Saturday 16 July 2016

Re: [wanabidii] Ukistaajabu ya Profesa Lipumba utayaona ya Chadema

Muhingo hoja zingine unazoandika unakua kama umeleww bro, hv huamini kua uongoz wa ccm ni mbovu.....simple'logic kwann wanatumbuliwa majibu.......uwenge na uwezo wa kujenga hoja mzee acha kunywa maji ya bebdera ya ccm.....
Lipumba, arejee cuf kwann nyie ccm ndio mnapenda sana arudi,'kaz mliomtuma imeshindwa huyo ni kibaraka wa ccm....asiejua labda ni mtoto aliezaliwa mwaka huu.....kibaraka mtiifu wa ccm anakomaa na njaa zake arud cuf kuharibu kaz waliofanya majemedar kina lowasa,sumaye, mh seif,mbowe na team yoote ya ukawa, na ndio maana sasa CUF ina wabunge kibao na madiwani bara....enzi za kibaraka huyo unaemshbikia alikuwepo mbunge mmoja tu wa lindi tena alishinda kwa nguvu zake mwenyewe ...leo wabunge kibao thru ukawa anaeinga yeye,sasa hata ww na ulevi wako wa akili utamkaribishaje tena mtu kama huyo anaependa kula tu bali hapiki.....simple logic is there, ni sawa na kuyarudia matapish yake, msomi mzima antaka ale matapishi yake, ss as ukawa tunasema hata ale matapishi yake kiti kile atapewa hata mh mtatiro,'kinamtosha kuliko prof huyu aliejiaibisha.
Elisa, siasa zake si za kupenda nchi bali ni za kishabiki na lengo lako ni kuona demokrasi ikifa, huwezi zuia demokrasia hap mh,hata mfanyeje

'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>Hivi kipi kinashangaza CDM kumpokea Lowasa akitokea CCM ambayo ilifahamika kwao kuwa chama kibovu AU CUF kumrudisha Lipumba kwenye nafasi yake kwa sababu alichokikataa kimekataliwa na watanzania wote? CCM mbovu ni ipi: Bendela yake, majengo yake au VIONGOZI WAKE? Kama ni viongozi iweje CDM wampokee kiongozi mbovu kutoka CCM iwe sawa lakini CUF kumrudisha kiongozi wake aliyemkataa kiongozi mbovu atake kurudi wamshambulie. Nani hajaelewa kwa nini kuna msemo kuwa upinzani ni manyumbu? Ninadhani viongozi wetu wanahitaji kujiuliza mara kadhaa kabla ya kutamka chochote.
>--------------------------------------------
>On Sat, 7/16/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Ukistaajabu ya Profesa Lipumba utayaona ya Chadema
> To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Saturday, July 16, 2016, 4:28 PM
>
> HAPO
> zamani za kale, paliibuka msemo maarufu, usemao,
> "Ukiyastaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni".
>
>
>
> Kwa muktadha wa haya yaendeleayo hii leo katika siasa
> muflisi nchini
> mwetu, lau kama utaamua kuubadili msemo huo, kwa kuwa akina
> 'Mtume
> Mussa' walikwishamalizika duniani, basi pale kwenye jina
> la 'Mussa'
> upabadili kwa kuliweka jina la 'Lipumba'.
>
>
>
> Walakini kwakuwa Mafirauni yangali yanaishi hadi hii leo,
> hivyo hapo
> kwenye jina 'Firauni' unaweza kupaacha vivyo hivyo, ima
> ukamtafuta
> Firauni yeyote mashuhuri hapa Tanzania kisha ukambandikia
> lakabu hiyo.
>
>
>
> Kwa mara nyingine tena Chama cha Wananchi – CUF kinaingiwa
> na tajriba
> nyingine, baada ya mwanachama wao aliyebingwa wa uchumi
> duniani,
> mzalendo wa enzi za BBC (Born Before Computer), mtoto wa
> mkulima wa
> Ilolangulu, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, kumwandikia
> barua Katibu
> mkuu wa chama chake cha siasa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,
> akiianika
> dhamira yake ya kutaka kuurejea wadhifa wake wa Uenyekiti wa
> chama hicho
> taifa, alioachana nao baada ya kuamua kujiuzulu takribani
> mwaka mmoja
> sasa, na kubakia kuwa mwanachama wa kawaida tu katika chama
> hicho.
>
>
>
> Katika maelezo yake wakati alipokuwa akijiuzulu wadhifa
> wake, gwiji na
> galacha huyo wa uchumi alitanabahisha kwamba dhamira yake
> ilimsuta
> kuendelea kumuunga mkono Edward Lowassa aliyejiunga na vyama
> vinavyounda
> Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA ili kugombea urais wa
> nchi hii.
>
>
>
> Msimamo wa Profesa Lipumba wa kutokuwa na imani juu ya
> Lowassa,
> aliyetoka CCM na kujiunga na CHADEMA ili agombee urais,
> haukuchipua tu
> mithili ya uyoga, bali ulianza siku nyingi tangu kipindi
> Lowassa angali
> CCM. Hivyo kudhihirisha maoni yake ilikuwa ni haki yake ya
> msingi na ya
> kikatiba. Na kuyasimamia hayo bila ya kutetereka ilikuwa ni
> ithibati ya
> ujasiri na kutoyumba kwake. Nani asiyemtaka mwenyekiti kama
> huyo?
>
>
>
> Wanasiasa wengi, hasa wa upinzani, hivi sasa wanalalama kuwa
> demokrasia
> inaminywa hapa nchini kutokana na kuzuiliwa kwao kutoa maoni
> yao kupitia
> mikutano ya hadhara na makongamano juu ya vile
> wanavyoviamini na
> kuvisimamia.
>
>
>
> Wanasiasa haohao, ndiyo waliyemshambulia na wanaoendelea
> kumshambulia
> mpinzani mwenzao Profesa Lipumba, kwa 'kosa' la kutoa
> maoni na misimamo
> yake juu ya kile alichokiamini.
>
>
>
> Yaani walimtaka Profesa Lipumba aikalifishe nafsi yake kwa
> kutokuwa huru
> kutoa maoni, na misimamo yake ili tu wao wakidhi matlaba
> zao, halafu na
> wao wanaloloma kubinywa uhuru wao wa kutoa maoni yao
> mikutanoni. Ama
> kweli ukiyastaajabu ya Lipumba, utayaona ya Chadema.
>
>
>
> Sasa kwa kuwa uchaguzi ulikwishamalizika, na kwamba Lowassa
> si mgombea
> tena, hivyo Profesa Lipumba akaonelea kwamba ili kuendelea
> kukiimarisha
> chama chake, ni vyema arejee kwenye kiti chake ambacho kwa
> yakini kabisa
> bado kina vumbi tangu alipokiacha kwa kukosa wa
> kukikalia.
>
>
>
> Maajabu yakaanzia hapo; baadhi ya upinzani hasa wasiokuwa
> wanachama wa
> CUF, wakaibuka na kujifanya wasemaji wa CUF kwa kumshambulia
> tena
> Lipumba kuwa hafai kurejea kitini kwa hoja kwamba Lowassa
> angali
> Chadema.
>
>
>
> Yaani baadhi ya wafuasi, washabiki, wanachama, wakereketwa,
> wafurukutwa,
> na hasa wa Chadema, walioshindwa kumburuza na kumsujudisha
> kwao Profesa
> Lipumba ili aisaliti dhamira yake ya kutomkubali Lowassa,
> leo wanataka
> kuwaburuza na kuwasujudisha wana CUF wamkane.
>
>
>
> Tukumbushane kidogo, hii hofu huja inapoguswa Chadema tu?
> Aliyewahi kuwa
> mwanachama wa CUF na Mbunge wa Bukoba, Wilfred Lwakatare,
> alipokihama
> chama hicho, na baadaye kujiunga na Chadema, na kuteuliwa
> kugombea
> ubunge, mbona hakukuwa na chuki vichwani mwa CUF, na badala
> yake
> wakamuunga mkono bila hiyana hadi akaukwaa ubunge?
>
>
>
> Haya kama haitoshi, mbona Chadema waliwahi kumpokea
> mwanachama na
> kiongozi mwingine wa CUF, Profesa Abdallah Safari, na bado
> CUF
> waliidumisha staamala yao bila ya kuisambaratisha UKAWA?
> Iweje leo CUF
> ikimrejeshea uenyekiti wake, kiongozi wao aliyejiuzulu,
> ambaye hadi sasa
> angali mwanachama wao, iwe nongwa? Amaa kweli ukiyastaajabu
> ya Lipumba,
> utayaona ya Chadema.
>
>
>
> Akihojiwa na vyombo vya habari kufuatia ombi la Profesa
> Lipumba kurejea
> kitini, kiongozi wa Chadema, ambaye pia ni mwalimu wetu wa
> Kiswahili,
> Profesa Abdallah Safari, pamoja na majibu marefu, alisema
> kwamba; "hana
> imani na Lipumba,"
>
>
>
> Nikajiuliza hivi kwanini hii kasumba ya watu wa Chadema
> kuwasemea semea
> CUF inataka kushamiri kwa kasi namna hii? Sikupata majibu.
> Nikajisaili
> tena; hivi hii 'jeuri' ya kiongozi huyu wa Chadema,
> dhidi ya Profesa
> Lipumba, ilikuwa wapi kipindi kile wakati viongozi wenzie
> tena wa ndani
> ya chama chake waliopata kutuhubiria hapo awali kuwa Lowassa
> hafai? Amaa
> kweli ukiyastaajabu ya Lipumba, utayaona ya Chadema.
>
>
>
> Ni Muhali kuwasikia viongozi wa CUF wakiyaingilia na
> kuyasemea semea
> mazingaombwe yoyote yale kutoka katika chama chochote kile
> cha siasa,
> lakini wanakosa ujasiri wa kuwakemea wale wote wanaoingilia
> mambo yao ya
> ndani hasa wakiwa wanatokea upinzani. Sasa nasaha zangu kwa
> CUF, hebu
> mtuweke wazi jamani labda wenzetu kuna kifungu kinawabana
> mbavu kila
> mnapofikiria tu kujikukurua dhidi ya hulka hii chafu.
>
>
>
> Chanzo Rai
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment