Duh, safi sana. Nimependa namna ulivyowakilisha.
Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com
--------------------------------------------
On Tue, 8/4/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Lipumba, Mbatia na Mbowe mnanidai Mijeledi
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, August 4, 2015, 12:36 AM
Lipumba, Mbatia na Mbowe mnanidai Mijeledi
Luqman
Maloto
Juzi, nikiwa nimeketi sebuleni natazama taarifa ya
habari, upande
wa pili mtoto wangu Nyambo alikuwa anafanya 'homuweki'
yake. Kila mmoja
alikuwa 'bize' na majukumu yake ya kumalizia siku.
Ila yeye alikuwa ananisumbua, "baba hii ni nini?" Shule
afundishwe yeye,
majibu nitoe mimi. Nyambo anadhani baba yake ni
'jiniaz',
ananiporomoshea 'viingereza' vyake "what is this?"
Habari kwamba umande
ulinitesa nikatoka nduki hana!
Nilikuwa natazama Televisheni ya Al Jazeera idhaa ya
Kiingereza, labda
kwa kuona hivyo ndiyo akadhani 'kiinglishi' kinapanda.
Nikimwambia sijui
mtoto anakuwa mkali, "teacher said you should help me"
hapo ikabidi
niwe mkali nikamwambia "tusitukanane mtoto, ohoo!"
Nikabadilisha 'chaneli', nikarudi kikwetukwetu! Si ndiyo
nikakutana na
habari moto ya Ukawa kumsafisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu,
Edward Ngoyai
Lowassa! Mchana wake nilisikia minong'ono kuwa
ameshajiunga na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Hapo nikaamini safari
imekwiva!
Baba mtu nikaanza kupayuka: "Yeees CCM kwisha, 2015 CCM
out!" Mtoto
akanihoji: "Unashangilia Lowassa kwenda upinzani au Ukawa
kumsafisha
Lowassa?" Nikamjibu: "Hapa ngoma inogile mwanangu,
Matumaini ameondoka,
CCM vipandevipande, CCM siwapendi walimkata Matumaini."
"Bora wewe huipendi CCM, mimi nawachukia Ukawa ni waongo
sana," Nyambo
alisema kwa sauti yenye ghadhabu, ikabidi nimrudi: "Wewe
fanya homuweki
yako achana na haya mambo ya wakubwa, unapiga kura
wewe?"
"Mengine yatapita, hili halipiti baba, Ukawa waongo sana
na ukiendelea
kuwatetea, siku nikisema uongo nisikuone unanishikia fimbo,
patachimbika," alisema akiwa anawaka, akafunga daftari kwa
hasira na
kuondoka.
Nikaona dogo anataka kunipanda kichwani, nikamwita sauti ya
kwanza
kimya, ya pili hakujibu akawa anaenda tu, mara ya tatu
nikakaza sauti
kiume, akaitika, nikamwambia arudi haraka.
Akaja 'kinundanunda', nikamuuliza kinachomtatiza, maana
'testi' yote ya
Matumaini kutoka CCM ilikuwa imetoweka kwa ajili yake.
Akanijibu: "Wewe
kila siku nikikuongopea unanichapa halafu wengine wakisema
uongo
unawashangilia." Ile sauti ya Nyambo ilikaa kulialia na
macho yalilengwa
machozi, kama baba ninayempenda mtoto wangu, nilijisikia
vibaya,
ikabidi niwe mpole.
"Kwani hao Ukawa wamekudanganya nini mwanangu?" Swali
langu liliamsha
mizuka ya Nyambo, alikuwa mkali kama pilipili kichaa.
"Huyu Profesa
Ibrahim Lipumba wa Cuf si ni yeye aliyesema CCM imewakosea
Watanzania
kwa kumpa Lowassa fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea
Urais?
"Tena alisema mtu aliyepaswa kuwa jela kwa kosa la ufisadi
anajitokeza
kugombea Urais na anakwenda kuchukua fomu anapewa. Hawa
akina James
Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Dk. Emmanuel Makaidi, si walikuwa
wanatangaza
huku na huko Lowassa fisadi? Leo hii wanamsafisha bila
aibu!"
Nilikosa cha kuzungumza kwa muda nikawa namtazama Nyambo,
nikawaza sijui
katumwa kunishawishi nibaki CCM! Alipoona nimekaa kimya
akazidi
kumiminika: "Siku ile Juni 18, mwaka huu kwenye mdahalo wa
wakuu wa
vyama vya siasa, ulioandaliwa na Taasisi ya CEO Roundtable,
si ilikuwa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan?"
Nikapiga hesabu, nikamjibu ndiyo. Akasema: "Basi Lipumba
hakufunga siku
hiyo, maana nilimuona kwenye runinga akiwa amekaza misuli
akielezea
jinsi Lowassa anavyostahili kuwa jela, leo hapa anamsafisha,
anasema
kama ni mchafu mbona hajapelekwa mahakamani, huyu babu
vipi?"
"Homuweki yako umemaliza?" Nilimhoji ili asiendelee
kukoroma, mtoto
mdogo anakoroma mbele ya mkubwa, nilimuona ananikata
'stimu'. Jibu
nililokutana nalo lilinikata maini. Nyambo wa siku hiyo si
sawa na wa
siku zote: "Nitafanya homuweki ukiniahidi na hao Ukawa
utawachapa kwa
kusema uongo kama vile ambavyo huwa unanichapa
nikiongopa."
Nikamtolea macho, jamani mimi nina ubavu gani wa kuwacharaza
viboko
Ukawa! Tatizo la watoto wanadhani sisi wazazi wao tuna nguvu
za kupiga
dunia nzima. Alipoona nipo kimya akanisisitiza: "Tena yule
Mwenyekiti wa
Chadema Freeman Mbowe na katibu wake Dk. Willibroad Slaa
ndiyo uwachape
mijeledi mingi."
Aliposema hivyo alikimbilia chumbani kwangu, aliporejea
alikuwa
ameshikilia nakala tatu za gazeti linalomilikiwa na Mbowe.
"Baba unaona
jinsi hawa watu wasivyofaa kuaminika? Hapa Mbowe anasema
Lowassa dhaifu
hatakiwi Ukawa kwa sababu ni bubu. Hili lingine linasema
Lowassa
anakaribishwa Ukawa.
"Hili la tatu linasema Slaa amekataa watakaokatwa na CCM
kwa sababu ni
makapi, Ukawa hawatasimamisha mgombea aliyekatwa na CCM. Leo
naona
chereko za Ukawa kumpokea Lowassa na kumsafisha. Kuna uongo
mkubwa
kuliko huu? Kuudanganya umma wa Watanzania."
Nyambo ndiye alikuwa nyota wa mazungumzo yetu siku hiyo,
aliteleza kama
amekanyaga ganda la ndizi: "Septemba 15, 2007 nilikuwa
sijazaliwa ila
baada ya kuzaliwa na kukuta Dk. Slaa anaitwa shujaa,
niliamua 'kugugo'
niuone ushujaa wake ulianzia wapi.
"Nikakuta aling'ara kwa kuanika majina 11 ya watu
wanaofilisi nchi.
Orodha ya Mafisadi, List of Shame! Katika majina hayo
aliyoyataja,
Lowassa ni namba tisa na washirika wake Rostam Aziz na Adrew
Chenge pia
wamo!
"Katika Uchaguzi Mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki mwaka
2012, Slaa
alisisitiza Lowassa ni fisadi na ndiyo maana baada ya
kutajwa kwenye
orodha ya mafisadi mwaka 2007 hakwenda mahakamani. Akasema
Lowassa
amejijengea ofisi binafsi ya mbunge yenye thamani ya
shilingi milioni
800 wakati wanafunzi wa Monduli wanakaa chini, vilevile
alipora mradi wa
maji Arumeru na kuupeleka Monduli.
"Sasa baba huyu aliyetupiwa kashfa zote hizo anasafishwaje
leo na watu
haohao? Fisadi papa wa jana, leo amekuwa kamanda, kivipi?
Juni mwaka
huu, Slaa aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter jinsi
ambavyo Lowassa
hafai kwa sababu ana madoa ya uadilifu."
Mtoto akachukua kompyuta mpakato, akatafuta vya kutafuta
kisha
akanionesha 'twiti' za Slaa, zilisomeka: "Lowassa
tumemtaja katika
Orodha ya Mafisadi walioifikisha nchi hii katika hali mbaya
kabisa.
Kilele kikiwa sakata la Richmond."
Nyingine ikasomeka: "Suala kwamba watu wenye madoa ya
uadilifu wanaota
Urais wa nchi ni wazi kwamba kupita katika chama chao si
uadilifu."
Akaniuliza: "Umeona?" Kwa sauti ya iliyokosa unyoofu
nilimjibu: "Ndiyo
mwanangu." Kwa hakika Nyambo alinithibitishia kuwa yeye ni
mzaliwa hasa
wa kizazi cha kuhoji. Kwa siku hiyo alinitoa 'nokauti'
kwa hoja zake
nzito. "Sijui shuleni kwao mwalimu huwa anawapigisha stori
za siasa,"
niliwaza, maana kwenye madaftari yake hakuna somo la
siasa.
Nyambo katika ubora wake: "Nilisoma pia Mwenyekiti wa
Chadema Kanda ya
Mashariki, Mabere Marando alimhusisha moja kwa moja Lowassa
na ufisadi
wa fedha Benki Kuu kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA),
vilevile
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amekuwa mshereheshaji
sana wa
ufisadi wa Lowassa. Sasa leo tunaona nini?
"Sasa chama kipi ambacho hakizingatii maadili katika
kupitisha majina ya
wagombea? CCM au Ukawa? Mtu ambaye kwa zaidi ya miaka nane
ameimbwa
nchi nzima kuwa ni fisadi, leo hii anasafishwa kienyeji tu!
Eti mbona
hakupelekwa mahakamani, walitaka apelekwe na nani kama
waimbaji ni wao
wenyewe?
"Yaani wewe mwenyewe utoe tuhuma halafu baadaye umsafishe
uliyemtuhumu
kwa sababu hakupelekwa mahakamani na unaongezea hakuna
mwenye ushahidi
aliwahi kujitokeza. Kwa hiyo ulikuwa unatoa tuhuma za uongo
kufurahisha
genge? Unajijenga kisiasa kwa uongo! Yaani baba usipowachapa
hawa Ukawa
na mimi hunichapi tena."
Kwa sauti ya unyenyekevu, nilimwambia: "Basi mwanangu
malizia homuweki
tukalale." Akaja juu: "Nimekwambia simalizii mpaka
uniahidi utawachapa
mijeledi Ukawa, waongo sana! Yule Godbless Lema aliwahutubia
wananchi
Arusha kuwa kumkataa na kumzomea Lowassa ni jambo lenye
heshima kubwa
kwa nchi kwa sababu ni fisadi, leo anatamba kuwa Safari ya
Matumaini
inaendelea Chadema, huyu naye ni muongomuongo lazima
umchape.
"Wanajitetea eti Lowassa hakuwa tatizo bali mfumo uliopo
CCM, wakati
kila siku walimtaja moja kwa moja kwamba ni tatizo. Naibu
Katibu Mkuu wa
Chadema, John Mnyika alisema CCM inamlinda Lowassa kwa
sababu upo
ushahidi wa ufisadi wake, leo hii CCM wamemkataa kuwa
mgombea Urais,
Chadema na Ukawa wamemkubali, nani anamlinda?"
Nilimwangalia, akanisistiza nijibu swali. Nikamwambia sijui,
akaendelea:
"Hujui eeh! Hivi Ukawa wanaposema tatizo ni mfumo, mfano
mtu akiwa
anaishi nyumba jirani, kila siku mnalamika hamlali
anawaibia, siku
akihamia nyumbani kwenu ndiyo mnasema tatizo la wizi wake
lilisababishwa
na nyumba aliyokuwa anaishi? Baba nijibu utawachapa
huwachapi?"
Kwa upole ikabidi nimwambie: "Nitawacharaza mijeledi
waongo sana hao."
Nilijibu hivyo ili kumaliza ubishi. Akasema: "Hapo sawa,
nami namalizia
homuweki yangu nikalale. Usipowachapa hatutaelewana, siyo
unaniitikia
tu. Na ukiwachapa uwaambie mimi ndiye niliyekutuma
JamboLeo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment