Hapoyness una haraka sana na wewe sio mwandishi wa habari bali msaka tonge hapo umeshaliwa na kupigwa bao huna tofauti na mtumwa mtu gani usiyebadilika hat mtoto anakua na kuwa mtu mzima viongozi wako wanaimba mabadiliko magufuli anaimba mabadiliko Lowasa naye anaimba wewe umesimama kama kibao cha kuelekeza wenzako dada yangu hebu piga hatua
On Aug 30, 2015 12:29 AM, "Erick Maro" <rikmaro@gmail.com> wrote:
-- Asante Nanyaro
On Aug 29, 2015 11:12 PM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:--Nimemsikiliza na kati ya hotuba zenye malengo mema kwa wananchi hii ni mojawapo. Inatekelezeka. Kwa kuzingatia mameno aliyoyasema Magufuli (kuwa yuko tayari kujifunza kutoka vyama vingine) ninaamini yale ambayo hayamo kwenye irani ya CCM atayatekeleza pia.
--------------------------------------------
On Sat, 8/29/15, Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] LOWASSA UNA TATIZO
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, August 29, 2015, 11:05 PM
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA
CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka
ishirini na
tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya
upinzani wa
CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba
ya Wananchi
kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea
mmoja katika
ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa
serikali za CCM
na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi
madaraka na
mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta
mabadiliko ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya
mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii
kama elimu, afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya
kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za
maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya
Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa
linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo
takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na
barabara bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama ya
kunywa. Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta
mabadiliko ya
kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa
umaskini,
maradhi,na ujinga inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye
mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto
nyingi za
ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya
sera za
utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga
wa siasa na
sera hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka
mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha
ya wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia
maendeleo kwa
vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali
hii.
Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa
wananchi wa
kanda ya ziwa wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza
umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa
mikakati sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa
sekta bali wa
sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji
wa sera za
kila sekta utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini
utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na
mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti
ukwepaji na
misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika
sekta
muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu
ikiwa ni
pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za
madini,
kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa
wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu,
afya, maji na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki
na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha
mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya
yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu
kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu
itatayogharamiwa
na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi
Chuo Kikuu na
pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na
ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika
soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya
elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote
nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika
mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na
kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa
walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia,
usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za
kata
AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania
itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya
hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na
kinga kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na
upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili
kuleta tija na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na
kujenga
hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na
jamii na pia
kuepukana na tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi
na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na
nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma
za afya bila
kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile
serikali na
hospitali za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi
kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya
wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na
kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili
kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa
kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na
kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa
kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na
kulinda vyanzo vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa
wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na
kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki
yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na
salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa
mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa
wakulima na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara
kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao
asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na
Uvuvi.
MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga
mpya kama
vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza
kwa bandari
za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia
ubora hasa zile za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya
kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa
linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na
kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es
salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa
umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano
ya Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili
wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika
mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano
mali ghafi
zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili
kuongeza
mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda
UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili
kuhakikisha
kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii
ambapo nguvu
za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa
mapato
unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa
ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani
kwa kuwapa
Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili
waimarike na
waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu
upendeleo
katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri
ya biashara
na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya
biashara kwa masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye
tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala
maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya
Serikali na Sekta
binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia,
kuwawezesha
Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye
mitaji mikubwa
bila kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha
mfumo wa Vyama
vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima
wenyewe ikiwa
na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa
kushirikiana
kujenga nyumba bora
7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa
viwanda
vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na
vyuo vya
ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana
kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha
ajira kwa
wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na
kuzipa unafuu
wa kodi ili zikue kwa haraka.
3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta
hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
1. Serikali itashiriki kikamilifu katika
uzalishaji wa nishati
2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera
yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia
kati yao na wageni.
3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa
umeme wa
maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe
kipaumbele namba
mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme
wa urana
kipaumbele namba nne.
4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye
usambazaji wa
huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga
masoko ya ndani,
ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya
nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia
maboresho.
6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa
zake kwenye
raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini
kama rehani
kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo
mbinu ya
mabomba ya gesi.
7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi
kwa wazawa
wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa
wageni
wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.
8. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya
kodi isiyo
lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza
kwenye kuongeza
thamani ya raslimali zake za madini.
9. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa
mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya
rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi
hiki na kijacho
2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha
utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya
utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na
kuimarisha mafunzo
4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion
mbili ifikapo 2020.
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA
RAIA
1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za
msingi za
wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na
viongozi,
Bunge na Mahakama.
2. Tutaboresha miundobinu ya sheria na
kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya
wafanyakazi
3. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya
sheria
kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti
jela kwa sababu
za kisiasa.
4. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi
hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa
kusimamia utoaji wa haki.
5. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na
usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania
aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na
uwajibikaji katika Sekta ya Umma
3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu,
wanawake na
vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira
stahiki ya kazi
pamoja na mafao.
4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika
sekta ya Umma na binafsi
5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya
serikali ikiwa ni
pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa
muhimu
pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya
mashangingi
serikalini.
6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na
ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi
yalivyotumika
7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika
shughuli za
serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni
pamoja na ile
ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali
kwa kupitia
upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia
ili
kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
2. Serikali itaanzisha Wizara maalum
itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina
ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na
mapato yake.
4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma
yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa
forodha na
kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni
ya fedha
yanayopotea kila wiki.
6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu
wa kulipa
kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti
makusanyo ya
kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama
afya na
elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa
Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa
katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya
kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya
uzazi
3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa
wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto
wadogo.
4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika
ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia
hamsini ifikapo 2020.
5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya
kujikimu
inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa
heshima na
kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa
na michezo
2. Tutarudisha viwanja vya michezo
vilivyovamiwa
3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya
michezo.
4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa
za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza
michezo ili
kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki
kwa ushindi
katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa
nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii
chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija
na Ujirani mwema.
2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na
kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya
kimataifa.
3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa
Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa
Mataifa.
4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja
na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi
shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua
nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili,
uzoefu na
nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi
jasho lenu na
uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka
utawala wa CCM
unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika
kuondoa
umaskini.
3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa
hadaa ya hongo
ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za
uchaguzi kwa
kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM.
Ukikubali
basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio
madarakani.
Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague
mabadiliko.
4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda
tofauti.
Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna
dharura ya
maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini
kuwa sisi
kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta
maendeleo yetu
wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi
zimefanikiwa
kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka
kwao.
5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake
kujiendeleza na
siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana
katika nchi
yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na
kuvaa
umaskini kama joho la fahari.
6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na
CCM.
Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa
miaka
thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa.
Miaka hamsini ya
CCM imetosha.
7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu
Watanzania mpo
nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako
ndiyo
itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda
kura yako.
Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana
2015-08-29 21:07 GMT+03:00
'francis kinyawela' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Hata
kama ni kupiga kampeni au kujipendekeza, hapa bado. Kafanye
review ya kazi yako halafu tuma tena
Sent
from Yahoo Mail on Android From:"'Happiness
Katabazi' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date:Sat, Aug 29, 2015 at 20:54
Subject:[wanabidii] LOWASSA UNA
TATIZO
LOWASSA
UNA TATIZO
Na
Happiness Katabazi
LEO
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua
rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani
Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni
sana.
Nimefuatulia
kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye
Televisheni.Nimewasikia wote waliopewa nafasi ya kuzungumza
a amezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu,
Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote
aliyoyasema Sumaye siyo mapya.
Lakini
wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo
kwasababu Sumaye ambaye amewahi kugombea urais mara mbili
kupitia CCM na hakufanikiwa.
Enzi
akiwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi
kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE VIZURI
UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii
ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.
Nirudi
Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.Mada hiyo nitajadili
uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA,
Edward Lowassa
Leo saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia
alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo
kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam,
hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao
watapata Sababu.
Kwasababu
hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo
hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website
ili wananchi waisome.
Jamani
, hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo
Siriazi kuutaka urais wa Tanzania.
Leo
Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais
kuja Uwanjani kueleza wanachi atayafanyia nini kupitia
Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .
Lakini
Lowassa Hilo Leo lime mshinda kashindwa kueleza kwa
wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake
akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu
kabisa.
Mgombea
urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa
kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba
yako badala yake Utaiweka Kwenye website?
Tumuulize
huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na
umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini
Kwenye masoko .
Sasa
Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone
wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia
website?
Jibu
ni Jepesi Watanzania Wengi
hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka
Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.
Sasa
ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa
kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu
utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?
Maana
hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye
,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa
Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu
ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?
Kama
Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini
wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa
kusimama jukwaani usome hotuba yako?
Lowassa
unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati
umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni
zako?
Kama
ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa
kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo
?Simngeweka
hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.
Hilo
limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha
naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda
Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au
mhadhara kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa
Moja?
Kwanza
Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es
Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini
walianza kukuchukia?
Polisi
wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo
zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii
ndiyo wanakuchukia?
Lowassa
wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele
ya watu tunaofikiri sawa sawa.
Leo
umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo
mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa
Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye eti amefanyakazi
nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.
Hili
Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu
umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.
Na
pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya
kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu
huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga
vijembe.
Sielewi
kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki
mna misimamo inayoyumbayumba na ya
msimamimii maneno yenu?
Itoshe
Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema
mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.
Sura
ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni
Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais
Jakaya Kikwete na serikali na CCM.
Na
kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe
Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na
kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati
akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi
Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.
Yaani
mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama
jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya
Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO Sheikh Farid
na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza
hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya
UKAWA?
Lowassa
Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua
utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika
uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina
maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na
kwasababu gani?Kama unajua utaibiwa kura zako kwanini
unaamasisha wananchi wakupige kura?.
UKAWA
simnajitapa Kuwa mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa
wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na
wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi
hamna wanausalama UKAWA?
Hivi
Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa
rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu
Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi
kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya
mzaa na usanii wa wazi kabisa.
Lowassa
jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi
walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi
walilokuwa wanalitajarajia kutoka kwako hawajalipata
maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.
Kumekuwa
na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa
Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho
cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda
kumalizika.
Je
hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya
kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi
kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.
Mungu
ibariki Tanzania
0716
774494Facebook:
Happy KatabaziBlogg: www.katabazihappy.blogspot.com29/8/2015
Sent from my
iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Ephata
Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754
834152Skype.nanyaro.ephata
"truth shall set you
free"
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment