Saturday 30 November 2013

Re: [wanabidii] Mtoto Mtanzania ashinda insha EAC

Nachukua nafasi hii kumpongeza sana kijana Peter kwa ushindi huo mzuri na wa kujivunia.

Pia nawapongeza wazazi, walimu na walezi wa Peter kwa malezi mazuri ya kijana huyo.

Penye nia siku zote pana njia, watanzania tujenge tabia ya kuthubutu na kushiriki katika mambo mbalimbali makubwa hususani ya kimataifa ili kuongeza nafasi ya nchi yetu kujitangaza nje ya mipaka yetu.

Wapo watanzania wachache huwa wanajitokeza kushiriki katika mambo ya kimataifa yenye ushindani na ni wachache zaidi huwa wanafanikiwa, tuna haja ya kuhamasishana ili tushiriki zaidi hususani katika nyanja za kitaaluma, kazi, biashara, burudani na michezo.

Na wachache ambao hujitokeza baadhi badala ya kuwapongeza na kuwatia moyo mara nyingine tunawabeza pale wanaposhindwa au wanapoteleza kidogo, tuwe chanya zaidi, tushirikiane, tutiane Moyo na tutafanikiwa zaidi.

Mungu Mbariki Peter afanikiwe zaidi,
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika Mashariki,
Mungu ibariki Afrika.

Phares Magesa.


Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

From: matinyi <matinyi@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 30 Nov 2013 19:31:28 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>; <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Mtoto Mtanzania ashinda insha EAC

Peter Robert Kilave, mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Tushikamane ya mjini Morogoro, amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika shindano la insha kuhusu ujenzi wa miundombinu Afrika Mashariki. 

Amepewa tuzo ya dola za Marekani 1,500 na cheti na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. 

Hiyo ilikuwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC jijini Kampala, leo Jumamosi, Novemba 30, 2013. Rais Jakaya Kikwete alimwita jukwaani na kumpa mkono wa pongezi huku ukumbi ukizizima kwa shangwe. 

Kijana huyo mtanashati na mpole alijizolea dola zingine kutoka kwa viongozi na maafisa wa Serikali ya Tanzania kwa kuibeba Tanzania katika kipindi hiki chenye changamoto za ajabu ajabu ndani ya Jumuiya.

Mshindi wa pili alitoka Uganda; wa tatu Burundi; wa nne Rwanda na Mkenya alishika mkia. 

Dogo huyo wa Tanzania ataendelea kuvinjari nchini Uganda kwa siku ili wamwone kwa karibu zaidi. Atakuwa na maafisa wa EAC, afisa mwandamizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Tanzania pamoja na mwalimu mkuu wake.

Hongera Watanzania wote.


Matinyi.


From my Android phone on T-Mobile. The first nationwide 4G network.

0 comments:

Post a Comment