Natamani kungekuwa na mbadala kwenye haya mabadiliko...Mimi binafsi watu waliotumua mfumo mbovu kutufikisha hapa haijalishi wanaahamia wapi...hao sio jibu wala mabadiliko tunayoyataka. Nakubali wananchi wamechoka na mfumo mbovu Wa ccm lkn majibu sio cdm chini ya EL
On 10 Sep 2015 15:40, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
--
Ndugu Kim,
Neno mabadiliko katika muktadha wa uchaguzi Tanzania mwaka huu 2015 linatumika kumaanisha wananchi kuchagua serikali mpya tofauti na serikali ya CCM iliyoko madarakani ambayo ilikataa kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
Katiba Mpya itaweka misingi ya kuzuia serikali kuwa chanzo ufisadi wa fedha za umma, watawala kujitajirisha na kuwatajirisha wawekezaji kutoka nje kwa kutumia rasilimali za nchi yetu huku mamilioni ya wananchi wakibaki masikini wa kutupa.
Mfano ufisadi wa mwaka jana 2014 wa Tegeta escrow bilioni 306, ufisadi wa Richmond bilioni 172 mwaka 2008 na ufisadi wa EPA bilioni 133 mwaka 2005 na hakuna aliyefikishwa mahakamani.
Mabadiliko ya kupata serikali inayoongoza na vyama vingine tofauti na CCM ikiandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ---Katiba hiyo itaweka misingi ambayo pamoja na mambomengine madaraka ya Rais yatapunguzwa—kuzuia Rais kuwa Mungu mtu.
Kadhalika madadiliko yataweka mihimili isiyoingiliana ya utawala—serikali—bunge na mahakama HIvyo serikali ikifanya ufisadi kama ule wa Tegeta escrow na EPA watawala hawatakwepa mkono wa sheria kama walivyokwepa.
Kadhalika mabadiliko yatazuia watawala wachache wakijitajirisha kwa kutumia fedha za wananchi kujilipa mishahara mikubwa, mafao na marupurupu wakati watumishi wengine wa umma madaktari, wauguzi, walimu, polisi na wananchi wengi wakibaki maskikini.
Pia Katiba Mpya itaweka misingi mizuri ya kuwepo usawa wa kijinsia katika uongozi hasa 50 kwa 50 wabunge wanawake na wanaume majimboni badala ya hili changa la macho ambalo baadhi ya vyama vinajidai eti kwa kuweka wagombea wanawake ni usawa wa jinsia.
Je inawezekana kuwa na usawa wa jinsia endelevu kama haijaandikwa kwenye Katiba ya nchi? Kama kweli serikali CCM walikuwa wanataka nchi iwe na usawa wa jinsia katika uongozi ni kwa nini waliikataa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo ilikuwa imependekeza utaratibu mzuri kabisa wa kupata asilimia 50 kwa 50 ya wanawake na wanaume bungeni kutoka majimboni?
Hivyo mabadiliko wanayoyataka wananchi wanaosumbuliwa na umaskini hapa nchini wao wenyewe wananchi wamejipanga kuweka msingi wake hapo hapo tarehe 25 Oktoba 2015 kwa kuiondoa CCM madarakani na kuweka serikali ya vyama vinavyounda UKAWA (CUF, NCCR Mageuzi, CHADEMA na NLD) ambavyo vilipigania Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi na vimeahidi kwamba wakichaguliwa Katiba Mpya ya wananchi itaandikwa.
Hivyo yeyote anatumia neno mabadiliko kwenye kampeni zake ajuwe akichaguliwa atatimiza yaliyobebwa katika tafsiri hii. Kinyume chake hayo siyo mabadiliko wanayoyataka wananchi. Mungu ibariki Tanzania.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Thu, 9/10/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, September 10, 2015, 2:45 PM
Kwanza
MABADILIKO ni nini?
Tukisema TUNATAKA MABADILIKO, maana yake ni
nini? ya wapi? kwenye nini? yatamgusa nani? yatatuchukua
muda gani? yatatokea tokeaje?
Mabadiliko yaweza kuwa baya kwenda zuri au zuri
kwenda baya, dogo kuwa kubwa au kubwa kuwa dogo, nyembamba
kuwa pana au....
Its all about "different" "utofauti wa hiki
kilichopo". nikikosea nisahihishwe. mie sio mtaalam wa
lugha!!
Mnazi awaye yeyote iwe wa Chama au mtu, aandike
akituelezea vizuuri na kwa ufasaha jinsi watakavyoleta
MABADILIKO nchini. i mean ameshawishikaje kuwa mnazi wa
flani/chama flani kuamini watafanya MABADILIKO ndani ya kila
mmoja wetu ili tukuamini na kukufuata popote ulipo!! Wanazi
wote hapa mkae mkijua nyie ni mawakala wa HAO mnaowasemea!!
kwa sababu sie hatumjui yule/wale vizur zaidi yako, umeamua
kuwa agent wake/wao ina maana unayajua ya kwake/kwao! Latin
proverb "if you host a guest, host his dog"
Tukibaki kuainisha MAHITAJI YA NCHI na
MTU/CHAMA chenye SULUHU yake bila kuijadili, kuchambua na
kuitafakari SULUHU yenyewe kwa kina, hatuna tofauti na mtu
anaeajiri bila vyeti na interview. Akiulizwa kwa nini? ati
" ameahidi ataongezea kampuni faida ndani ya miaka
5" ****!!! Its the question of HOW not WHO!!! WHO will
come later to filter HOW!!
Watanzania tumelogewa wapi??? tunashindwa na
hesabu ndogo ambazo tunazifanya kwenye maisha ya kila
siku!!!!!????? Mpaka inakera.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment