Saturday 30 November 2013

[wanabidii] MIKOA SABA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUINUA UBORA WA ELIMU NCHINI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA
Novemba 29, 2013
MIKOA SABA  KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUINUA UBORA WA ELIMU NCHINI  


Katika kuinua ubora wa elimu nchini, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la Department for International Development (DfID) itaanza kutekeleza Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu nchini [The Education Quality Improvement Programme in Tanzania (EQUIP – Tanzania)] kuanzia mwaka ujao, 2014.

Mikoa itakayonufaikia na mpango huu wa miaka minne (4) katika awamu ya kwanza kuanzia mwaka 2014 ni Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Awamu ya pili itaanza mwaka 2015 na kuhusisha mikoa ya Mara na Lindi.  

Mpango huu una lengo la kuinua ubora wa elimu ya msingi na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari hasa wasichana. Aidha, mpango huu  utanufaisha wilaya 36 zenye shule za msingi zaidi ya 4,000 za serikali katika 
mikoa hiyo ambao utasimamiwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na TAMISEMI.

Akizungumzia utekelezaji wa Mpango huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome  amesema kuwa mpango huu utasaidia kuinua kiwango cha ubora wa elimu katika mikoa husika.

'Tunaanza na mikoa hii ambayo baadhi yake imekuwa ikifanya vibaya katika matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ili kuhakisha kuwa ubora wa elimu unaimarika na hatimaye kuongeza ufaulu wa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari,'  anasema Profesa Mchome.

Mpango huu wa Kuinua Ubora wa Elimu utatoa mafunzo kazini kwa walimu kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kitaalam na kuongeza ufanisi katika kufundisha na kujifunza, kuimarisha mbinu za usimamizi na uendeshaji wa shule, kuimarisha mifumo itakayosaidia usimamizi wa elimu katika wilaya na mikoa, kuimarisha ushiriki wa jamii na kuhimiza uwajibikaji  katika masuala ya elimu.

Ni matumaini ya Wizara kuwa wadau wote katika Mikoa na Wilaya husika watatoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa mpango huu. Lengo ni kupata Matokeo Makubwa Sasa.

Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment