Sunday 3 July 2016

Re: [wanabidii] Wapinzani kutoka bungeni ni mkakati wa kimakosa

. . . . . . Hakuna asiyekubaali kuwa nchi hii imeundwa juu ya misingi ya Sheria.
Hakuna jambo lolote katika jamii yetu ambalo likitafsiriwa tofauti na upande wowote haliwezi kutafutiwa ufumbuzi katika Mahakama zetu na ikibidi hata mahakama za Africa au Zaidi ya hapo . . . . . 
naamini Wabunge wanao susia vikao vya bunge hawaja tafakari kwa kina mbinu za kufanya kila panapo kuwa na hoja ambayo wao hawaikubali . . . . Aidha iwapo Spika au mbunge mwingineo hajawatendea Haki bado wanazo njia za kisheria kuweza kudai haki zao.

Ni aibu sana kuna kuwa hawa wabunge wanao toka nje na kususia vikao vya Bunge hawaelewi kuwa Bunge ndio sehemu ya juu kuliko zote katika kutoa, kujenga, kupinga na kupambana kwa kutumia Hoja.
Hta hawaelewi kuwa Hoja ndizo zinazo pelekea kutungwa kwa Sheria!!

Bunge sio Ndoa, ambao usiporidhika na mwenzio unahama kitanda au chumba na kusubiri jazba zako zipungue.
Bunge ni baraza ambamo unasikiliza Hoja za mwingine na ewe kupinga au kuunga mkono kwa njia ya Hoja bora zaidi. Bila utaratibu huo sidhani tungeweza hata kutunga hizi sheria zinazo tuongoza. . . . .  ni wazi kuwa wapo wabunge ambao bado hawaelewi kuwa hata kupitisha Bajeti ya Nchi ni kuidhinisha sheri za kutuongoza sote  . . . . .  .
na Msingi wa kwanza wa demokrasia ni kukubali kusikiliza Hoja na kuipinga au kuikubali kwa Hoja.
Kushindwa kuelewa au kukubali kuwa Demokrasia ni Hoja ni sawa na kushindwa kuishi katika Utawala wa Kidemokrasia 


On Sunday, July 3, 2016 10:01 PM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Maggid nakushukuru kwa utulivu mwanzao mwisho wa kuandika makala hii. Limetushinda wengine tukawa na jasba. Lakini ukweli uko pale kuwa wapinzani wamefanya kosa na kosa kubwa. Ukweli halitawagarimu wao bali watanzania maana upinzani ni kwa manufaa ya watanzania wote.
Wangetoka siku ya kwanza wakarudi wangeeleweka. Kwa sasa inakuwa ngumu hata kuwasikiliza kwa jinsi walivyofululiza vituko kadri walivyochezewa kwa Saibu spika kuendelea kuongoza vipindi. Huko tuendako uchaguzi unaweza kuelemea upande mmoja. Hii sio afya kwa ustawi wa taifa letu. Huenda nitafaa sasa wapinzani wakaamua kurudi bungeni bila mjadala maana uweje Mjadala wowote wataonekana walikosea.
--------------------------------------------
On Sun, 7/3/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Wapinzani kutoka bungeni ni mkakati wa kimakosa
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, July 3, 2016, 5:53 PM

Maggid
Mjengwa
KWENYE Jamhuri mengine hayawezekani kubadilishwa
kwa wabunge kutoka tu
kwenye vikao vya Bunge.  Kuna wakati mbunge Tundu Lissu
hakuonyesha
kumtambua Rais. Ni hivi, kwenye Jamhuri Rais akishaapishwa
ndio
ameshakuwa Amiri Jeshi Mkuu.
  Hii ndio tafsiri halisi ya jambo hilo.

Yawezekana, mwingine akaona, kuwa aliyeapishwa si Rais wake,
nalo
haliwezekani, kama Rais atakula kiapo kulitumikia Bunge la
Jamhuri,
basi, huyo ndiye rais pia kwa  wabunge waliomo bungeni, ni
kwa miaka
mitano ijayo.


Maana, unaposema Jamhuri haina Rais una maana
Jamhuri haina pia Amiri
Jeshi Mkuu. Na kwenye Jamhuri ambapo unaweza kusimama na
kusema hayo na
kurudi nyumbani kwa amani na utulivu, basi, ujue Jamhuri
hiyo ina Rais,
na hivyo, mfumo wa kidola unaoheshimu haki za raia kujieleza
kwa uhuru
na hata kulindwa dhidi ya watakaochukizwa na kauli zao.


Tukaona wakati ule, kuwa  Rais alihutubia Bunge,
kuna wabunge wa
upinzani wakaleta rabsha za hapa na pale, na kuna waliotulia
kumsikiliza
  Rais wa Awamu ya Tano alipotoa mwelekeo kwa taifa.


Kilichopo sasa, wabunge wa upinzani wanatoka
wakimsusia Bunge Naibu
Spika, Dk. Ackson Tulia. Swali la kujiuliza; Unafanyaje na
Naibu Spika
aliyechaguliwa na wabunge wenyewe na kuapishwa?


Hakika swali hili lilipaswa wajiulize wabunge wa
upinzani wenye kutoka
bungeni kila baada ya dua ya asubuhi. Kwa kufuatilia kwangu
siasa za
nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi
kwa sasa,
naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.


Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa
wapinzani huko tunakokwenda
kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi bungeni.
Unapopanga
kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo
husika. Kwa
sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na
mengineyo, wapinzani
kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza
ingeeleweka
kwa wapiga kura.


Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya
siku ya kazi za Bunge
walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga
hisia
miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni
kukosekana kwa
umakini.


Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na
hakika nilisikitika moyoni.
  Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya
Watanzania kuwa
na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama
yale.

Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni

tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika
nafasi yake na
  ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa
mujibu wa kanuni,
sheria na taratibu zetu kimfumo.


Kama mbunge hamtaki au hampendi Naibu Spika,
hakuna anayemlazimisha, nje
  ya Bunge, kumwalika Naibu Spika kwenye kipaimara cha
mwanawe au sherehe
  ya Maulid.


Na kimsingi, yanapotokea mapungufu ya kimfumo
ndani ya kanuni, sheria na
  taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za
kuyabadili hayo ni
  ndani ya Bunge au mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge.
Na kwa
ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku
itawalazimu
wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo
hapa watakuwa
wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na
kufanya kazi
  ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.


Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio
watakaounda serikali na
Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama
wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu
hawatampenda
  au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu
wabunge hao wa
  CCM kwa wakati huo.

Chanzo Raia Mwema




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment