Elisa,
Uwe unajipanga kabla hujakurupuka na kuanza kujibu. Naona ni kama unaongea peke yako hapa jukwaani, gatimaye watu watu wanakuchoka sasa! Na hasa kuchoka zaidi na kauli zako.
Kuhusu afya, ni hiari ya mtu kusema au la.
Nakukumbusha ukasome sheria zilizopo, bila kuacha sheria ya Kupambana na Virusi vya UKIMWI ya Mwaka 2008, uuone mziki mnene uliomo humo. Hao hl wagonjwa ndo walioipitisha na kusaini. Mkishaisoma, naamini wao, na wewe mtafunga midomo na hasa wako.Come on! Usiwe unaongea ovyo tu!
Hebu sasa wewe , na hao wanaomsema Lowassa anaumwa, anzeni kupima walau Virusi vya UKIMWI kisha mtuletee majibu hapa kwenye mtandao, tuanze kusambaza kwanza majibu ya kwako.
.Shukuruni Sumaye kuna wagonjwa , ya nani, hakuyataja.
Wee endelea tu kumchunguza bata...
SB
Acha ushabiki usio na tija Kapime kwanza, lete majibu yako hapa, ndipo uanze kuwasema wengine
On Aug 30, 2015 8:25 AM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Watanzania wamekuwa na mashaka makubwa juu ya afya ya mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA. Sababu kubwa ya mashaka ni kuwa wasije wakamchagua mtu ambaye mbele akasababisha kurudiwa kwa uchaguzi kutokana na rais kushindwa kutimiza madaraka yake. Jambo hili kamwe halistahili kuwa hoja ya majukwaani. Haistahili kuanza kujadili afya ya mtu maana ikifikia hatua hiyo inakuwa si swala la itikadi. Kila mmoja anaguswa. Ni vibaya kabisa kugeuza afya ya mtu jambo la jukwaa la kisiasa. Kwa kweli si ustaarabu kuanza kujadili Fulani anaumwa. Hakuna shida kusema Fulani hafai kutokana na tabia au mwenendo wake. Lakini si afya. Afya mtu haamui bali hujikuta anaumwa.
> Katika jukwaa la kisiasa Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amewaeleza watanzania kutohoji afya ya Lowasa kwa sababu hata marais waliotangulia waliwahi kwenda kutibiwa. Amewataja Rais mkapa na Kikwete. Ameeleza kuwa mtu akishafika miaka 50 basi afya yake lazima itakuwa na matatizo. Kitu ambacho hakusema ni kuwa Lowasa haumwi. Amewaacha watanzania kutafsiri na kuamua alimaanisha nini. Mimi ninadhani alitaka kututaarifu kuwa anaumwa kweli. Maana yake mfumo tulio nao hautusaidii kuwapima na kuwajua watu afya zao. Hii kwa kweli inastahili kuwa kazi ya Tume ya uchaguzi. Kuhakikisha haituletei wagonjwa.
> Sumaye ni kiongozi mwandamizi wa taifa hili. Anastahili kuonyesha upeo wa kufikiri. Sijui kwa nini ameshindwa kuonyesha hilo. Au hatumjui huyo ndiye Sumaye.
> Hivi tunaweza kumchagua mtu mgonjwa asiyejimudu kwa sababu mtu Fulani alipokuwa madarakani aliumwa? Sumaye haoni tofauti kati ya JK au Mkapa walioingia madarakani wakiwa wazima halafu wakaumwa wakiwa kazini? Huyu kiongozi wetu ana upeo gani? Haoni kuwa hili si swala la kushindaniwa majukwaani? Yeye anasema Ikulu hawabebi zege? Yaani hajawahi kusikia kuna mazingira rais anaweza kushindwa kumudu majukumu yake? Majukumu ya kubeba nini? Hiki kifungu tena kimo kwenye katiba ambayo Sumaye aliwahi kuapa kuilinda Jamani UKAWA kuzoa zoa kutakuja kuwaaibisha siku moja!
>
> Kama CHADEMA inataka kuja kubadili mfumo inastahili kumleta mtu anayetiliwa shaka kuwa rais wetu? Au inataka kuingiza mfumo wa kusimamisha wagonjwa. Ningeelewa kama wangesema tunataka watu wapimwe afya kabla ya kugombea yaani kuondoa mfumo wa kusimamisha wagombea tusiowajua au tulio namashaka nao. Kama tunahakikisha hatupitishi mgombea aliyewahi kuhukumiwa makosa ya jinai tunashindwa kumzuia mgonjwa kugombea urais?
> Nakumbuka sana 2005 Mtikila akiwa anajiandaa kumlipua JK kuwa ameathirika yeye (JK) akawahi kupimwa na kutangaza afya yake. JK angesema na Mbowe ni mgonjwa (2005 JK alishindana na Mbowe kwa karibu zaidi) tusingemuelewa maana hapo asingetoa mashaka yetu. Lakini alipopimwa na akatangaza afya yake watu wakajua wanachagua kiongozi atakaye maliza kipindi chake na ikitokea asimalize ni bahati mbaya.
> Mashaka ya watanzania kuhusu afya ya Lowasa yanaongezeka kila kukicha. Hata zilipotoka habari kuwa serikali imepiga marufuku usafiri wa helicopter kwenye uchaguzi mimi nilidhani (kama ni kweli) basi ni njama kutaka kumchosha Lowasa kwa kusafiri na barabara. Jana aliposema anakaa Dar kwa sababu ndicho kitovu na akawataka watu wa Dar wamuombee kura mikoani nikawaza hivi asiposafiri kwenda kuomba kura itakuwaje? Kwa nini CDM ikafanya maamuzi magumu kabla kampein hazijapamba moto? Inataka kutuletea ya 2005 uchaguzi kucheleweshwa tena?
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from i
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment