Kasema alimselema-Halija!! Wimbo wa Mangufuli! Baadae ndio kasema-People's........ Tuchague mwenye kumbukumbu na uwezo!! Hapa kazi tu.
--------------------------------------------
On Thu, 1/10/15, mary ndaro <mary.ndaro2@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Tuseme ukweli na tusiwapotoshe wananchi
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 1 October, 2015, 17:12
Bam
On 1 Oct 2015 13:44,
"'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Privatus Karugendo
TUNAPOELEKEA Uchaguzi Mkuu wa 2015, tutayasikia mengi. Na
tumeanza
kuyasikia na tutaendelea kuyasikia kufikia tarehe yenyewe ya
uchaguzi,
Oktoba 25, 2015. Mengine ya ukweli na mengine ya uongo. Watu
wataanza
kupakana matope na kuharibiana majina. Kutakuwa na mapambano
makali kati
ya chama na chama. Vyama vikubwa vinakabana .
Kila mtu anataka ashinde na kila chama kinataka kishinde.
Hiyo ndiyo
siasa na huo ndiyo ubinadamu. La msingi ni kusema
ukweli.Tusipindishe
mambo. Wezi wa nchi hii wanafahamika, mafisadi wa nchi hii
wanafahamika,
wazalendo na watu safi wasiohongeka wanafahamika na ni
wengi. La msingi
ni kuacha siasa za chuki na kumshambulia mtu binafsi. Vile
vile ni
vyama kutangaza sera na kuyaeleza yale watakayoyafanya
wakiingia
madarakani.
Maisha ya mtu binafsi, maisha ya familia yake, maisha ya
afya yake si
suala la kisiasa. Pamoja na uangalifu wa kuzuia kurudia
uchaguzi kwa
kipindi kifupi, mengine tumwachie Mwenyezi Mungu, yeye
akitaka, tunaweza
kuurudia uchaguzi hata mara tatu kwa mwaka. Tuache siasa za
uongo na
chuki. Siasa hizi za uongo, chuki, umbea na uhasama,
zimeanza kujitokeza
kwa nguvu.
Tumeweka mambo ya msingi pembeni na kuanza kushughulikia
umbea na
uhasama. Baadhi ya vyombo vya habari vinavyoaminika vimeanza
kupotea
njia. Magazeti yanaandika uongo na kueneza chuki. Watu
tulioambiwa ni
magamba, wakatangazwa na vyombo vya habari kwamba ni
mafisadi, leo hii
wamesafishwa na watu wale wale walio watangaza. Tunaambiwa
wametubu na
kusamehewa.
Wametubu wapi? Fedha za Richmond zimerudi? Aliyepitisha
mkataba huo
mbovu amekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria? Sifa za
Edward Lowassa,
tunazifahamu.
Hata ukirudi nyuma kwenye vyombo vya habari utauona ukweli
huo. Leo
hii ndiye anapamba magazeti yote. Leo hii ndiye baadhi ya
watu wanamtaka
awe Rais wa Tanzania. Huku ni kuupotosha ukweli na
kuwapotosha
wananchi. Hizi ndizo tunaita siasa za uongo na siasa za
hatari.
Tumekuwa tukisikia sifa za Dk. John Magufuli. Hata ukirudi
nyuma na
kupekuwa magazeti yote, utakuta Magufuli, mchapakazi.
Magufuli,
anayejenga barabara na kupambana dhidi ya wezi kama
alivyoshika meli
iliyokuwa ikivua samaki kwenye Bahari ya Hindi. Leo hii
tunaanza kusikia
uongo juu yake kwa vile anapambana na mtu mwenye nguvu za
kifedha.
Tuseme ukweli na kuacha uongo. Lowassa na Magufuli,
wamekuwa ndani ya
serikali. Ni wazi kwa wagombea urais waliojitokeza, hawa
wawili wana
nafasi kubwa mmoja wao kutokea mshindi. Sote tunajua
utendaji kazi wao.
Tukiacha ushabiki wa vyama vyao vya siasa na kulitanguliza
taifa letu.
Tutakubaliana kwamba sifa za Magufuli ziko juu zaidi. Na
kama kweli
tunayataka mabadiliko, tunayoyalilia, tunalazimika kumchagua
Magufuli.
Jambo la msingi ambalo tunapaswa kuliangalia kwa makini
ili tuhesabike
kati ya jamii iliyostaarabika na inayoheshimika duniani ni
lazima
tufanye siasa zinazozingatia ukweli. Ni jambo la kawaida
katika
ushindani wa kisiasa watu kutafuta kuangushana, na kila
mmoja anataka
kushinda, ili ushindi uwe wa amani, ni lazima washindani
kueleza ukweli
dhidi ya wapinzani wao. Maana kama lengo ni kuijenga
Tanzania bora,
yenye amani na utulivu, hakuna haja ya kuupindisha ukweli.
Gharama ya
kupindisha ukweli ni kubwa na yenye hasara kuliko faida.
Ni ukweli kwamba Lowassa, aliachia ngazi ya Uwaziri Mkuu,
kwa kashifa
ya Richmond. Hadi ninapoandika makala hii, hatujamsikia
akifafanua juu
ya suala hili.
Nani alihusika na Richmond? Ni ukweli kwamba Lowassa, ndiye
baba wa
mtandao. Mashabiki wake wanatamba kwa hili hadi kusema
kwamba mtandao
huo, aliouanzisha Lowassa na kuendelea kuuratibu ndio
ulimwingiza
madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Mtandao umekivuruga Chama Cha Mapinduzi, mtandao umelivuruga
taifa letu.
Kama una kitu cha kujutia ni mtandao. Mfumo huu ndio
uliozaa "kichaa"
cha kila mtu kufikiri anaweza kuwa rais wa nchi, kila mtu
anaweza kuwa
mbunge. Mtandao umezaa utamaduni mpya wa kutumia fedha
kwenye uchaguzi,
utamaduni wa kununua kura na kununua shahada za uchaguzi.
Huu ni mfumo mchafu ambao hauwezi kuanzishwa na mtu msafi,
mtu wa kuwa
na sifa za kuliongoza taifa letu.Uchunguzi wa kina
unaonyesha Magufuli,
si sehemu ya mtandao huu, ndiyo maana maadui zake wanasema
hana mizizi
ngani ya CCM. Kuwa na mizizi ni kuwa kwenye mtandao, na kuwa
kwenye
makundi. Hivyo huyu ana nafasi ya pekee ya kukiunganisha
chama chake na
kuliunganisha taifa zaidi ya baba wa mtandao. Huyu ndiye
anayefaa
kuliongoza taifa letu.
Haya tunayasema bila ushabiki wowote na bila lengo au nia ya
kuomba
fedha kutoka sehemu yoyote ile. Tunayesema bila kuangalia
vyama vya
siasa, nguvu na ushawishi wa vya hivi. Tunaangalia uhai wa
taifa letu.
Tunaiangalia Tanzania ya leo na kesho. Huu ni ukweli ambao
ni lazima
kuusema na ni ukweli utakaotuweka huru.
Hapa Tanzania, ukiachia mbali kiti cha rais, nafasi
nyingine
zinazokuwa na ushindani mkubwa ni ubunge na udiwani. Hizi
zote ni nafasi
za uwakilishi. Mbunge anawawakilisha watu wa jimbo lake
bungeni na
diwani anawawakilishia watu wa kata yake kati vikao vya
halmashauri ya
wilaya. Nafasi hizi zinakuwa na siasa za uongo, chuki, umbea
na uhasama.
Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya wale wanaochaguliwa kwenye
nafasi hizi
wanafikiria zaidi juu ya posho kuliko kuuzingatia na
kuutafakari wajibu
wao wa kuwawakilisha wananchi, wajibu wa kuelezea ukweli,
kulinda
ukweli na kuusimamia ukweli. Kazi hii ni ngumu kiasi kwamba
kama watu
wangeifahamu vizuri, ni wachache wangeikimbilia!
Ni bora wananchi wakatambua hili kwamba wanapomtafuta
mbunge wa
kuwakilisha jimbo lao ni lazima wamtafute mtu mwenye uwezo
na karama ya
kutetea ukweli na kuusimamia bila kuyumbishwa na vitisho,
rushwa,
upendeleo au ubinafsi. Bunge ni chombo muhimu katika taifa
letu. Katiba
inasema:
"Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya
Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya
wananchi, kuisimamia
na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
vyake vyote
katitika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba
hii" (Ibara
63(2)).
Tumekuwa na utamaduni wa mafiga matatu. Kila chama cha
siasa kina
kauli mbiu ya mafiga matatu. Utatu mtakatifu wa kura ya
rais, mbunge na
diwani. Yawezekana ni utamaduni mbaya au mzuri, la msingi ni
kuchagua
kwa kuzingatia vigezo. Tusichague kwa ushabiki wa vyama vya
siasa.
Tuchague kwa kulitanguliza taifa letu la Tanzania.
Tumchague rais wa
kuliongoza taifa letu, rais wa vyama vyote vya siasa, rais
wa makabila
yote, rais wa waumini wote. Hii ndiyo kazi kubwa iliyo mbele
yetu. Ni
kazi inayohitaji ukweli zaidi ya upotoshaji
Raia Mwema
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment