI SERIKALI KIVULI YA TANZANIA NA TUMEONA BAADHI YA WABUNGE ZAKE NI MAWAZIRI VIVULI KWAHIYO HII NI SERIKALI KIVULI - UNAPOJARIBU KUPINDUA UONGOZI WAKE AMBAO NI HALALI MAANA YAKE UMEPINDUA SERIKALI HIYO HUO NI UHAINI .--PIA KAMA WEWE NI KIONGOZI WA UPINZANI UKAKUBALI KUTUMIKA KAMA ILIVYO KWA ZITTO , MWIGAMBA NA KITILA KWA NAMNA YOYOTE HATA WAKIVULIWA UONGOZI CHADEMA HAWATOAMINIKA NDANI YA VYAMA VINGINE NA HATA SERIKALI HAITOWAAMINI HASWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA .HATA IKITOKEA WATU KAMA HAWA WAKAPATA FURSA YA KUONGOZA NCHI KUTOKANA NA TUHUMA KAMA HIZI NI RAHISI KUONDOLEWA MADARAKANI AU KUSABABISHA MATATIZO YA KIUSALAMA .UJUMBE WANGU WA MWISHO NI HUU .KAMA KWELI WALITUMIKA KUHUJUMU CHAMA CHAO KWA NAMNA YOYOTE ILE WAJUE HATA HAO WALIOWATUMA AU KUWAFADHILI HAWATOWAPOKEA KWA SHANGWE , WATAKUONDOA TU
On Thursday, November 28, 2013 5:32:32 PM UTC+3, xavery njovu wrote:Tafsiri ya pili
Ilikuwa inawatia hatiani watu wengi na adhabu ya uhaini ni kifo auOn Nov 28, 2013 5:10 PM, "Magiri paul" <kig...@gmail.com> wrote:
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment