Saturday, 29 August 2015

Re: [wanabidii] LOWASSA UNA TATIZO

Asante Nanyaro

On Aug 29, 2015 11:12 PM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Nimemsikiliza na kati ya hotuba zenye malengo mema kwa wananchi hii ni mojawapo. Inatekelezeka. Kwa kuzingatia mameno aliyoyasema Magufuli (kuwa yuko tayari kujifunza kutoka vyama vingine) ninaamini yale ambayo hayamo kwenye irani ya CCM atayatekeleza pia.
--------------------------------------------
On Sat, 8/29/15, Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] LOWASSA UNA TATIZO
 To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Saturday, August 29, 2015, 11:05 PM

 HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA
 CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA



 YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU



  Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015



 Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu



 1.      Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka
 ishirini na
 tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya
 upinzani wa
 CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba
 ya Wananchi
  kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea
 mmoja katika
 ngazi zote.



 2.      Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa
 serikali za CCM
 na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi
 madaraka na
 mali za nchi.



 3.      Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta
 mabadiliko ya kweli nchini.



 a.      Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya
 mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.



 b.      Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii
 kama elimu, afya, maji na makazi.



 c.       Mabadiliko ya kuondoa umaskini.



 d.      Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya
 kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za
 maisha.



 4.      Kila mwaka hali na ubora wa  maisha ya
 Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa
 linakuwa.



 5.      Lakini  Watanzania wanachotaka siyo
 takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na
 barabara bora zinajengwa.



 6.      Wanataka kupata maji safi na salama ya
 kunywa. Wanataka makazi bora.



 7.      CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta
 mabadiliko ya
  kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa
 umaskini,
 maradhi,na ujinga inahitimishwa.



 8.      Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye
 mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.



 9.      Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto
 nyingi za
 ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya
 sera za
 utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini.  Sote ni wahanga
 wa siasa na
 sera hizi.



 10.  Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka
 mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.



 11.  Tusidanganyike, CCM hawana jipya.



 12.  Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha
 ya wananchi.



 13.  Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia
 maendeleo kwa
 vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali
 hii.
 Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa
 wananchi wa
 kanda ya ziwa wanapata maji safi.



 Ndugu watanzania

 14.  CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza
 umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.



 15.  Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa
 mikakati sahihi na siyo nadharia.



 16.  Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa
 sekta bali wa
  sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji
 wa sera za
 kila sekta utakao leta maendeleo.



 17.  Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini
 utakuwa na nguzo tano:-

 a.      Kupunguza matumizi ya serikali na
 mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.

 b.       Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti
 ukwepaji na
 misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika
 sekta
 muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji

 c.       Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu
 ikiwa ni
 pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za
 madini,
 kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa
 wanyonge.

 d.      Kuimarisha huduma za umma kama elimu,
 afya, maji na makazi, na mazingira

 e.       Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki
 na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.



 18.  Chini ya misingi hii na ili kufanikisha
 mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya
 yafuatayo:-



 ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA

 Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu
 kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.



 Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu
 itatayogharamiwa
 na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi
 Chuo Kikuu na
  pia:-



 1.      Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na
 ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri  na ushindani katika
 soko la ajira.

 2.      Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya
 elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.

 3.      Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote
 nchini.

 4.      Kuimarisha  taaluma na mitaala katika
 mashule.

 5.      Kuondoa utoro darasani, na
 kuboresha afya za wanafunzi.

 6.      Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa
 walimu ikiwa  ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia,
 usafiri na zana za teknolojia.

 7.      Kufuta michango ya maabara ya shule za
 kata



 AFYA

 1.      Afya na tiba ya kila Mtanzania
 itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya
 hifadhi ya jamii

 2.      Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na
 kinga kupunguza gharama za tiba.

 3.      Serikali itahakikisha kuna uwiano na
 upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili
 kuleta tija na huduma stahiki.

 4.      Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na
 kujenga
 hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na
 jamii na pia
 kuepukana na tiba za nje ya nchi.

 5.      Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi
 na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na
 nyumba na usafiri.

 6.      Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma
 za afya bila
  kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile
 serikali na
 hospitali za sekta binafsi.



 ARDHI, MAJI NA KILIMO



 1.      Tutaimarisha  mfumo wa umiliki wa ardhi
 kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya
 wakulima na wafugaji.

 2.      Tutapima ardhi yote ya Tanzania na
 kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili
 kuipa thamani.

 3.      Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa
 kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na
 kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.

 4.      Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa
 kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.

 5.      Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na
 kulinda vyanzo vya maji.

 6.      Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa
 wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na
 kujenga miundombinu husika.

 7.      Tutaweka mazingira rafiki
 yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na
 salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa
 mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa

 8.      Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa
 wakulima na wafugaji.

 9.      Tutasimamia kilimo cha biashara
 kinachozingatia maslahi ya nchi na  ya Watanzania.

 10.  Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao
 asilia ya Tanzania hususan mkonge.

 11.  Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na
 Uvuvi.



 MIUNDOMBINU

 1.      Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga
 mpya kama
 vitega uchumi vya  Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza
 kwa bandari
  za nchi jirani.

 2.      Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia
 ubora hasa zile za vijijini.

 3.      Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya
 kisasa

 4.      Tutajenga shirika la Ndege la Taifa
 linalojiendesha kwa misingi ya faida.

 5.      Tutajenga miundombinu ya kisasa na
 kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es
 salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha

 6.      Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa
 umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano
 ya Watanzania



 VIWANDA



 1.      Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili
 wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu

 2.      Tutajenga viwanda vipya vya kusindika
 mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

 3.      Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano
 mali ghafi
 zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili
 kuongeza
 mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.

 4.      Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda




 UCHUMI

 1.      Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili
 kuhakikisha
 kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii
 ambapo nguvu
  za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa
 mapato
 unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa
 ufanisi.

 2.      Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani
 kwa kuwapa
 Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili
 waimarike na
 waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu
 upendeleo
 katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri
 ya biashara
 na kodi endelevu.

 3.      Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya
 biashara kwa masharti nafuu kabisa.

 4.      Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye
 tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala
 maslahi kwa Taifa.

 5.      Tutaimarisha sera ya ubia baina ya
 Serikali na Sekta
 binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia,
 kuwawezesha
  Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye
 mitaji mikubwa
  bila kujali wanapotoka.

 6.      Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha
 mfumo wa Vyama
 vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima
 wenyewe ikiwa
 na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa
 kushirikiana
 kujenga nyumba bora

 7.      Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa
 viwanda
 vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na
 vyuo vya
 ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.



 AJIRA

 1.      Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana
 kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri

 2.      Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha
 ajira kwa
 wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na
 kuzipa unafuu
  wa kodi ili zikue kwa haraka.

 3.      Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta
 hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.



 NISHATI NA MADINI

 1.      Serikali itashiriki kikamilifu katika
 uzalishaji wa nishati

 2.      Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera
 yatakayovutia na kuwezesha ushiriki  wa Watanzania na ubia
 kati yao na wageni.

 3.      Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa
 umeme wa
 maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe
 kipaumbele namba
 mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme
 wa urana
 kipaumbele namba nne.

 4.      Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye
 usambazaji wa
  huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga
 masoko ya ndani,
 ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.

 5.      Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya
 nishati na madini  ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia
 maboresho.

 6.      Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa
 zake kwenye
 raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini
 kama rehani
 kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo
 mbinu ya
 mabomba ya gesi.

 7.      Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi
 kwa wazawa
 wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa
 wageni
 wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.



 8.      Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya
 kodi isiyo
 lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza
 kwenye kuongeza
 thamani ya raslimali zake za madini.

 9.      Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa
 mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni



 MALIASILI NA UTALII

 1.      Tutasimamia uvunaji na matumizi ya
 rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi
 hiki na kijacho

 2.      Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha
 utunzanji wa hifadhi za taifa  na mazingira

 3.      Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya
 utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na
 kuimarisha mafunzo

 4.      Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion
 mbili ifikapo 2020.



 UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA
 RAIA

 1.      Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za
 msingi za
 wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na
 viongozi,
 Bunge na Mahakama.

 2.      Tutaboresha miundobinu ya sheria na
 kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya
 wafanyakazi

 3.      Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya
 sheria
 kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti
 jela kwa sababu
  za kisiasa.

 4.      Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi
 hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa
 kusimamia utoaji wa haki.

 5.      Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na
 usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi






 UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI

 1.      Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania
 aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku

 2.      Tutaimarisha nidhamu, utendaji na
 uwajibikaji katika Sekta ya Umma

 3.      Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu,
 wanawake na
 vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira
 stahiki ya kazi
 pamoja na mafao.

 4.      Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika
 sekta ya Umma na binafsi

 5.      Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya
 serikali ikiwa ni
  pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa
 muhimu
 pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya
 mashangingi
 serikalini.

 6.      Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na
 ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki  jinsi
 yalivyotumika

 7.      Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika
 shughuli za
  serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni
 pamoja na ile
 ya mafuta, madini na gesi asilia





 KUKUZA PATO LA SERIKALI

 1.      Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali
 kwa kupitia
 upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia
 ili
 kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.

 2.      Serikali itaanzisha Wizara maalum
 itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.

 3.      Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina
 ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na
 mapato yake.

 4.      Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma
 yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.

 5.      Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa
 forodha na
 kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni
 ya fedha
 yanayopotea kila wiki.

 6.      Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu
 wa kulipa
 kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti
 makusanyo ya
  kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama
 afya na
 elimu kikamilifu.





 KUIMARISHA MUUNGANO

 1.      Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa
 Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa



 WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE

 1.      Wanawake watapewa fursa na haki sawa
 katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.

 2.      Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya
 kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya
 uzazi

 3.      Tutaimarisha elimu ya watoto hasa
 wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto
 wadogo.

 4.      Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika
 ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia
 hamsini ifikapo 2020.

 5.      Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya
 kujikimu
 inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa
 heshima na
 kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.



 SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO



 1.      Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa
 na michezo

 2.      Tutarudisha viwanja vya michezo
 vilivyovamiwa

 3.      Tutafuta kodi zote za vifaa vya
 michezo.

 4.      Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa
 za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia

 5.      Tutajenga taasisi  na vyuo vya kukuza
 michezo ili
 kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki
 kwa ushindi
 katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha

 6.      Tutalinda Hakimiliki za sanaa
 nchini

 7.      Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii
 chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.



 SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA



 1.      Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa  wenye tija
 na Ujirani mwema.



 2.      Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na
 kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya
 kimataifa.



 3.      Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa
 Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa
 Mataifa.



 4.      Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja
 na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi
 shiriki.



 Ndugu Watanzania



 Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo



 1.      Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua
 nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.



 2.      Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili,
 uzoefu na
 nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi
 jasho lenu na
 uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka
 utawala wa CCM
 unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika
 kuondoa
 umaskini.



 3.      Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa
 hadaa ya hongo
  ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za
 uchaguzi kwa
 kupewa pesa au vitu.  Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM.
 Ukikubali
 basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio
 madarakani.
 Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague
 mabadiliko.



 4.      Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda
 tofauti.
 Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna
 dharura ya
 maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini
 kuwa sisi
 kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta
 maendeleo yetu
 wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi
 zimefanikiwa
  kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka
 kwao.



 5.      Tuwe taifa linalotumia raslimali zake
 kujiendeleza na
 siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana
 katika nchi
 yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na
 kuvaa
 umaskini kama joho la fahari.



 6.      Mabadiliko  ya kweli hayawezi kuletwa na
 CCM.
 Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa
 miaka
 thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa.
 Miaka hamsini ya
  CCM imetosha.



 7.      Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu
 Watanzania mpo
 nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako
 ndiyo
 itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda
 kura yako.
 Wakati wa mabadiliko ni sasa.



  Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana
 2015-08-29 21:07 GMT+03:00
 'francis kinyawela' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:

 Hata
 kama ni kupiga kampeni au kujipendekeza, hapa bado. Kafanye
 review ya kazi yako halafu tuma tena 
 Sent
 from Yahoo Mail on Android  From:"'Happiness
 Katabazi' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date:Sat, Aug 29, 2015 at 20:54
 Subject:[wanabidii] LOWASSA UNA
 TATIZO



 LOWASSA
 UNA TATIZO
 Na
 Happiness Katabazi
 LEO
  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua
 rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani
 Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni
 sana.
 Nimefuatulia
 kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye
 Televisheni.Nimewasikia wote waliopewa nafasi ya kuzungumza
 a amezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu,
 Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote
 aliyoyasema Sumaye siyo mapya.
 Lakini
 wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo
 kwasababu Sumaye ambaye  amewahi kugombea urais mara mbili
 kupitia CCM na hakufanikiwa.
 Enzi
 akiwa   Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi
 kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE  VIZURI
 UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii
 ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.
 Nirudi
 Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.Mada hiyo nitajadili
 uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA,
 Edward Lowassa
   Leo  saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia
  alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
 Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo
 kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam,
 hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao
 watapata Sababu.
 Kwasababu
 hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo
 hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website
 ili wananchi waisome.
 Jamani
 , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo
 Siriazi kuutaka urais wa Tanzania. 
 Leo
 Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais
 kuja  Uwanjani kueleza wanachi atayafanyia nini kupitia
 Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .
 Lakini
 Lowassa Hilo Leo lime mshinda kashindwa  kueleza kwa
 wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake
 akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu
 kabisa.
 Mgombea
 urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa
  kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba
 yako badala yake Utaiweka Kwenye website? 
 Tumuulize
 huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na
 umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini
 Kwenye masoko .
 Sasa
 Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone
 wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia
 website? 
 Jibu
 ni Jepesi Watanzania Wengi
  hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka
 Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.
 Sasa
 ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa
 kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu
 utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?
 Maana
 hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye
 ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa
 Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu
 ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?
 Kama
 Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini
 wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa
 kusimama jukwaani usome hotuba yako?
 Lowassa
 unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati
 umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni
 zako? 
 Kama
 ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa
 kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo
 ?Simngeweka
  hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.
 Hilo
 limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha
 naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda
 Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au
 mhadhara  kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa
 Moja?
 Kwanza
 Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es
 Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini
 walianza kukuchukia?
 Polisi
 wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo
 zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii
 ndiyo wanakuchukia? 
 Lowassa
 wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele
 ya watu tunaofikiri sawa sawa.
 Leo
 umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo
 mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa
 Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye  eti amefanyakazi
 nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.
 Hili
 Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu
 umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.
 Na
 pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya
 kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu
 huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga
 vijembe.
 Sielewi
 kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki
  mna misimamo  inayoyumbayumba na ya
  msimamimii maneno yenu?
 Itoshe
 Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema
 mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.
 Sura
 ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni
 Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais
 Jakaya Kikwete na serikali na CCM.
 Na
 kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe
 Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na
  kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati
 akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi
 Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.
 Yaani
 mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama
 jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya
 Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO  Sheikh Farid
 na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza
 hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya
 UKAWA?
 Lowassa
 Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua
 utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika
  uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina
 maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na
 kwasababu gani?Kama unajua utaibiwa kura zako kwanini
 unaamasisha wananchi wakupige kura?.
 UKAWA
 simnajitapa Kuwa  mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa
 wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na
 wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi
 hamna wanausalama UKAWA?
 Hivi
 Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa
 rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu
 Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi
  kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya
 mzaa na usanii wa wazi kabisa.
 Lowassa
 jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi
 walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi
 walilokuwa wanalitajarajia  kutoka kwako hawajalipata
  maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.
 Kumekuwa
 na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa
 Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho
 cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda
 kumalizika.
 Je
 hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya
 kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi
 kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.
 Mungu
 ibariki Tanzania
 0716
 774494Facebook:
 Happy KatabaziBlogg: www.katabazihappy.blogspot.com29/8/2015











 Sent from my
 iPad



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




 --
 Ephata
 Nanyaro
 P.o.box 15359
 Arusha
 +255 754
 834152Skype.nanyaro.ephata
 "truth shall set you
 free"




 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment