Friday, 14 November 2014

Re: [wanabidii] WAMASAI WANAPAMBANA NA JAMII NYINGINE WILAYANI KITETO

Tatizo ni watanzania kuweka SIASA mbele kulinda KURA na KULA badala ya kuzingatia ethics za Kazi, Sera na sheria. Watu wa mifugo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wafugaji wanafuga kulingana na carrying capacity ya ardhi. Pia kilimo wanalima sustainably.

Lakini hatuzingatii wote hata pale wananchi wanapoelimishwa. Kwa nini unalishia mazao ktk shamba si lako na mwenyewe akija kufukuza mifugo isile mazao unamtandika bakora asiondoe aiache ile chakula mpaka kumuua muhusika. Kwa wanawake-wanabakwa kama adhabu. Mikumi kijana wa kimasai alimbaka bibi kizee na kisha kutoroka akiwa korokoroni police katorokaje? (kahonga).

Anachapwa kiongozi wa kijiji na mkulima mshitaki kiongozi akiwa amewaita kuamua kesi ya kulishia shamba. Wanawapa watoto kuchunga katika mashamba ya watu kwa makusudi ili kusingizia-watoto hao wazembe hawajui kitu. Si haki hata kujitesa na kujionea wenyewe wakati mwingine analimbikiza mifugo kifahari.

Ukifika Dodoma kijiji (Ibwaga) cha MP msaidizi wa Makinda bungeni mifugo hadi milimani na kilimo hadi milimani kwenye mawe ambayo hufanywa yawe loose na mito imejaa michanga. Mvua kubwa ikija mawe yanaweza kuzika watu. Kwa nini kiongozi asikemee jimboni kwake kukomesha maovu? Kwa nini University of Sokoine Morogoro, Idara ya ardhi na Mzumbe waachie wananchi wanalima milimani na kujenga mpaka juu kabisa katika hali hatarishi. Chuo cha Utawala (mzumbe), cha ardhi Moro,  na cha kilimo na ufugaji vinashindwa kusaidia proper land use planning na elimu ya matumizi bora katika miaka yote toka vianze kwa kuweka programme ya kupata donor funds (DHV-SNV, Finida, etc money)? Practical field work ya wasomi si ingekuwa kuumaliza mkoa huo kwanza ambako mapigano ndi donda kuu na uharibifu wa vyanzo vya maji na misitu maji?

Ukifika Handeni mifugo haikai ilikopangiwa wanakwenda maeneo ya wakulima eti wanafuata huduma (na mifugo inapita njia nyembamba, kuharibu na kuingia mashambani). Wananyweshea ndani ya mabwawa ambayo wenzao ni source ya maji ya kunywa na walilipia 20% ya total cost ya msaada waTASAF. Nao mifugo ni utajiri,wafugaji  wakichanga na kukaa walikopangiwa wanaweza kujenga mabwawa sio bwawa moja pia boreholes, dip na manywesheo ila kiburi wanaingiza makusudi mabwawa ya kunywa binadamu.

Sio Handeni tu kwenye matatizo-hadi Ngerengere, Kilosa  mpaka irrigation scheme zimeharibika (Malolo Tarafa ya Mikumi) na ya Ruvu chini Bagamoyo-Makurunge village etc. Lori zinashusha mifugo porini usiku na utakutana nazo zinahama usiku. Viongozi, police wanaziona. kwa sasa Dawasa inahaha na source za maji ya bomba na pia kuhaha kujenga Bwawa la Maji Kidunda Dam huko juu  source ya Mto Ruvu, Mgeta na Mkulazi ili Mkoa wa Dar na coast upate maji. Hata hivyo kuondoa mifugo Mto Ruvu, Ngerengere na milimani juu Mgeta ni kazi kubwa Morogoro Rural and South.  Na kwa sasa, mifugo inazunguka kupanda Udzungwa range kwa kupitia Ruaha, Msimba ipande iingie Chonwe na udunghu Kidodi and Vidunda ward na sasa na ipo ndani ya Mikumi na Saadan National Park.

Mabonde ya Mikumi hayalimiki kwa sasa. Viongozi wa chini, police, mahakimu-Rushwa. maneno yanayotetea uovu- Msiwasumbue wapiga kura wangu; kipato cha chini wanaganga njaa-suluhisheni, wawekeni kikao yaishe. Haya si maneno mazuri ya utii wa sheria. Ndio yanayofanya watu wafanye watakavyo kuharibu urban planning na rural livelihoods na mazingira. Utii wa sheria must kwa wote.

Pimeni ardhi, Land use planning nchi nzima na certification ni vital; kupiga marufuku kuhamahama; kuvamia misitu na kuchimba hovyo na kutumia kemikali zinazosababisa cancer za koo na maradhi mengine kwa watumia hayo maji. Marufuku kuuza ardhi uliyopewa bila ya kibari  cha wizara husika na mahakama. Na kama ardhi isingewekwa chini ya Rais ingeuzwa kama maandazi na hata sasa wanapewa Mabwepande-wanauza wanarudi bondeni na hawabomolewi.

Kumepimwa mwananyamala, kinondoni-wanaziba njia zote wanaweka frame za biashara; barabara nzima mapishi ya moto na feeder roads zimezibwa, open space za kucheza watoto, bustani ni garage, viosk, magari yamejaa mpaka barabarani ni biashara na welding za hatari na pembeni food vending. Vumbi la gari, mchanga, fumes za petroli ndani ya chakula wazi. Moto ukiwaka na kuunguza nyumba gari ya zima moto haina pa kupita-viongozi na watumishi wa umma husika wanaangalia tu. Wazimu mtupu. Hakuna anayejali hali hii inazidi kukua.

Urban planning haitofanikiwa kwa kujenga nyumba za NHC nje ya miji kutatua msongamabno na uchafu mijini. Ni kwa kubomoa kwa nguvu kutumia sheria pale inapovunjwa. Huko nje ya miji ardhi ya kilimo mnaichukua kujenga Cities-mnaongeza prostitution na HIV. Vizee vinakosa pa kulima chakula, ninyi ni kuongeza EPZ na cities (kibaha city, Chalinze city, Handeni city, Kigamboni city etc) ni mauaji. Arable land kuichukua watu hawana social security fund na food stamps for survival. Watauza vitoto ili wapate hela ya chakula. Sheria za ardhi zimetafsiriwa na vitini vya participatory land Use Planning vipo mpaka kwa Kiswahili-tunangoja nini? Igharimiwe mbona posho za bunge ni mamiliopni na Land use planning kwa kijiji ni millioni 10 tu???

Ni aibu pia kuwa na University of Agriculture and Livestock, Livestock multiplication units, vyuo vya maendeleo lakini huko huko mapigano ufugaji kienyeji wa kuhamahama, kilimo kisicho endelevu ndio kimetawala kama Kawa; land degradation ndio chronic disease na milima ipo degraded adjacent na chuo cha kilimo na ufugaji. Practical training yao ni wapi? Ni sawa na kuwa na course za civil and construction engineering lakini hapo chuoni ngazi zote za concrete zimebomoka kila unakopita na mpaka material testinga lab ya maijinia ceiling board imebomoka inaning'inia. Unafika nje ya Chuo cha maji mto uliozunguka chuo haupo protected, raia wanachimba mchanga, wanatupa taka ngumu na kuunganisha vyoo; wanajenga mabanda ya biashara na magari kukatiza hovyo ndani ya eneo la chuo nacho kinaangalia tu; Ukifika chuo cha Public Health Enginers vyoo vimefurika unakaribishwa na harufu ya kinyesi. Haya yote yanatokea Bongoland. Unajiuliza-tumemkosea nini Mungu-hatuoni yote haya?

Kwa nini pale tulipo tusiwe mfano kuunganisha theory with practice? Tunaona mauaji vijiji vyuo vilipo na pia land degradation-adopt vijiji viwe vya field practice `kutatua matatizo. Mbona hatuchukui hatua? Sio Anna Tibaijuka pekee-sekta zote kila mtu pale alipo kwa nafasi yake. Tunaona uhamaji na uvamizi misitu, ukataji miti hovyo-leseni tunatoa za nini? Panda miti kibiashara ndio ukate uuze!!

Sheria ya kila mtu akae kwake sasa itekelezwe kuzuiai kuhamahama kwa kilimo na ufugaji na sekta nyingine pia zimulikwe (uvuvi na matumizi ya mabomu kuvulia; misitu kuchoma mkaa porini wanapewa leseni??!!). Inanikera sana, niatamani niendelee kuandika tu kukemea!!*~X( at wits' end
 



On Friday, 14 November 2014, 20:35, Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:


ukweli ni prof tibaijuka kashindwa kazi, hana weledi na kielelezo cha
watanzania waishio nje ya nchi kuwa hawana uwezo kikazi na wasaka
tonge zaidi.

On 11/14/14, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
> Hali tuliikuta mbaya vijiji vya Matuli, Diguzi,  Chanyumbu, Kidunda kuelekea
> Kisarawe ukitokea Ngerengere township Morogoro Rural hadi upandishe Mgeta
> milimani. Kuna wafugaji wa Kimasai, Mang'ati, Mbulu, Sukuma. Kulishia
> mashamba na owners kuchapwa bakora na baadhi kukatwa mapanga kufa. Usifukuze
> mifugo iliyoingia shambani kula hapo utakula bakora. Mwenyekiti wa Kijiji
> Kibubwa cha Kidunda na wa kitongoji kijiji cha Chanyumbu katika kuamua
> ugomvi wa mfugaji kulishia shamba wamepigwa wao na walioharibiwa mashamba.
> Uvunaji wa madini Geita, Mererani, Loiboisirret (manyara) na maeneo mengine
> kwa wafugaji yanaongeza mifugo kwani pesa hutumika kuongeza wealth status
> kupitia mifugo. Ardhi haiongezeki. Tatizo nao huko kwao wanalima badala ya
> kununua mazao wanaokoa hela. Lakini iwe Mwanza, Shy, Magu, Dunda, Musoma
> rural, Manyara-Orkusumet, Terrat, Landanai au Kiteto, Kilosa,
> Loliondo-Engerosambu, Soitsambu au Ngorongoro NCAA-Olbalbar, Endulen etc
> -mfugaji anayelima hata siku moja hatoingiza mifugo kulishia mimea yake.
> Lakini atatoka atokako kilomia mamia afike Mbeya, Kilwa, Kilosa-atalishia
> apendavyo. Ardhi haiongezeki. Kama kila mkulima akilima sustainably na
> mfugaji kufuga sustainably haya mapigano yataisha. lakini hata pale penye
> zonal livestock multiplication unit-hatuigi kufuga kisasa, kununua mitaba au
> kwenda kupandisha wetu au kununua mbuzi wa kisasa atoae lita 3 za maziwa kwa
> siku. Kiteto ni bread basket ya mahindi na nafaka nyingine mapogano
> yanaharibu food security pande zote. Muhimu sasa serikali kugharimia land
> use planning and titling kila mtu apate hati miliki ya kimila kwa mtu au
> kikundi au formal title ya wizara ya individual au kundi. Pia, kila mtu akae
> kwake. Kuruhuzu watu kutoka mkoa mmoja na makundi ya mifugo kwenda mkoa
> mwingine au kuhama haka kwa kilimo na mifugo hatutoisha kuuana. Pata hati
> kaa kwako na pia kuhakikisha wingi wa mifugo unalingana na available land.
> Kufuga kienyeji kwa kuhamahama kumepitwa na wakati. Pia kilimo cha
> kuhamahama kuvamia misitu ya hifadhi ya kijiji au central GVT. Tunza chako
> ukitumie kwa busara. Watu wanauza ardhi halafu wanahama kuvamia misitu au
> wetland areas. Bado hao wavamizi wachimba madini lakini hela wanachofanyia
> cha maana hakuna ni ulevi machimboni, anasa, ukimwi. Tutafika kuushinda
> uchumi kweli ta tamia hizi za mwaka 1947? Kuuana mpaka lini? Usipoingia
> kulishia shamba la mwezio ugomvi utatoka wapi? Tuache tabia za kijinga.
>
>
>
>
>      On Thursday, 13 November 2014, 21:06, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
> wrote:
>
>
>  Tafadhali piga 0715 009929 ni askari wanaelekea eneo la tukio unaweza
> kuwapa habari zaidi .
> On Thu, Nov 13, 2014 at 8:32 PM, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:
>
> Hali ni mbaya sana muda huu katika kata ya Oliboloti baada ya mapigano
> makala sana kuanza muda mfupi uliopita baina ya Wamasai na jamii nyingine ,
> na taarifa nilizopewa na diwani wa kata hiyo wa CUF ni kuwa mpaka sasa
> wameshakufikia watu wanne na majeruhi kibao kwani wananchi wa jamii nyingine
> wameamua kuchukua gobore zao na mapigano yanaendelea .
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
> --
>
> Yona Fares Maro
> Institut d'études de sécurité - SA
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

>
>
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment