Saturday 30 November 2013

RE: [wanabidii] Kesho Nitahutubia Kwa Mara Ya Kwanza Kijijini Kwetu Nyeregete...!

Maggid,

Ndio unaanza kujipanga? Au vipi?  Ninakutakia kila la heri

Herment A. Mrema


Date: Sat, 30 Nov 2013 00:04:01 +0300
Subject: [wanabidii] Kesho Nitahutubia Kwa Mara Ya Kwanza Kijijini Kwetu Nyeregete...!
From: mjengwamaggid@gmail.com
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com

Ndugu zangu,

Matukio mengine ni ya muhimu katika maisha ya mwanadamu. Kesho Jumamosi nitahutubia kwa mara ya kwanza kijijini kwetu Nyeregete. Ni kijiji alichozaliwa baba yangu. Naisubiri kwa hamu siku ya kesho.

Ni kijiji nilichocheza utotoni kila nilipopata likizo ya shule. Na kesho nitasikilizwa na ndugu na jamaa wa kijijini kwetu.

Ni kwenye tukio la harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kikundi cha wanawake kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi kwa shughuli za kilimo.

Nitaongea kuhusu elimu na maendeleo. Watu wengi wakiwemo wazee wa kijiji wamealikwa. Na pengine hakuna hotuba ngumu kama ya kuhutubia kijijini kwenu. Si wamesema, nabii hakubaliki kwao.

Natumaini hakuna atakayenirushia yai viza!

Usiku Mwema.

Maggid.
Iringa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment