Saturday, 29 August 2015

Re: [wanabidii] du kumbe alianza kitambo

Sikumbuki kama hata hapa hakupata nafasi ya kujitetea. nakumbuka iliandikwa na alistahili kuwajibu vijana. labda atatusaidia tusije tukamhukumu bila kujieleza.
--------------------------------------------
On Thu, 8/27/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] du kumbe alianza kitambo
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, August 27, 2015, 8:55 PM



Lowassa
kiboko

Na Saed Kubenea - Imechapwa 02
September 2008


Asaini mkataba pekee yake

Makamba: Tutaita Kamati Kuu

MKATABA wa kitegauchumi cha ujenzi wa
jengo la Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) umechukua sura mpya
baada ya wajumbe wa
Baraza la Wadhamini mmoja baada ya mwingine, kumkana
mwenyekiti wao, Edward
Lowassa.


William Lukuvi, ambaye amepata kushika
nafasi mbalimbali za
uongozi katika serikali, CCM na UV-CCM anasema,
"Sijahajawahi kushiriki katika
kikao kilichopitisha maamuzi ya ubia kati ya UV-CCM na
muwekezaji."

"Sina
chakuficha. Kama ningeshiriki ningesema.
Sijashiriki, na hivyo ndiyo ninavyoweza kusema mahali popote
pale. Kwamba
mkataba ule siujui," anasema Lukuvi"


Hatua hii ya Lukuvi kukana mkataba
inamweka pabaya Edward
Lowassa aliyeweka saini mkataba huo. Lukuvi anasema mkataba
baina ya UV-CCM na muwekezaji ameuona
kwenye gazeti. "Nilisoma katika gazeti lako, kwamba
hamjanipata. Ahaa," anasema
huku akiengua kicheko.

Akiongea kwa uchungu, Lukuvi anasema,
"Mimi sijawahi
kushiriki katika kupitisha maamuzi hayo. Hapa hakuna jambo
la kuficha. Si tabia
yangu kutenda mambo kwa kificho. Mimi ni muwazi …ndiyo
maana nasema
sijashiriki. Nahili nitalisema popote
nitakapoulizwa."


Gazeti hili liliripoti mwezi mmoja na
nusu uliopita, kwa
mara ya kwanza, kuwa Baraza la Wadhamini la UV-CCM chini ya
Lowassa lilisaini
mkataba wenye thamani ya zaidi ya Sh. 30 bilioni, kati yake
na makampuni mawili
ya uwekezaji, bila wenye chama kujulishwa na
kuridhia.


Mara baada ya taarifa hiyo, Lowassa
alinukuliwa akitishia
MwanaHALISI kwamba atalifikisha mahakamani kwa kile
alichosema, "Limezoea
kunizushia na kunichafua." Hadi sasa hajakwenda mahakamani
na wala hajaleta
malalamiko yake rasmi.

Lukuvi anasema ni vema ukafahamu
kwamba "mimi sikushiriki.
Katika vikao nilivyohudhuria,, hatukuwahi kujadili suala
hilo. Nataka kila mtu
abebe mslaba wake."


Lukuvi aliyepata kushina nafasi
mbalimbali za uongozi katika
UV-CCM tangu enzi za Youth League, ikiwamo Kaimu Katibu Mkuu
wa UV-CCM kati ya
mwaka 1992 hadi 1993, Mkuu wa Kitengo katika UV-CCM kati ya
mwaka 1984 hadi
1989 anasema, "Ni kweli kwamba mimi ni mdau ndani ya
UV-CCM. Lakini si katika
mambo ya kuangamiza umoja wetu. Humo mimi simo."


Mjumbe mwingine, Dk. Mary Nagu
ameliambia MwanaHALISI juzi
Jumatatu, kwamba hajawahi kushiriki maamuzi ya kupitisha
mkataba huo.

Dk. Nagu
anasema, "Mimi ni msema kweli. Mimi
nimehudhuria kikao cha juzi tu," kikao  ambacho
kilifanyika wakati wa
mkutano wa Bunge.


Anasema ndani ya kikao hicho ambacho
kilifanyika mjini
Dodoma wakati wa mkutano wa Bunge uliokwisha, aliwataka
wenzake waache kufanya
mambo gizani.

"Kama unazungumzia mkataba wa awali,
mimi ni kama anavyosema
Yusuf (Mjumbe kutoka Zanzibar) kwamba nimeona mkataba katika
kikao
kilichofanyika majuzi.

Kabla ya hapo mimi sikujua kama tayari
mkataba
umesainiwa," anasema Dk. Nagu.

Ni ndani ya kikao hicho, Dk. Nagu
anasema, "Nikawaambia
jamani haya mambo yaende kama yanavyotakiwa ili kuepesha
yale yaliotokea katika
UWT."

Anasema, "Nikawambia mtengeneze
mambo haya vizuri, ili
kuepesha yale ya UWT. Muandae  kila nyaraka na
mtekeleze kila
kinachotakiwa, kisha mpeleke katika vikao
vinavyohusika."


Kabla ya hapo, Dk. Nagu anasema
hajawahi kulisikia jambo
hilo. "Labda kwa kuwa mimi huwa mara kwa mara nasafiri.
Lakini hata kama
ingekuwa hivyo, ningejulishwa. Mimi ni mjumbe halali,
ningejulishwa," anasema
kwa hali ya kulalamikia chama chake.


Kwa uchache tayari wajumbe watatu
wamekana kuhusika na
mkataba huo wa kinyonyaji, huku mjumbe mwingine ikidaiwa
kulazimishwa na
Lowassa kuwa shahidi wake. Duru za ndani ya UV-CCM zinamtaja
mjumbe
aliyelazimishwa kuwa ni Amos Makalla.


Taarifa zinasema Makalla aliitwa na
Lowassa ofisini kwake na
kuelezwa kwamba asaini mkataba huo. "Unajua kwamba Lowassa
alikuwa Waziri Mkuu na hakuna
aliyetarajia kama angeanguka, zaidi ya kupanda. Katika
mazingira hayo, Makala
asingekuwa na ubavu wa kumkatalia Lowassa. Lakini ninavyojua
Makalla
hakubaliani na mkataba huu," alisema kiongozi mmoja wa
UV-CCM aliyekaribu na
Makalla.

Alipoulizwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph
Makamba kuhusiana na
hatua ya wadhamini kukana mkataba huo alisema, ""Kama
haya unayonieleza ni ya
kweli, basi kuna tatizo.



Makamba alielezwa na mwandishi wa
gazeti hili ofisini kwake
kwamba wajumbe karibu wote wa Baraza la Wadhamini ambao
wameongea na
MwanaHALISI wamekana kuhusika katika mkataba huo.


"Mimi ninamuhtasari wa kikao
unaonyesha kuwa hawa watu
walikutana na kujadili. Sasa kama kuna watu wanakana,
tutawaita katika Kamati
Kuu (CC) watueleze," alisema Makamba. 



Alisema mpaka sasa msimamo wa chama
chake ni kupeleka
mkataba huo katika kikao cha CC. "Huko ndiko tutakakwenda
kuulizana,"
alisisitiza.

Alipoambiwa kwamba baadhi ya
walionatajwa kushiriki katika
kupitisha mkataba si wajumbe wa CC akiwamo Lowassa mwenyewe,
Makamba alisema,
"Ndiyo, lakini tutawaita."



Hata hivyo, Makamba hakusema kama
tayari wameshajulishwa juu
ya kuitwa kwao.

Wakati Makamba anasema mkataba wa
ujenzi wa mradi
unaokadiriwa kufikia Sh. 40 bilioni kati ya UV-CCM na
mfanyabiashara Subhash
Patel unafikishwa CC, kwa maamuzi ya mwisho, Baraza Kuu la
UV-CCM, limesema
halikuhusishwa katika suala la mkataba huo, huku Makamba na
Lowassa wakidai
kuwa mkataba haujafikiwa wala kuwekwa saini.


Mjumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM na
Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), Nape Nnauye alisema tarehe 22 Julai mwaka huu kwamba
baraza la Lowassa
halikuwa na madaraka ya kufikia maamuzi hayo kwa sababu
"Baraza Kuu la UV-CCM,
lenye mamlaka ya uamuzi wa mwisho, lilikuwa halijaridhia
mkataba huo."

Mkataba ambao Makamba anasema
unafikishwa kwenye CC, bado
umejaa utata kutokana na kuwapo vipengele vinavyosema
"mkataba huu ni sehemu ya
mkataba ule."



Maneno hayo yanathibitisha hoja ya
MwanaHALISI kwamba
kilichosainiwa na Lowassa ni mkataba halisi na si
makubaliano ya awali kama
alivyodai yeye. Mbali na Lowassa wengine ambao wanaweza
kutumbukia katika
matatizo kutokana na mkataba huu, Mwenyekiti wa UV-CCM
Emmanuel Nchimbi na
Kaimu Katibu Mkuu Isack Francis ambao wanatuhumiwa kuwa
vinara wakuu wa
mkataba.


Nchimbi ndiye mwenyekiti wa vikao
vyote vya UV-CCM;
hajaonekana kuchukua hatua. Isack ni Kaimu Katibu Mkuu,
wakati mkataba
unasainiwa alikuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa UV-CCM.
 



Katika hatua nyingine, kuna taarifa
kwamba baadhi ya wajumbe
wa Baraza Kuu la UV-CCM wanakusudia kwenda mahakamani
kushitaki Baraza la
Wadhamini, iwapo Kamati Kuu ya CCM itaupitisha mkataba huo
bila kushirikisha
Baraza lao.


"Katika hili wala hatutanii. Kanuni
za chama zinazuia
wanachama kwenda mahakamani kwa ajili ya shughuli za
kisiasa. Kanuni hazizuii
kwenda mahakamani kutetea mali za chama," alisema mmoja wa
wajumbe wa Baraza
anayewakilisha wenzake ambaye hakutaka kutajwa
gazetini.


Tayari Yusuph Mohammed Yusuf mjumbe wa
Baraza la Wadhamini,
anayewakilisha Zanzibar amekana kushiriki kupitisha mkataba
huo uliosheheni
utata.

Yusufu ambaye ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Mjini Magharibi,
Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC), alisema, "Baraza la
Wadhamini halijawahi
kukutana kupitisha mkataba huo."


"Mimi ni mjumbe wa Baraza. Kama
mkataba ni ule mlioandika
kuwa ulisainiwa 2 Januari 2007, hakika siufahamu; sikuwahi
kukutana na wenzangu
na kukubaliana kusaini mkataba huo," amesema Yusufu.



Alisema yeye hafahamu na wala
hakumbuki kama Baraza la
Wadhamini chini ya Lowassa iliwahi kukutana na kukubaliana
juu ya kusainiwa kwa
mkataba huo.

Yusufu amesema walipelekewa mkataba na
kuelezwa kuwa ni
"maelewano" na kusema kuwa waliyapitia na "tukaagiza,
kwa vile yalivyo sharti
yapelekwe katika CC ya chama chetu."
chanzo Mwanahalisi






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment