Saturday 16 July 2016

Re: [wanabidii] Ukistaajabu ya Profesa Lipumba utayaona ya Chadema

Hivi kipi kinashangaza CDM kumpokea Lowasa akitokea CCM ambayo ilifahamika kwao kuwa chama kibovu AU CUF kumrudisha Lipumba kwenye nafasi yake kwa sababu alichokikataa kimekataliwa na watanzania wote? CCM mbovu ni ipi: Bendela yake, majengo yake au VIONGOZI WAKE? Kama ni viongozi iweje CDM wampokee kiongozi mbovu kutoka CCM iwe sawa lakini CUF kumrudisha kiongozi wake aliyemkataa kiongozi mbovu atake kurudi wamshambulie. Nani hajaelewa kwa nini kuna msemo kuwa upinzani ni manyumbu? Ninadhani viongozi wetu wanahitaji kujiuliza mara kadhaa kabla ya kutamka chochote.
--------------------------------------------
On Sat, 7/16/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Ukistaajabu ya Profesa Lipumba utayaona ya Chadema
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, July 16, 2016, 4:28 PM

HAPO
zamani za kale, paliibuka msemo maarufu, usemao,
"Ukiyastaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni".



Kwa muktadha wa haya yaendeleayo hii leo katika siasa
muflisi nchini
mwetu, lau kama utaamua kuubadili msemo huo, kwa kuwa akina
'Mtume
Mussa' walikwishamalizika duniani, basi pale kwenye jina
la 'Mussa'
upabadili kwa kuliweka jina la 'Lipumba'.



Walakini kwakuwa Mafirauni yangali yanaishi hadi hii leo,
hivyo hapo
kwenye jina 'Firauni' unaweza kupaacha vivyo hivyo, ima
ukamtafuta
Firauni yeyote mashuhuri hapa Tanzania kisha ukambandikia
lakabu hiyo.



Kwa mara nyingine tena Chama cha Wananchi – CUF kinaingiwa
na tajriba
nyingine, baada ya mwanachama wao aliyebingwa wa uchumi
duniani,
mzalendo wa enzi za BBC (Born Before Computer), mtoto wa
mkulima wa
Ilolangulu, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, kumwandikia
barua Katibu
mkuu wa chama chake cha siasa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,
akiianika
dhamira yake ya kutaka kuurejea wadhifa wake wa Uenyekiti wa
chama hicho
taifa, alioachana nao baada ya kuamua kujiuzulu takribani
mwaka mmoja
sasa, na kubakia kuwa mwanachama wa kawaida tu katika chama
hicho.



Katika maelezo yake wakati alipokuwa akijiuzulu wadhifa
wake, gwiji na
galacha huyo wa uchumi alitanabahisha kwamba dhamira yake
ilimsuta
kuendelea kumuunga mkono Edward Lowassa aliyejiunga na vyama
vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA ili kugombea urais wa
nchi hii.



Msimamo wa Profesa Lipumba wa kutokuwa na imani juu ya
Lowassa,
aliyetoka CCM na kujiunga na CHADEMA ili agombee urais,
haukuchipua tu
mithili ya uyoga, bali ulianza siku nyingi tangu kipindi
Lowassa angali
CCM. Hivyo kudhihirisha maoni yake ilikuwa ni haki yake ya
msingi na ya
kikatiba. Na kuyasimamia hayo bila ya kutetereka ilikuwa ni
ithibati ya
ujasiri na kutoyumba kwake. Nani asiyemtaka mwenyekiti kama
huyo?



Wanasiasa wengi, hasa wa upinzani, hivi sasa wanalalama kuwa
demokrasia
inaminywa hapa nchini kutokana na kuzuiliwa kwao kutoa maoni
yao kupitia
mikutano ya hadhara na makongamano juu ya vile
wanavyoviamini na
kuvisimamia.



Wanasiasa haohao, ndiyo waliyemshambulia na wanaoendelea
kumshambulia
mpinzani mwenzao Profesa Lipumba, kwa 'kosa' la kutoa
maoni na misimamo
yake juu ya kile alichokiamini.



Yaani walimtaka Profesa Lipumba aikalifishe nafsi yake kwa
kutokuwa huru
kutoa maoni, na misimamo yake ili tu wao wakidhi matlaba
zao, halafu na
wao wanaloloma kubinywa uhuru wao wa kutoa maoni yao
mikutanoni. Ama
kweli ukiyastaajabu ya Lipumba, utayaona ya Chadema.



Sasa kwa kuwa uchaguzi ulikwishamalizika, na kwamba Lowassa
si mgombea
tena, hivyo Profesa Lipumba akaonelea kwamba ili kuendelea
kukiimarisha
chama chake, ni vyema arejee kwenye kiti chake ambacho kwa
yakini kabisa
bado kina vumbi tangu alipokiacha kwa kukosa wa
kukikalia.



Maajabu yakaanzia hapo; baadhi ya upinzani hasa wasiokuwa
wanachama wa
CUF, wakaibuka na kujifanya wasemaji wa CUF kwa kumshambulia
tena
Lipumba kuwa hafai kurejea kitini kwa hoja kwamba Lowassa
angali
Chadema.



Yaani baadhi ya wafuasi, washabiki, wanachama, wakereketwa,
wafurukutwa,
na hasa wa Chadema, walioshindwa kumburuza na kumsujudisha
kwao Profesa
Lipumba ili aisaliti dhamira yake ya kutomkubali Lowassa,
leo wanataka
kuwaburuza na kuwasujudisha wana CUF wamkane.



Tukumbushane kidogo, hii hofu huja inapoguswa Chadema tu?
Aliyewahi kuwa
mwanachama wa CUF na Mbunge wa Bukoba, Wilfred Lwakatare,
alipokihama
chama hicho, na baadaye kujiunga na Chadema, na kuteuliwa
kugombea
ubunge, mbona hakukuwa na chuki vichwani mwa CUF, na badala
yake
wakamuunga mkono bila hiyana hadi akaukwaa ubunge?



Haya kama haitoshi, mbona Chadema waliwahi kumpokea
mwanachama na
kiongozi mwingine wa CUF, Profesa Abdallah Safari, na bado
CUF
waliidumisha staamala yao bila ya kuisambaratisha UKAWA?
Iweje leo CUF
ikimrejeshea uenyekiti wake, kiongozi wao aliyejiuzulu,
ambaye hadi sasa
angali mwanachama wao, iwe nongwa? Amaa kweli ukiyastaajabu
ya Lipumba,
utayaona ya Chadema.



Akihojiwa na vyombo vya habari kufuatia ombi la Profesa
Lipumba kurejea
kitini, kiongozi wa Chadema, ambaye pia ni mwalimu wetu wa
Kiswahili,
Profesa Abdallah Safari, pamoja na majibu marefu, alisema
kwamba; "hana
imani na Lipumba,"



Nikajiuliza hivi kwanini hii kasumba ya watu wa Chadema
kuwasemea semea
CUF inataka kushamiri kwa kasi namna hii? Sikupata majibu.
Nikajisaili
tena; hivi hii 'jeuri' ya kiongozi huyu wa Chadema,
dhidi ya Profesa
Lipumba, ilikuwa wapi kipindi kile wakati viongozi wenzie
tena wa ndani
ya chama chake waliopata kutuhubiria hapo awali kuwa Lowassa
hafai? Amaa
kweli ukiyastaajabu ya Lipumba, utayaona ya Chadema.



Ni Muhali kuwasikia viongozi wa CUF wakiyaingilia na
kuyasemea semea
mazingaombwe yoyote yale kutoka katika chama chochote kile
cha siasa,
lakini wanakosa ujasiri wa kuwakemea wale wote wanaoingilia
mambo yao ya
ndani hasa wakiwa wanatokea upinzani. Sasa nasaha zangu kwa
CUF, hebu
mtuweke wazi jamani labda wenzetu kuna kifungu kinawabana
mbavu kila
mnapofikiria tu kujikukurua dhidi ya hulka hii chafu.



Chanzo Rai



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment