Makala hii ni danganya toto. Hakuna ugonvi kati ya Kikwete na Lowassa. Huko ni kumpaka Kikwete kuwa ana chuki na LOwassa kama mlivyompaka Lowassa kwamba ni fisadi wa Richmond. Ni siasa nyepesi za maji taka, ambazo hazina nafasi Tanzania.
Kinachopiganiwa ni kitu kizito. Ni CCM iliyochafuka kwa ufisadi mfano EPA, Richmond na Tegeta Escrow ibaki madarakani ili kikundi cha watawala wachache kiendelee kujitajirisha kifisadi kwa fedha na mali za nchi huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanachama wa kawaida wanaCCM wakibaki katika mafuriko ya umaskini. Mwenye kuandika makala hii atambua kuwa fumbo mfumbie mjinga mwerevu analing'amua.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Thu, 10/1/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "Mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 1, 2015, 1:11 PM
NIANZE makala haya kwa kusahihisha eneo moja dogo
katika makala
yangu ya wiki iliyopita iliyokuwa imebeba kichwa cha habari
kisemacho;
Hapa Kazi Tu, tutarajie nini? kwa lengo la kuweka kumbukumbu
sawa.
Katika makala hayo, kuna eneo niliandika: "Mwalimu
aling'atuka na
kukabidhi nchi hii kwa Mzee Mwinyi mwaka 1985, akiiacha
thamani ya
Shilingi ya Tanzania ikiwa juu, huku noti kubwa ya fedha za
Tanzania
ikiwa ni noti ya Sh 2,000 tu, sarafu ya senti tano (5) ikiwa
na thamani
ya kununua kitu dukani, noti ya Sh 100, maarufu mijini kwa
jina la Masai
kama inavyoitwa leo Msimbazi noti ya Sh 10,000 ikiwa na
thamani ya hali
ya juu pia.
"Ndani ya miaka mitano ya kwanza tu ya Mzee Mwinyi,
Tanzania
ikashuhudia anguko kubwa la viwanda, mashirika na kampuni za
umma.
Mfumuko wa bei ukapanda kwa kasi, Tanzania ikashahudia
serikali
ikiingiza noti ya Sh 5,000 kama moja ya mkakati wa kudhibiti
mfumuko huo
wa bei, kabla ya kuingizwa kwa noti ya Sh 10,000 katika
awamu ya pili
na ya mwisho ya miaka yake mingine mitano."
Usahihi ni kwamba Mzee Mwinyi alikabidhiwa nchi hii mwaka
1985, noti
kubwa ya fedha za Tanzania ikiwa ni noti ya Sh 100 na si Sh
2,000 kama
nilivyoeleza katika makala ile ya wiki iliyopita.
Baadhi ya wasomaji wangu wenye kumbukumbu nzuri
wamenikumbusha kwamba
wakati Baba wa Taifa anang'atuka uongozi wa taifa hili na
kumkabidhi
Mzee Mwinyi mwaka 1985, taifa lilikuwa na noti nne tu za Sh
5.00, Sh
10.00, Sh 20.00 na Sh 100, ambapo katika mwaka wake wa
mwisho huo wa
1985, noti ya Sh 5.00 iliondolewa na badala yake ikaletwa
sarafu ya Sh
5.00, maarufu wakati ule kwa jina la Gwala au Dala (dola),
ikiwa na
alama ya trekta, ishara ya nchi inayotegemea uchumi wa
kilimo cha
kisasa.
Sarafu hiyo ya Sh 5.00 au Gwala au Dala, ilikuwa sawa na
dola moja ya
Kimarekani, ndiyo maana vijana wa mijini wakaiita Dala,
wakiwa na maana
ya dola, lakini pia Sh 5.00 hiyo ndiyo iliyokuwa bei ya
nauli kwa mtu
mmoja kwenye mabasi ya mijini, na ndicho kisa cha mabasi
hayo ya mijini
kuitwa daladala kwa sababu ya nauli yake hiyo ya wakati
ule.
Kwa upande wa sarafu, wenye kumbukumbu sahihi
wamenikumbusha kwamba
Mwalimu aliacha sarafu tano tu, kwa maana ya sarafu ya senti
5.00
iliyokuwa na alama ya samaki, sarafu za senti 10 iliyokuwa
na alama ya
pundamilia, sarafu ya senti 20 iliyokuwa na alama ya ndege
aina ya
mbuni, sarafu ya senti 50 au thumani, iliyokuwa na alama ya
sungura na
Shilingi moja iliyokuwa na alama ya Mwenge.
Kwa mujibu wa wasomaji wangu hao wenye kumbukumbu bado za
tangu wakati
ule, takriban miaka 30 iliyopita, bei ya kinywaji baridi
aina ya soda,
ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi moja na thumuni (Sh 1.50)
katika karibu
maduka yote nchi nzima.
Nimekumbushwa pia na wasomaji wangu hao kwamba noti za
200, Sh 500,
1,000, 2,000 na 5,000 ziliingizwa na Serikali ya Mzee Mwinyi
katika
kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano tu, kati ya mwaka
1985 na
1990, wakati noti ya Sh 10,000 iliingia katika kipindi chake
cha pili
cha kati ya mwaka 1990 hadi 1995!
Sababu za kuongeza noti zenye thamani kubwa tano hizo
ndani ya miaka
yake hiyo mitano ya kwanza, zimetajwa kwamba ni kutokana na
hatua ya
serikali hiyo ya Mzee Mwinyi kukubali kutii na kutekeleza
masharti ya
Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa
Duniani (IMF),
yaliyotaka, pamoja na mambo mengine, kushushwa kwa thamani
ya Shilingi
ya Tanzania, jambo ambalo Baba wa Taifa alilipinga kwa nguvu
zake zote.
Nichukue fursa hii kuwaomba radhi wasomaji wangu wote kwa
upungufu huo
wa kumbukumbu za kitakwimu kuhusiana na sarafu na noti
katika kipindi
kile cha taifa hili kutoka mikononi mwa Mwalimu kwenda
mikononi mwa Mzee
Mwinyi.
Mada ya leo imebebwa na maneno; ugomvi wa Lowassa na Kikwete
wawapumbaza Watanzania.
Hili nimelipata sehemu fulani kwenye kijiwe cha mijadala ya
kisiasa,
inayojadili hali ya kisiasa ndani ya nchi hii, hasa katika
kipindi hiki
cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Kijiwe hicho ni maarufu kwa kahawa na michezo ya bao na
karata.
Kinapatikana wilayani Kinondoni, katika Jimbo la Kawe. Mzee
mmoja wa
makamo, baada ya kusikiliza ubishi wa kisiasa juu ya nani
zaidi kati ya
mgombea wa CCM, Dk John Pombe Magufuli na mgombea wa
Chadema, Edward
Lowassa, aliinuka kutoka kwenye benchi alilokuwa amekalia na
kutamka:
"Ninyi wote hapo ni wajinga tu. Mngekuwa mnafahamu kuwa
mnachokishabikia kwa sasa ni ugomvi binafsi wa madaraka kati
ya Mkwere
na Mmasai, msingepoteza muda wenu kumjadili Lowassa."
Katika kutoa ufafanuzi wake juu ya kauli yake hiyo, Mzee
huyo anasema
Lowassa ana hasira sana na Kikwete, hasa baada ya Mwenyekiti
huyo wa CCM
kuzuia jina lake lisifikishwe hata ndani ya kikao cha
Kamati Kuu mjini
Dodoma ili lijadiliwe na wajumbe wa kikao hicho na hatimaye
wajumbe
wenyewe waamue hatima yake.
Anasema hasira hizo zinazotokana na kitendo hicho cha Rais
Kikwete,
cha kutumia nguvu nyingi kuzuia jina la Lowassa kufikishwa
katika vikao
vya uamuzi vya chama chake, ndizo zilizomwongezea ghadhabu
na chuki
zaidi Lowassa, hivyo kuachana na CCM na kuhamia Chadema ili
tu
kumuonyesha Rais na
Mwenyekiti Kikwete, ni nani zaidi katika siasa za nchi hii
kati yao hao wawili.
Kwa mujibu wa Mzee huyo, tukio lile la Dodoma la jina la
Lowassa
kushindwa kufikishwa ndani ya vikao vikuu vya uamuzi vya
Chama, lilikuwa
ni tukio la tatu kwa mwanasiasa huyo kutoshwa na swahiba
wake mkuu
huyo, Rais Kikwete, jambo lililompandisha hasira Lowassa,
hivyo kuamua
potelea mbali, liwalo na liwe!
Binafsi, nakubaliana na hoja hizo za Mzee huyo. Watanzania
tumejikuta
hapa tulipo sasa, kutokana na kukumbwa na upepo wa ugomvi wa
madaraka wa
watu hawa wawili; Rais Kikwete na Lowassa, si kitu
kingine!
Kwa haiba na heshima aliyokuwa nayo Lowassa ndani ya CCM,
chama
kilichomlea na kumjenga kisiasa hadi kumfikisha hapo alipo,
isingekuwa
kazi rahisi kwa mbunge huyu wa Monduli kuchukua uamuzi mgumu
huo
alioufanya wa kuamua kuachana na chama chake hicho na
kujiunga na
Chadema, chama ambacho kwa karibu miongo miwili, viongozi
wake walikuwa
wakimchafua na kumdhalilisha mbele ya jamii ya
Watanzania.
Binafsi, naamini hata uamuzi wa Waziri Mkuu Mstaafu,
Frederick Sumaye,
wa kuamua kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na upinzani,
hautokani na
chuki na kukerwa na hatua ya chama hicho kukata jina lake
katika mbio
zake za urais mwaka huu mjini Dodoma, bali ni chuki na
hasira dhidi ya
Rais na Mwenyekiti Kikwete.
Nitaeleza. Imesemwa na bado inaendelea kusemwa kwamba
Lowassa na Rais
Kikwete ni marafiki wakubwa. Ni kutokana na urafiki huo,
uliowafanya
wawili hao, mwanzoni mwa miaka ya 2000 waingie katika
makubaliano ya
kirafiki ya kuachiana awamu za utawala wa nchi hii kwa
kuungana mkono na
kuunganisha nguvu zao za kisiasa.
Ni makubaliano hayo ya kirafiki kati ya wawili hao,
yalishuhudiwa bila
shaka na wapambe wao wa karibu, ndiyo yaliyomhakikishia na
kumwaminisha
Lowassa kwamba baada ya Rais Kikwete, yeye ndiye angekuwa
mrithi wake,
Rais wa Awamu ya Tano ya uongozi wa taifa hili.
Katikati kujiamini huko kwa Lowassa, kunakotokana na
makubaliano hayo
ya kirafiki, ya yeye kumwachia na kumuunga mkono rafiki yake
2005 ili
itakapofika mwaka 2015 achukue yeye nafasi kwa kuungwa mkono
pia na
rafiki yake huyo, ndiko kulikompa jeuri hadi kufikia
kukiambia chama
chake kwamba ndani yake hakuna yeyote mwenye uthubutu wowote
wa kukata
jina lake.
Lowassa hakutegemea kabisa kuona Rais na Mwenyekiti
Kikwete anayejua
makubaliano yao hayo, anaweza akamgeuka na kuwa upande wa
wanachama
wenzao kina Samuel Sitta, Bernard Membe na wangineo
waliokuwa hawataki
kabisa kusikia jina la Lowassa likiteuliwa na chama chao
kuwa mgombea
urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Hatua hiyo ya Rais na Mwenyekiti Kikwete, kuongoza na
kusimamia
mikakati ya kuhakikisha jina la Lowassa halipitishwi na
chama chake kuwa
mgombea mteule wa urais, lilikuwa ni pigo la tatu na mwisho
kwa
mwanasiasa huyo lililotonesha madonda ya mapigo mengine
mawili ya huko
nyuma, ambayo nayo yalisimamiwa na rafiki yake huyo.
La kwanza lilikuwa ni lile la mwaka 2008, pale Lowassa
akiwa Waziri
Mkuu, alipojikuta akijiuzulu wadhifa wake huo katika
mazingira ya
fedheha, aibu na udhalili.
Naamini, kabla ya kupatwa na mkasa huo wa kujiuzulu,
Lowassa hakuwa
amewahi kukaa chini na kufikiria dhamana ya nafasi hiyo
aliyokuwa
amepewa ya kuwa waziri mkuu, wala hakuwahi kufikiria kuwa
ingeweza
kutokea akakwamia njiani kabla ya 2015 kwa sababu kuamini
katika dhana
ya 'ushakaji' na Rais Kikwete.
Lowassa alijiamini na kujawa na jeuri ya hali ya juu
katika utendaji
wake wa uwaziri mkuu, akijua kwamba hakuna yeyote, awe
mteuzi wake
mwenyewe Rais Kikwete au mwingine yeyote yule anayeweza
kumwondolea
uwaziri mkuu wake kwa sababu ya makubaliano yao ya kirafiki
ya wawili
hao.
Alijua, hata akifanya chochote kile kibaya kwa serikali
yao,
angefumbiwa macho tu na mamlaka yake ya uteuzi kutokana na
'ushikaji'
wao. Akasau kitu kimoja muhimu katika uongozi wa nchi.
Dhamana! Ni nani
kati ya Lowassa na Rais Kikwete mwenye dhamana na nchi hii
na mwenye
dhamana na serikali yao.
Lowassa akasahau kwamba mambo yakiharibika, atakayeulizwa
na kulaumiwa
na umma wa Watanzania ni mkuu wa nchi, si yeye. Imani yake
hiyo ya
'kiushikaji' ilimfikisha mahali akatenda kinyume hata
cha maelekezo ya
serikali kupitia vikao vya Baraza la Mawaziri, hasa
lilipokuja suala la
kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura kwa njia sahihi na
salama kwa
Serikali.
Lowassa akasimama kidete, kwa kutumia mamlaka yake ya
uwaziri mkuu,
huku akijua fika kuwa mamlaka ya juu yake ni ya
'kishikaji' akahakikisha
kwamba bila Richmond, bora nchi iingie gizani kwa kukosa
umeme!
Alikataa ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma
(PPRA),
akakataa ushauri wa Bodi ya Zabuni ya Tanesco, akasema hapa
ni Richmond
tu!
Kwa hiyo, hata baada ya kupatwa na mkasa huo wa Richmond
baada ya
Bunge, kupitia Kamati Teule ya Dk Harrison Mwakyembe,
kumkalia kooni na
kumtaka ajitathimini na kujipima kama anastahili kuendelea
na uwaziri
mkuu wake huo, kwa vyovyote vile, Lowassa alitegemea kuwa
atalindwa,
atapiganiwa na kukingiwa kifua na Rais Kikwete. Haikuwa
hivyo, Rais
Kikwete alimtosa likawa pigo kuu la kwanza kwa Lowassa!
Pigo la pili kwa Lowassa lilikuwa lile la uamuzi wa chama
chake,
ukiongozwa na Rais na Mwenyekiti Kikwete na mitume 12 wa
CCM, waliokuwa
wakimtaka Lowassa na washirika wake wajivue gamba kwa
kujiondoa wenyewe
kwa hiyari yao ndani ya chama hicho, kutokana na kuandamwa
na tuhuma za
ufisadi kila kona.
Lowassa akawekwa kati. Kule viongozi wa Chadema, huku
viongozi wa CCM,
wakiongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye. Lowassa
akala ganzi, akajikausha huku akijenga hoja za utetezi ndani
ya vikao
vikuu vya chama chake akitegemea kuungwa mkono kwa kupata
utetezi wa
Rais na Mwenyekiti Kikwete ndani ya vikao vyao hivyo, lakini
haikuwa
hivyo!
Ni baada ya pigo hili la tatu mjini Dodoma, la Lowassa
kukatwa jina
lake katika mazingira yenye utata, ndipo hapo amefunguka
akili na
kubaini kwamba kumbe rafiki yake huyo alikwishampuuza na
kuvunja urafiki
wao pamoja na makubaliano yao yote ya kupeana utawala wa
nchi hii kama
mali yao.
Lowassa, baada ya kufunguka akili na kubaini hali hiyo,
ameamua
kumtangazia vita ya kisiasa Kikwete. Kuhakikisha anatumia
rasilimali
zake zote, kuing'oa CCM madarakani ikiwa mikononi mwa
Kikwete bado!
Kama ilivyo kwa Sumaye, mgomvi wa Lowassa si CCM, bali ni
Kikwete.
Ugomvi wa Kikwete na Sumaye, ulianza mwaka 2005 wakati wa
mchakato wa
kusaka mgombea mteule wa urais ndani ya chama hicho.
Kwa wenye kumbukumbu Sumaye alifikia hatua ya kumwambia
Kikwete kwamba
mtu yeyote anayetafuta urais kwa kuwaua washindani wake kwa
kalamu
(magazeti), akipata urais ataua kwa risasi!
Chuki ile ya Sumaye ya mwaka 2005 dhidi ya Kikwete, bado
anayo hadi
leo baada ya jina lake kukatwa mjini Dodoma chini ya
usimamizi wa Rais
na Mwenyekiti Kikwete, ndiyo maana waziri mkuu huyo mstaafu
ameamua,
katika hilo la 'kumshughulikia' Kikwete, azike tofauti
zake na misimamo
yake dhidi ya Lowassa na kuungana na Lowassa.
Hapo ndipo Tanzania imefikishwa, hapo ndipo CCM
imefikishwa, na zaidi,
hapo ndipo Watanzania walipofikishwa na wanasiasa hao
watatu. Hivi
ugomvi huo wa mafahari wawili hawa, Lowassa na Kikwete una
tija gani
yoyote kwa taifa hili, kiasi cha kuwavuta baadhi ya
Watanzania wenzetu
kujitoa akili na kumshabikia mtu mwenye hasira na chuki zake
aliyedhamiria kununua urais kwa gharama yoyote ili kuwakomoa
na kulipa
visasi kwa wagomvi wake?
Nihitimishe makala haya kwa kusema kwamba wote
wanaomshabikia Lowassa,
kama anavyoonya mzee yule wa kwenye kijiwe cha kahawa,
wameamua kununua
ugomvi usiokuwa wa kwao. Ni vema wakakumbuka kuwa siku zote
mwenye kisu
kikali, ndiye mwenye kula nyama. Katika ugomvi huu, Lowassa
ameshika
makali, yatamkata tu!
Chanzo Raia
Mwema
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment