Sunday, 3 November 2013

Re: [wanabidii] Zitto Kabwe - Ninakerwa na Siasa za Majungu CHADEMA

wanassiasa ndio zao kutoana kafara,kuchongeana na vitukama hivyo, zoote hizi ni siasa chafu za bongo....hakuna cha cdm, cuf wala ccm wote mambo ni yale yale



On Wednesday, October 30, 2013 5:41 PM, Francis Kasili <Francis.Kasili@nmbtz.com> wrote:
Ndugu wana jukwaa inabidi kuwa makini sana katika kutoa comments kwani mwaweza kushabikia sana vitu ambavyo baadae mtajagundua kuwa ni uzushi mtupu! Toeni kwanza mwanya wa pande zinazotuhumiwa au ikiwezekana mfanye uchunguzi wa kina ili baada ya hapo mtu apate jambo na hoja yenye nguvu ya kuongea. Hapa cha kujiuliza ni kwa nini mambo yote haya yanatokea kwa sasa wakati uchaguzi wa CDM ndio umekaribia sana? Mimi naamini if we go an extra mile ni lazima utagundua there is something behind the curtain.
 
Regards
F.Kasili
Mob: 0784850583 or 0755850583
Always darkness will never comprehend light

From: wanabidii@googlegroups.com [wanabidii@googlegroups.com] on behalf of mchangehabibu [mchangehabibu@yahoo.com]
Sent: Wednesday, October 30, 2013 4:55 PM
To: ELISA MUHINGO; wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Zitto Kabwe - Ninakerwa na Siasa za Majungu CHADEMA

Majungu Ndio mtaji wa siasa ndani ya chadema. Bila majungu hakuna chadema Ndio maana kunazuka mpaka migogoro ya kutengeneza.
Kuna watu ndani ya chadema kazi yao ni kutengeneza migogoro tu.

Ndio maana hoja zao mara zote hazinaga mashiko mbele ya watu wenye akili zao timamu.

Ninafahamu ni jinsi gani baadhi ya vongozi wa chadema wanatumia nguvu kubwa kumkandamiza zitto, bahati mbaya tu kwao ni kwamba zitto yeye kwenye siasa za Tanzania ni kama maji, usipo mnywa basi utamuoga, usipomuoga utamuoshea vyombo tu.

laiti kama zitto angekuwa mwnasiasa mwepesi ndani ya siasa za Tanzania, Nina hakika mpaka Sasa tungeshamsahau.

Ama kama watu wote tungekuwa tunawaza kama waavyowaza wapinzani wa zitto kwenye chadema, Nina imani Leo hii tusingekuwa naye kwenye ramani ya harakati hai.

Wa kuwa ninazifahamu hiatoria nyingi za viongozi wengi waliofanikiwa kisiasa dunani, ninaamini zitto anakwenda kufanikiwa. Vikwazo anavyowekewa ni vyepesi kuliko uwezo wake wa kuvitatua.

Kila la heri zitto.
Changamoto kwako Ndio mafanikio yako.
Regards

ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:

CHADEMA; CHADEMA CHADEMA!
Wananchi watasikitika sana mkikubali kuvurugwa. Wakati wa uongozi wa awamu ya pili Augustine Mrema alilisaidia taifa kwa kubaki na matumaini kuwa anaweza kuleta mabadiliko hadi vyama vingi vilipoingia.
Kwa kipindi hiki moja kati ya matumaini ya Watanzania ni vyama vingi kuleta mabadiliko nchini. CHADEMA ni moja kati ya vyama hivyo vinavyotazamwa na Watanzania kwa matumaini.
Zitto. Unafanya kazi kubwa sana na watanzania wanaifuatilia kwa makini. Ufuatiliaji wa pesa zetu zilizoibiwa na kufichwa nje. Ni haki kweli kuwa CHADEMA inaweza kukukatisha tamaa. Usithubutu kukata tamaa ndani ya Chama wala harakati zako.
Haraka tatueni migogoro hii na tunawategemea sana.
Tunawasihi sana Mbowe; Slaa na wengine wote acheni kuparurana. Galatia 5: 13-15.

From: Pauline Mengi <paulinemengi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 30, 2013 1:18 PM
Subject: [wanabidii] Zitto Kabwe - Ninakerwa na Siasa za Majungu CHADEMA

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ameelezea kukerwa na siasa za majungu na vikao vinavyoishia kupigana ndani ya chama chake na badala yake amewataka viongozi wenzake kuelekeza nguvu kwa wanachama, kwani malumbano hayatakijenga chama.

Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alitoa kauli hiyo jana, baada ya RAI Jumatano kutaka kujua msimamo wake kutokana na kuhusishwa kuwa nyuma ya usaliti anaodaiwa kuufanya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Katika majibu yake hayo aliyoyatoa kwa njia ya mtandao, Zitto alisema wanaojaribu kumhusisha na suala la Mwigamba ni kawaida yao kupenda kumhusisha na mambo yasiyomhusu.

"Mwigamba ni Mwenyekiti wa chama wa Mkoa mwenye utashi wake wa kisiasa. Ana uwezo wa kusimama mwenyewe. Siyo kila mtu mwenye mawazo yake anatumika. Sasa hao wanaomtuhumu Mwigamba wao wanatumiwa na nani?" alihoji Zitto. 

Kuhusu hoja kwamba sakata hilo la Mwigamba chanzo chake ni msuguano wa kuwania nafasi ya uenyekiti kati yake na Mbowe, Zitto alisema uchaguzi ndani ya chama haujatangazwa, kwa hiyo yeyote anayezungumzia kugombea au la anavunja kanuni za uchaguzi.

Katika hilo, Zitto alisema hahitaji mtu wa kumsemea, kwamba akihitaji uenyekiti wa chama atasema yeye mwenyewe.

"Nina sifa zote, siyo tu za kuongoza chama, bali kuongoza nchi. Nina elimu ya kutosha, nina rekodi ya kazi za kibunge kubwa kuliko wabunge takribani wote wa sasa, kwa miswada binafsi, hoja binafsi na hata kuibua masuala nyeti ya nchi.

"Uadilifu wangu hauna shaka, uzalendo wangu kwa nchi yangu ni wa kupigiwa mfano. Zaidi ya yote, najua kero za wananchi na changamoto zao. Sihitaji kusemewa na mtu. Nikitaka uenyekiti nitasimama mwenyewe," alisema Zitto. 

Zitto alisema kitendo cha kutaka kumhusisha na masuala yanayoendelea ndani ya Chadema na kuhusu sakata zima la Mwigamba, ni kutaka kuhamisha mjadala na kumtoa kwenye ajenda ya kuwafuatilia watu wanaodaiwa kuficha mamilioni ya fedha nje ya nchi. 

"Kwa sasa nina kazi ya kuhakikisha mafisadi na wahuni 'criminals' walioficha fedha na mali nje ya nchi wanaibuliwa na kurejesha fedha hizo," alisisitiza Zitto. 

Kuhusu madai ya kuchunguzwa na chama chake kama na yeye ni mmoja wa wasaliti, Zitto alisema kuwa hizo ni mbinu za kumuondoa kwenye kazi anayofanya ya kupambana na ufisadi. 

"Wanajua nikishika jambo siachi mpaka mwisho, hivyo wanajaribu kutengeneza uongo wanaouita uchunguzi. Watanzania wasipumbazwe na vituko vya siasa vinavyoendelea. Tuendelee kudai Katiba Mpya na kupambana na ufisadi. Kwa Wanachadema tuendelee kujenga chama kwenye kanda zetu. Chama kitakachochukua dola ni kile chenye mtandao mpana kwenda vijijini," alisema. 

Zitto aliwataka viongozi wenzake na wanachama wa Chadema kupunguza vikao vya majungu vinavyoishia kupigana na badala yake waende kwa wananchi wakafanye kazi, kwamba malumbano hayajengi chama.

Kwa upande mwingine, chama hicho kimeendelea kusisitiza kuwa madai yote yaliyotolewa na Mwigamba dhidi ya chama chao ni ya upotoshaji, uongo na ya kichonganishi.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari Mwandamizi wa chama hicho, Tumaini Makene, wameshangazwa na hatua ya Mwigamba kuendelea kuvunja katiba ya chama kwa kutunga mambo yasiyokuwepo, badala ya kuwasilisha hoja zake kupitia vikao halali vya chama.

Alisema kwa kuwa Mwigamba amekiri mbele ya waandishi wa habari kuwa amevunja katiba ya chama na kukubali kuwa aliandika kwa kutumia jina bandia waraka na kuuweka kwenye mitandao ya kijamii, ni wazi hana lengo zuri na chama chao, hivyo apuuzwe.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
*************************************************************************************** *************************************************************************************** This e-mail and any attachments are proprietary to NMB PLC. Any unauthorized use or interception is illegal. The views and opinions expressed are those of the sender, unless clearly stated as being those of NMB PLC. This e-mail is only addressed to the addressee and NMB PLC shall not be responsible for any further publication of the contents of this e-mail. If this e-mail is not addressed to you, you may not copy, distribute or disclose the contents to anyone nor act on its contents. If you received this in error, please inform the sender and delete this e-mail from your computer.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment