Thursday, 1 October 2015

Re: [wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki

Ninamheshimu na kuheshimu kazi za uandishi za Johnson Mbwambo. Lakini ninapingana na miwani yake ya uchambuzi ilichoona kuhusu jambo moja;chanzo cha ufisadi uliosababisha nchi yetu kuwa na mafuriko ya mamilioni ya wananchi masikini.

Kadhalika napingana na Mbwambo kwamba serikali ya Dr Magufuli (serikali ya CCM) ufisadi wake utakuwa ni poa (afadhali) kuliko ufisadi wa serikali Lowassa (serikali ya CHADEMA-UKAWA).

Kimsingi kwa vile wagombea Urais wote wawili Dr Magufuli na Lowassa wamelelewa katika chama fisadi, ni afadhali Lowassa aliyeondoka kwenye chama kinacholea na kunufaika na ufisadi --na sasa anaomba Urais kupitia chama ambacho hakijawahi kuunda serikali na serikali yake (mlizi) ikawa fisadi--mwizi (mfano wizi EPA,Richmond,Tegeta escrow).

Zaidi ni afadhali serikali ya Lowassa (serikali ya UKAWA) kwa sababu chama kilichomsimamisha kugombea Urais (chadema) ilani yake inasema wataweka misingi ya kuzuia serikali (mlizi) kuwa mwizi-- kwa kuandika Katiba Mpya inayotokana na mamoni ya Wananchi.

Chama anachogombea nacho Urais Dr Magufuli --CCM hata kama Magufuli angekuwa ni mtu msafi kama malaika na mwenye dhamira njema kabisa ya kukomesha ufisadi--hawezi kufurukuta--hawezi kuleta mabadiliko yoyote endelevu--sana sana ataishia kuumizwa na mfumo wa kifisadi wa chama chake.

Serikali yake ya CCM itaendelea kuwa mwizi kwa sababu chama chake CCM kinanufaika na ufisadi vinginevyo watueleze ni kwa nini hasa chama CCM ilikataa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo ingejenga misingi ya kuzuia serikali (mlinzi wa mali za nchi) iwe ni ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR -Mageuzi au chama chochote kile isiwe serikali fisadi?

Tukumbuke--tatizo lolote katika nchi-linaondolewa kwa kuweka misingi ya utatuzi wa tatizo. Watu wa kutekeleza misingi hiyo hupatikana kulingana na misingi iliyowekwa. Tanzania ya Dr Magufuli bila misingi ya kuleta mabadiliko ya kukomesha ufisadi--ni janga la taifa. Kama CCM ilivyo janga la taifa hivi sasa kwa kuzalisha mafuriko ya maskini tukubali tukatae--time will tell iwapo Dr Magufuli atachaguliwa--janga litakuwa mara dufu maana mfumo uliopo utahitaji serikali ya Dr Magufuli ifanye ufisadi mkubwa zaidi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

Kwa hiyo, ili kukomesha ufisadi nchini ni afadhali Watanzania wamchague Lowassa, vyama vilivyomsimamisha Urais viandike Katiba Mpya--kuweka misingi ya kukomesha serikali zijazo zisiwe fisadi--kuepusha nchi yetu kuendelea kuzalisha mafuriko ya wananchi masikini.


Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 10/1/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 1, 2015, 1:20 PM





NIANZE kwa
kuwaomba radhi wasomaji wangu kwamba sitaonekana tena katika
safu hii kuanzia
toleo lijalo hadi mwanzoni mwa Desemba mwaka
huu.


Sababu
yenyewe ni kwamba narejea kijijini kwangu wiki hii kwa ajili
ya shughuli zangu
za kilimo. Msimu wa kilimo utakapomalizika nitarejea tena
Dar kuendelea na
shughuli za uandishi wa habari.


Nimeona
niyaweke wazi hayo kwa sababu kutoweka kwangu ghafla kwenye
safu hii (bila
maelezo) kunaweza kutafsiriwa vibaya mitandaoni. Uongo
unaweza kutembezwa
mitandaoni kwamba nimehongwa fedha ili nisiendelee kuandika
kwenye safu hii
hadi uchaguzi mkuu umalizike.


Kwa wiki
kadhaa sasa nimekuwa nikiitumia safu hii kuweka msimamo
wangu bila kificho
kuhusu mgombea urais John Magufuli ambaye, kwa mtazamo
wangu, naamini ndiye
anayeweza kuaminika kukabidhiwa dhamana ya kuiendesha nchi
yetu kwa kipindi cha
miaka mitano ijayo.


Johnson Mwambo

Walio nje ya
taaluma hii ya uandishi wa habari pengine walishangaa kuona
mwandishi wa safu
(Mbwambo) anamuunga mkono moja kwa moja mgombea urais wa CCM
na kumkosoa wa
Chadema. Hiyo ilikuwa tu katika kutekeleza wajibu wangu –
yaani kuchangia
katika juhudi za kuepusha nchi yetu isitawaliwe na mtu
mwenye tuhuma za miaka
mingi za ufisadi.


Napenda
kuitumia fursa hii kuwafahamisha wasomaji wangu ya kwamba
mwandishi wa safu
kumuunga mkono mgombea fulani wa urais ni jambo la kawaida
kabisa duniani
katika taaluma hii. Wanafanya hivyo kule Uingereza,
wanafanya hivyo kule
Marekani, na hata hapa Afrika ni hivyo hivyo.


Gazeti au
mwanasafu wa gazeti anaruhusiwa kabisa kuunga mkono mgombea
fulani wa urais
(endorse a candidate) ili mradi tu afanye hivyo wazi bila
kificho, na wasomaji
waelewe msimamo wa huyo mwanasafu au hilo gazeti tangu
mwanzo kabisa.


Kwa mantiki
hiyo, napenda pia nifafanue kwamba bodi ya wahariri ya
gazeti la Raia Mwema
haikupewa maagizo yoyote na wamiliki wa gazeti hili ya
kumuunga mkono mgombea
yeyote wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Na badala
yake wahariri wetu
wamepewa maelekezo ya kuwatendea haki wagombea wote kwa
kuzingatia zile kanuni
kuu za habari zinazofuatwa kote duniani.


Kwa ufupi,
Raia Mwema halina rasmi mgombea urais wake – yaani
haliku-endorse yeyote - awe
Magufuli, Lowassa, Mama Anna Mghwira nk. Hata hivyo, kwa
wanasafu wanaoandika
maoni binafsi wa Raia Mwema, wao wana uhuru huo wa
ku-endorse mgombea urais
wanayemtaka. Na kama nilivyoeleza, hicho ni kitu cha kawaida
kabisa katika
tasnia yetu duniani.


Ni kwa
sababu hiyo nimekuwa nikiitumia safu yangu hii ya Tafakuri
Jadidi kuwaeleza
Watanzania maoni yangu binafsi kwamba Edward Lowassa hafai
kuwa rais wetu mpya
kwa sababu, licha ya kuandamwa na kashfa za ufisadi kwa
miaka 20, hana jipya
ambalo hakuweza kulitenda katika miaka yake zaidi ya 20 ya
uongozi serikalini.


Wakati huo
ndio msimamo wangu binafsi, wanasafu wenzangu wengine nao
wamekuwa wakitumia
safu zao kwenye gazeti hili hili kuwahamasisha Watanzania
wamkatae Magufuli na
CCM yake na wamchague Lowassa. Narudia tena; yote hayo ni
mambo ya kawaida
kabisa katika uendeshaji wa magazeti duniani.


Baada ya
ufafanuzi huo, niseme kwamba ninaondoka Dar es Salaam kurudi
kijijini nikiwa na
imani kuwa mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli
ataibuka mshindi katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Nisichokuwa na uhakika nacho ni
ushindi wake
utakuwa ni wa asilimia ngapi.


Matokeo ya
utafiti wa hivi karibuni wa asasi za TWAWEZA na IPSOS
(SYNOVATE) yanaweza
yasiwe na usahihi wa asilimia 100, lakini ukweli ni kwamba
yanaakisi ukweli wa
mambo ulivyo na utakavyokuwa Oktoba 25.


Sina lengo
la kurudia hoja nilizokuwa nikizitoa kwa zaidi ya mwezi
mmoja katika safu hii
zinazonifanya niamini kuwa Magufuli atambwaga Lowassa katika
Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25. Itakuwa ni kuwachosha tu bure kurudia hoja
hizo.


Hata hivyo,
jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba CCM kimejiandaa
mapema kwa uchaguzi huu
kuliko Chadema, na kinaendesha kampeni zake kisayansi;
ilhali Chadema ni
mbwembwe
na usanii
tu.


Hata uamuzi
wa Chadema wa hivi karibuni wa kuongeza angani idadi ya
helkopta za kampeni ni
sehemu tu ya hizo mbwembwe. Kuna wakati kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa
kiliwahi kutumia helkopta tatu lakini kikaambulia ushindi
kwenye kata tatu tu!


Vyovyote
vile, ubashiri wangu ni kwamba Magufuli atashinda. Ubashiri
wangu mwingine ni
kwamba kuhamia kwa Lowassa katika Chadema na kampeni ya
urais aliyoifanya
hakutaleta mabadiliko makubwa kwa chama hicho kwa maana ya
kuongeza viti vya
ubunge.


Kwa hiyo,
kwa upande wa Chadema, ujio wa Lowassa utakuwa
umekidhoofisha tu chama hicho
kiutendaji kiuliko kilivyokuwa huko nyuma. Baada ya Oktoba
25, hali ya Chadema
itakuwa mbaya, na kama nilivyopata kusema awali, sitashangaa
ACT Wazalendo
kikiziba baadaye pengo la Chadema kama chama kikuu cha
upinzani nchini. Ni
suala la muda tu hilo kutokea.


Na hili
linanikumbusha maneno ambayo (sina hakika na ukweli wake)
niliyoambiwa hivi
karibuni na swahiba mmoja wa karibu wa Lowassa kwamba
mheshimiwa huyo alipoamua
kujiunga na Chadema ili agombee urais alijua fika kwamba
hatashinda urais huo
kupitia chama hicho!

Kwa mujibu
wa maelezo yake aliyodai kaambiwa na Lowassa mwenyewe,
swahiba huyo anasema
Lowassa aliamua kugombea urais kupitia Chadema ili
'kukiadhibu' chama hicho kwa
kumchafua kwa zaidi ya miaka tisa kuwa ni fisadi
mkubwa.


Lakini pia
aliamua kugombea urais kupitia chama hicho ili kupata fursa
maridhawa ya
kulipiza kisasi kwa Rais Kikwete ambaye aliweka kando
uswahiba wao na kumtosa
wakati ule alipoandamwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond
kiasi cha kumlazimisha
kujiuzulu uwaziri mkuu.


Swahiba huyo
wa Lowassa aliniambia ya kwamba 'adhabu' ya kwanza kwa
Chadema ni huo
mparaganyo uliosababisha Katibu Mkuu wa chama hicho
aliyeshiriki sana
kukijenga, Dk. Slaa kujiuzulu nafasi yake. Si siri kwamba
mpaka sasa Chadema
kinapwaya kwa kumkosa mtu wa sampuli ya Dk. Slaa kukaimu
nafasi hiyo.


Adhabu ya
pili au tuseme pigo la pili la Lowassa kwa Chadema ni hilo
la 'kuwalazimisha'
kina Mbowe na Lissu ambao walikuwa vinara wa kumwita fisadi,
kuyameza matapishi
yao wenyewe kwa kumsafisha wakati wa kampeni za urais kuwa
si fisadi.


Kwa mujibu
wa swahiba huyo wa Lowassa, hakuna jambo linalomfurahisha
mgombea urais huyo wa
Chadema hivi sasa zaidi ya kuwaona Lissu na Mbowe wakihaha
jukwaani kujaribu
kuuaminisha umma kuwa walikosea kumwita Lowassa fisadi.
Yaani anafurahi kuwaona
wakimeza matapishi yao wenyewe!


Kwa mtazamo
wake, hiyo ni adhabu kubwa kwa kina Mbowe na Lissu kwa
sababu heshima yao,
weledi wao, uungwana wao, uadilifu wao na uaminifu wao kwa
wanachama wa Chadema
sasa uko shakani kwa sababu ya 'kumeza' matapishi yao
hayo.


Kwa maana
hiyo, Lowassa anajiona 'kalipiza kisasi' kwa vinara hao
wa Chadema waliomwita
fisadi, na kwa Chadema yenyewe ambayo anaamini
itasambaratika baada ya Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba 25!


Kuhusu
kulipiza kisasi kwa Kikwete, swahiba wake huyo alinieleza ya
kuwa kwa kugombea
urais kupitia Chadema, Lowassa amepata fursa maridhawa ya
kulipiza kisasi kwa
kumpaka matope Kikwete wakati wa kampeni kuwa utawala wake
wa miaka 10 ulikuwa
hovyo kabisa, na kwamba ndiye aliyemlazimisha kuutia saini
mkataba wa kifisadi
wa Richmond. Fursa hiyo
asingeipata kwa kiwango anachopata hivi sasa wakati wa
kampeni za urais.


Kama hayo
aliyonieleza swahiba huyo wa Lowassa ni ya kweli, basi
inamaanisha kuwa tangu
mwanzo Lowassa alijua ya kuwa hatashinda urais kupitia
Chadema, na alichokifanya,
hivyo basi, ni kutafuta tu fursa ya kulipiza visasi kwa
Chadema na Kikwete.


Bila shaka
anafanya hivyo kwa sababu hana cha kupoteza. Sitashangaa
baada ya Oktoba 25
akajirudia Monduli kustaafu kabisa mambo ya siasa; maana
atakuwa amemaliza
'kuwashughulikia' waliomwita fisadi kwa miaka
tisa.


Kwa hiyo,
imani yangu ya tangu mwanzo kabisa kwamba Lowassa hana na
hatakuwa na faida
yoyote kubwa kwa Chadema baada ya Oktoba 25 imeimarishwa na
kauli hiyo ya
swahiba wake huyo.


Tukirejea
kwa CCM, ni kweli kuwa Magufuli atashinda lakini mambo
hayawezi kubakia
vilevile katika chama hicho na katika uendeshaji wa serikali
yake. Kwa maneno
mengine, mageuzi hayataepukika baada ya Oktoba 25 labda kama
CCM kinataka
kuishia vilikoishia KANU cha Kenya na ZANU cha
Zambia.


Kwa maneno
mengine, kampeni zilizoendeshwa na zinazoendeshwa na Lowassa
na Chadema yake,
ni maandiko mengine ukutani ambayo CCM lazima itakuwa
imeyaona na kuyasoma
vyema kwa sababu ya ukubwa wa herufi zake! Itakuwa imeweza
kuyasoma hata kama
ina makengeza!

Na maandiko
hayo ukutani yanasomekaje? Yanasomeka hivi: "Ni wakati wa
mabadiliko.
Tumeichoka CCM kiasi kwamba hata shetani tuko tayari
kumpigia kura aingie
Ikulu".


Huo ni
ujumbe mzito na unaotisha, na ni chama-mfu tu cha kisiasa
ndicho kinachoweza
kuudharau ujumbe wa namna hiyo. Watu wakishafikia hatua ya
kukata tamaa
kimaisha kiasi cha kusema kwamba hata kama ni shetani wako
tayari kumwingiza
Ikulu, ni lazima CCM kijiulize; kulikoni?


Na ujumbe
huo si mtupu (hollow). Ni ujumbe unaoendana na hali ambayo
imekuwa ikionekana
katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa – yaani
maelfu ya vijana waliokata
tamaa ya maisha hufurika katika mikutano yake
kumsikiliza.


Hata hivyo,
kitakachoikoa CCM na kumfanya Magufuli ashinde urais Oktoba
25 ni kwamba,
tofauti na Chadema, chenyewe kina muundo na mtandao wa hadi
ngazi za vijiji na
kata uliokiwezesha kuhahakikisha kila mwanachama wake
amejiandikisha kupiga
kura na siku ya kupiga kura kuhakikisha anajitokeza kupiga
kura.

 

Chadema
hakina muundo huo, na pia hakina mtandao huo wa hadi ngazi
ya vijiji na kata.
Kwa hiyo, kinabakia tu na imani (potofu!) kuwa vijana wote
wanaofurika kwa
maelfu katika mikutano ya kampeni ya Lowassa wamejiandikisha
kupiga kura -
kumbe ukweli ni tofauti kabisa na huo. Kasoro hiyo ndio
iliyomwangusha Dk. Slaa
mwaka 2010, na ndio itamwangusha Lowassa Oktoba
25.


Lakini
Chadema na ACT Wazalendo nk haviwezi kukubali kubakia na
udhaifu huo huo kwenye
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020. Bila shaka navyo
vitajitahidi kuweka ofisi na
mitandao ya hadi ngazi za vijiji na kata, na hivyo uchaguzi
mkuu mwingine wa
mwaka 2020 unaweza kuleta matokeo tofauti kabisa na
tutakayoyapata Oktoba 25
mwaka huu.


Na ndiyo
maana nasema ya kwamba kama CCM kinataka bado kuendelea
kukamata dola, ni
lazima baada ya Oktoba 25 kifanye mageuzi makubwa
yatakayoipa serikali yake
mwelekeo mpya wa kutatua kero ambazo kwazo zilifanya vijana
wafurike katika
mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa wakiwa na mategemeo
kwamba ndiye
atakayetatua matatizo yao.


Yaani kama
kama tatizo ni ajira, basi serikali ijayo ya CCM ni lazima
ionekane kweli kweli
ikitatua tatizo hilo. Kama tatizo ni maji, basi lazima liwe
historia ifikapo
mwaka 2020. Au kama tatizo ni kilimo duni na ukosefu wa
masoko kwa wakulima,
serikali ijayo ya CCM lazima ilitatue hilo kabla ya mwaka
2020. Na kama tatizo
ni kutamalaki kwa ufisadi nchini, basi lazima janga hilo
liwe limemalizwa
ifikapo mwaka huo.


Vinginevyo,
CCM kitakwenda na maji ifikapo 2020! Safari hii kitashinda
uchaguzi kwa taabu,
lakini safari ijayo kisipojirekebisha kitashindwa kiurahisi.
Ndiyo maana
naamini ya kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Lowassa
ameisaidia/ataisaidia mno CCM kujiona kilivyo, na ndio
sababu naamini kwamba
baada ya Oktoba 25 'kitajivua gamba' lake la
zamani.


Vyovyote
vile, kwa kuwa hii ndiyo makala yangu ya mwisho kabla ya
Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25, napenda nirudie kile ambacho nilikisema huko
nyuma. Kitu hicho ni
kwamba wagombea wote wawili wa urais – Lowassa na Magufuli
wana mapungufu ya
wazi.


Niliandika
huko nyuma kwamba pamoja na wote kuwa na mapungufu makubwa
kuna mmoja ambaye ni
nafuu kidogo kuliko mwenzake (a lesser devil). Ombi langu ni
lile lile: Kwa
kuwa wote wana mapungufu makubwa tutajitakia balaa kama
tutampa lesser devil
wetu wingi wa wabunge wa chama chake bungeni. Yaani
akivurunda tutakuwa hatuna
njia ya kumdhibiti bungeni kwa sababu atakuwa na wingi wa
wabunge.


Kwa hiyo,
salama yetu ni kwamba yeyote tutakayempigia kura – awe
Lowassa au Magufuli,
tusimpigie kura mgombea ubunge wa chama chake. Kwa mfano,
kama kura ya urais
unampa Lowassa, basi kura ya ubunge mpe mgombea wa CCM au
ACT Wazalendo. Na
kama kura yako ya urais unampa Magufuli, basi kura ya ubunge
kipe Chadema au
ACT Wazalendo.


Kwa namna
hiyo, tutajipa matumaini (japo kidogo) kwamba yeyote
atakayeshinda urais kati
ya hao wawili, Bunge litaweza kumdhibiti kama ataongoza nchi
hovyo. Lakini kama
akiwa na wingi wa wabunge wa chama chake bungeni (kama
ilivyokuwa kwa CCM kwa
miaka mingi), hatutaweza kumfunga 'gavana' hata kidogo
kama akivurunda.


Na mwisho
kabisa nawatakia uchaguzi mwema na wa amani Oktoba 25.
Nikirejea Desemba
nitaendelea kuandika makala za kumkosoa (kwa hoja) mtawala
wetu mpya bila
kujali ni Magufuli au Lowassa; maana hiyo ndiyo kazi
niliyojitwisha katika fani
hii ya uandishi wa habari.


Sikuingia
katika fani hii ili kuwaremba na kuwasifu watawala wakiwa
madarakani.
Nitawasifuje watawala kama wanatekeleza kile ambacho
wananchi walikitarajia
wakati wanawapa kura zao?

Nimeingia
katika fani hii kuwakosoa watawala wanapovurunda ili
wasilale usingizi; ilhali
wananchi wanateseka. Kazi hiyo nitaendelea nayo bila kujali
rais mpya ni
Magufuli au Lowassa.


Vyovyote
vile, rais akichapa vyema kazi hakuna 'habari' hapo.
'Habari' ni pale rais
anapokuwa mvivu, mlevi, legelege, fisadi nk. Kwenye taaluma
yetu ya habari tuna
msemo maarufu; mbwa akimng'ata binadamu hakuna habari.
Habari ni binadamu
akimng'ata mbwa.


Kwa maana
hiyo, nitaendelea kuwakosoa watawala wetu, na sitajali ni
Magufuli niliyempigia
kura yangu au Lowassa. Nitamkosoa (kwa hoja) yeyote kati ya
hao wawili
atakayefanikiwa kuingia Ikulu Oktoba 25; maana hakuna
'habari' katika kumsifu.
Tafakari.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment