Monday, 31 August 2015

[wanabidii] Re: "Anashangazwa na wapinzani kusema watajenga reli na kufufua ATC wakati hiyo ni ni mipango ya serikali ya CCM"

  Nashindwa nianzeje kujenga hoja kujibu usemi wa waziri wa uchukuzi, labda niseme hivi, je CCM haina mpango wowote kuhusiana na elimu, afya, kilimo, biashara na maeneo mengine ya maendeleo?  Kwa nini kuhusu hayo maeneo mengine hajayataja kuwa wapinzani wanawaiga?

Kapeini za CCM zingelilenga kuelezea wanataka kufanya nini kwa Watanzani na siyo kusema kwa nini wengine wana mipango kama ya kwao.

Kwanza kabisa kitu cha kushangaza kuliko vyote ni kuona mipango mingi na mikubwa kuzinduliwa wakati wa kampeini. Huo ni usanii na unyama wa ajabu sana, yaani pesa za maendeleo kwa shughuli mbali mbali zitalimbikizwa bila kutumiwa kwa faida ya wananchi, ili siku za kampeni zikifika utasikia, mara mabasi yaendayo kasi yaanza, Gesi imezinduliwa, ujenzi wa reli unefuuliwa na hiyo ATC nayo yafufuliwa kwa nini vitu hivyo havikufanika miaka mnne mitano iliyopita.

Kuhusiana na ATC, ni mara kadhaa chini ya uongozi uliopo  iliwahi kufufuliwa, wakakodisha ndege sijui kutoka wapi, na mara zote ATC imeanza kwa nguvu ya soda, kesho yake mambo yanarudi pale pale. Je, waziri haoni kama ni majaribio ya kulifufua hilo shirikyika sana bila mafanikio? Safari zote zimemeza pesa za wananchi na hali imebaki pale pale?

Pengine ni wakati mwafaka watu wengine kujaribu, kulaumu nani ananakili mipango yako haisaidii, maana ni mipango hiyo hiyo iliyopo ya kufanya Tanzania iendelee, tungelikuwa tayari na njia nyingi za reli,  Shirika/mashirika ya ndge yanayofanya kazi kifanisi, na umeme wa kutumia gesi unafanya kazi, halafu wakati wa kampeni, mtu akasema anataka aongeze upanuzi wa hivyo vitu wakati ambapo hakuna umhimu wa kufanya hivyo hapo unaweza ukasema. Lakini kwa sasa Tanzania haina reli, waliyo facilitate kufa kwa reli ni hao hao CCM kwa kuruhusu uchukuzi ufanywe kwa maroli, wengine wakija na wazo linalofanana na la kwako inakuwa wanakunakili, ulikuwa wapi kuvifanya siku za huko nyuma?.

Hata kama wazo hilo lilikuwepo na mipango ilikuwepo, narudia, vipi uzinduzi wa miradi mikubwa mikubwa isubiri uchaguzi mkuu ndipo izunduliwe, kama si mipango ya kuwazuga watazania kuwa serikali inafanya kazi za maeelo! Na kwa namna hii hakuna maendeleo ya maana yatayofikiwa maana kila ki kiri kuja kutumika kama kichocheo cha kutafuta, watu hao hao wanarudi serikani, wanafanya usanii huo huo kila uchaguzi ukifika.

0 comments:

Post a Comment