Saturday 29 November 2014

Re: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO

Huyu dada naye ni controversial figure!! Haaminiki kama kweli anaongelea haya from objectivity point of view, or under undue influence ya wanao mchukia ZZK!!


--------------------------------------------
On Sat, 11/29/14, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "Wanazuoni" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Saturday, November 29, 2014, 10:47 AM

ZITTO
KABWE UNAJIANDALIA ANGUKONa
Happiness KatabaziMTUME
Muhammad S.A.W amewahi kunukuliwa akizitaja alama kuu tatu
za mnafiki. Ambazo ni ; "Mnafiki akisema anasema
uongo,mnafiki akiaidi hatimizi na mnafki akiaminiwa
,haaminiki'.Nukuu
hiyo ya Mtume inapendwa mno kutumiwa na rafiki yangu ambaye
ni Mbunge wa Jimbo la Rombo (Chadema), Joseph
Selasini,katika harakati zake za kisiasa tangu nimfahamu
akiwa Chama Cha NCCR-Mageuzi.Na
nanukuu hiyo ndiyo imekuwa kama salamu yangu mimi na yeye
pindi tunapowasiliana kwa simu au kukutana hana kwa ana na
mwishowe tunaishia kucheka sana kutokana na sifa hizo za
Mnafiki.Alhamisi
wiki hii huko Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) ,
Jaji Fredrick Werema akiwa bungeni alimuumbua Mbunge wa
Kigoma Kaskazini ,Zitto Kabwe kwa vielelezo kuwa Zitto
alishakiri chini ya kiapo ofisini kwa Jaji Werema kwamba
hana majina wala akaunti za watu hao , kinyume cha kauli
yake huko nyuma alipowahi kusema kuwa anawajua.Jaji
Werema alilazimika kusema hayo muda mfupi bungeni baada ya
Zitto kusisitiza kuwa serikali haionyeshi nia ya
kuwachukulia hatua walioficha fedha hizo nje ya
nchini.Jaji
Werema ambaye ni Mwanasheria Kitaaluma aliigeukia taaluma
yake na kuanza kutoa vielelezo vinavyopinga kauli hiyo ya
Zitto kwamba serikali haina nia ya kuwawajibisha walioficha
fedha hizo, ambapo Jaji huyo alisema Februali 28 mwaka 2013
, Kamati iliyoundwa kuchunguza kama fedha hizo ni haramu ,
kutambua benki walizoficha , kuandaa mashitaka na kisha
kuishauri serikali."Februali
28 mwaka 3013, Kama "Februari 28, mwaka 2013, Kamati
ilikutana hapa bungeni katika ofisi yangu na ilipomuita
Mheshimiwa Zitto aje atoe ushahidi, alikuja akatwambia anazo
nyaraka na taarifa ila akaomba ahakikishiwe usalama ili pale
ambapo angezileta pasingelikuwa na mtu wa kumzonga."Pia,
alitaka mimi nitoe kiapo ambacho baada ya kutaja hayo majina
halafu ikawa siyo kweli, basi yeye awe 'free' (huru),
kwa hiyo alitaka apewe kinga ya kiapo."Machi
23 tulipomuita aje akatukwepa, akasema anakwenda Tanga
kwenye mafunzo ya mgambo, kwa hiyo, tukaona tumsubiri hadi
atakapomaliza."Aprili
12, mwaka 2013, tukakutana naye hapa Dodoma katika viwanja
vya Bunge, akasema hawezi kutwambia chochote kwa sababu
alikuwa akijiandaa kwenda Afrika Kusini."Mei
4 tulimuita tena kwenye kamati hapa Dodoma na katikati ya
mahojiano alidai ana jambo muhumu lenye maslahi kwa taifa,
akasema anaomba aondoke atarudi, kamati ilimruhusu, hata
hivyo hakurudi tena."Tulipompigia
simu alisema alikuwa Dar es Salaam na alikuwa 'busy'
akijiandaa kwa kongamano la Kigoda cha Mwalimu
Nyerere."Mei
24 kamati ilimfuata Dar es Salaam, akasema hana nafasi kwa
sababu wakati huo alikuwa akijiandaa kuisaidia Timu ya
Taifa," alisema Jaji Werema na kuongeza:"Kamati
iliamua sheria ichukue mkondo wake kwa mujibu wa Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Kifungu cha sita ndipo
tukachukua maelezo ya Zitto Kabwe chini ya kiapo na
akatwambia hakuwa na jina, wala akaunti ya Mtanzania yeyote
aliyeficha fedha nje."Lakini,
leo hapa amesema serikali haina nia ya kurudisha fedha
zilizofichwa Uswisi. Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika,
Zitto Kabwe ni mzito na nakubaliana na Lema (Mbunge wa
Arusha Mjini) aliyesema hapa, kwamba Zitto alete majina
hayo.Itakumbukwa
kuwa kwa takribani mwaka mmoja sasa Zitto amekuwa
akilandalanda mitaani na kunukuliwa na vyombo vya habari
kuwa kuna vigogo wameficha fedha nchini Uswis na anawajua.
Kweli kwa watu wanaopenda kudakia mambo bila kufanyia
utafiti nao wakajikuta wanaiomba wimbo huo aliokuwa akiumba
Zitto.Ambapo
mwisho wa siku Jaji Werema ,Alhamsi ya wiki hii bungeni
alikuja kufumbua macho watanzania kuwa huyu huyo Zitto
aliyekuwa anatamba mitaani kuwa anawajua walioficha fedha,
aliitwa kwenye Kamati hiyo maalum ili akaisaidie kutoa hayo
majina ya namba za akaunti zao lakini hakwenda na matokeo
yake Zitto alikwenda ofisini kwa Jaji Werema chini ya hati
ya kiapo kuwa hayafahamu majina wala akaunti za watu
hao.Kisheria
tunasema kila tuhuma inayoibuliwa au kesi inayofunguliwa
mahakamani lazima iwe na mlalamikaji ambaye mlalamikaji huyo
anapaswa kufika katika mamlaka husika kuisaidia kutoa
vielelezo anavyodai kuwa watu fulani wamevunja sheria.Sasa
kwa muktadha huu ambapo Zitto aliaminisha umma kuwa kitendo
hicho cha kufichwa fedha nje ya nchi kimemkera na ushahidi
anao, kwanini Zitto huyu kwa zaidi ya mara nne ameitwa
kwenye Kamati hiyo akashindwa kufika kutoa vielelezo
hivyo?Je
alikuwa na lengo moyoni na akilini mwake?Maana tuhuma hizo
alizoziibua ni kubwa sana na serikali yoyote makini nilazima
tu ingeanza kufanyiakazi tuhuma hizo na hivyo ndivyo
ilivyofanya serikali ya Tanzania, baada ya Zitto kuibua
skendo hiyo , serikali iliamua kuunda kamati ya kuchunguza
ukweli wa tuhuma hiyo , lakini cha kustaajabisha muibuaji wa
skendo hiyo Zitto ambaye alikuwa akijitapa kuwa ana
ushahidi, hakuweza kwenda kwenye Kamati hiyo kutoa
ushahidi.Naweza
kusema pia kama yaliyosema na Jaji Werema ni kweli, basi
watanzania hatuna budi ya kumwambia Zitto tena bila haya
kuwa anaichezea serikali yetu sambamba na kuchezea
rasilimali watu na fedha za walipa kodi.Kwani
ni yeye aliyeshupalia skendo hiyo na serikali ikajikuta
inatumia fedha za kuunda kamati, kutumia rasilimali watu na
muda wa serikali muda kuja kuhoji watu mbalimbali ambapo
mwisho wa siku Zitto ndiyo alikuwa mtu muhimu sana wa
kuisaidia Kamati hiyo kupata ukweli wa tuhuma hizo lakini
cha kushangaza Zitto inaelezwa alishindwa kutoa ushirikiano
kwa Kamati hiyo.Kama
kweli maelezo ya Jaji Werema ni ya kweli,Je wananchi wamuite
Zitto ni Mnafiki ,Mzandiki, muongo, msahaulifu, au ni mtu
anayekurupuka?Maana
inashangaza kwa watu wenye kumbukumbu na Zitto kipindi kile
alivyokuwa amekomaa na skendo hiyo, leo hii Jaji Werema
anakuja kuliambia Bunge eti Zitto ameeleza chini ya kiapo
kuwa hana majina wala hafahamu akaunti za vigogo na kwamba
alikwepa kwenda kwenye Kamati kuhojiwa?Hapo
ndiyo ninampomheshimu Mbunge wa Vunjo(TLP), Agustine Mrema
enzi zile alipoibua kashfa wa wizi wa Sh.milioni 900 kwa
mawaziri wa serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa ikiongozwa
na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuwa wametafuna fedha hizo na
kweli Mrema alikubali kuhojiwa na Kamati ya Bunge na
akafunguliwa kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu na
alishinda kesi hiyo.Mrema
aliibua kashfa hiyo iliyomhusisha Rais Mkapa na baadhi ya
mawaziri wake kwenye mikutano yake kisiasa , na alipoitwa
kuhojiwa kwenye kamati ya bunge kipindi hicho hakukimbia,
alikwenda na akahojiwa na mwisho wa siku alifunguliwa kesi
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoka na kuibuka
kashfa hiyo ambayo upande wa jamhuri ulidai kashfa hiyo ni
uzushi, lakini mahakama ilimwachiria huru Mrema.Hivyo
Mrema awe ni funzo kwa wanasiasa wengine walioibuka hivi
sasa ambao wanajifanya mahiri sana wa kudai wanaibua tuhuma
za ufisadi lakini wakiitwa katika mamlaka husika kutoa
ushahidi huo ,wanakwepa.Aprili
12 mwaka 2012 gazeti hili lilichapisha makala yangu
iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho 'Zitto Kabwe
,Mbona U msahaulifu?Maudhui
ya makala hiyo nilikuwa namuelezea Zitto kumbe na yeye ni
jamiii ile ya baadhi ya wanasiasa wale wale wenye hulka za
kinyang'au ambao wanakasumba ya kuzungumza uongo mbele ya
umma, ili umma uwapende na uamini kuwa kiongozi huyo ni mtu
safi na mtetezi wa wanyonge, kumbe siyo kweli. Ieleweke wazi
hapo nyuma Zitto alipata bahati ya kupata umaarufu ndani ya
jamii kwa kile kilichoelezwa ni mwanasiasa kijana ambaye ana
misimamo thabiti na asiyeyumba katika kile
anachikiami.Sisi
waumini wa sheria tunasema tuhuma zitabaki kuwa tuhuma hadi
pale zitakapothibitika na mahakama au vikao husika vya chama
chake.Lakini kwa kuwa mungu ni mwema kadri siku zinavyozidi
kwenda mbele atazidi kutuonyesha kama kweli Zitto ni
mwanasiasa msafi ,mhadilifu kuliko wanasiasa wenzake
wanaotoka katika vyama mbalimbali vya siasa.Na
kweli utabili wangu huo umetimia kwa hivi karibuni Kamati
Kuu ya Chadema, ikatangaza kumvua nyadhifa zote ndani ya
chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa wamebaini kuwa Zitto
anakisaliti chama chao.Hali iliyosababisha baadhi ya
wanananchi kuanza kumtazama tofauti Zitto.Itakumbukwa
kuwa Zitto alikuwa msatili wa mbele kushinikiza baadhi ya
watumishi wa serikali na viongozi wakiwemo mawaziri na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda wawajibishwe kwa kile alichokuwa
akikidai kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao na wengine
wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali na kweli kuna
mawaziri waliondolewa kwenye baraza la mawaziri kwasababu ya
tuhuma hizo zilizokuwa zikiibuliwa na Zitto na mwisho wa
siku zikaungwa mkono na wananchi.Waswahili
wanamsemo wao usemao 'linalomkuta Boko na Mamba pia
litamkuta kwasababu wote wanaishi majini'. Kwa hiyo
yaliyowakuta baadhi ya mawaziri kwa kuondolewa kwenye baraza
la mawaziri kwa kigezo cha tuhuma tu...ndicho ambacho
kimemkuta Zitto leo hii kwa Kamati Kuu ya chama chake kumvua
nyadhifa zake zote kwa tuhuma kuwa ni msaliti.Iwe
Chadema walimsukia zengwe Zitto na kuamua kumpokonya
madaraka kwa kisingizio cha usaliti au ni kweli.Minaona
itakuwa ni funzo sasa kwa Zitto kujifunza kuwa siyo jambo
jema tena kwake kuendelea na kasumba yake ya kupenda
kushinikiza wanasiasa wenzake hasa wa CCM wawajibishwe au
kupokonywa madaraka kwasababu wanakabiliwa na tuhuma za
ufisadi na kuutaka urais mwaka 2015.Kwa
uzoefu wangu kwa wanasiasa wengi wa nchi hii ni mabingwa
kuwatengenezea wenzao majungu, fitna na mwisho wa siku
majungu wanayapeleka kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia
baadhi ya waandishi wa habari kuwachafua mahasimu wao na
kweli wanafanikiwa na majungu hayo kwa kuwachafua maasimu
wao na mwisho wa siku maasimu wao wanachafuka mbele ya jamii
na kama asimu wake ni mbunge, wananchi wake katika chaguzi
zijazo wananchi wake hawamchagui tena kwa kisingizio kuwa
mbunge wao huyo anakabiliwa na tuhuma za ufisadi kumbe
wakati mwingine ni uzushi mtupu.Ushauri
wangu kwa Zitto ni kwamba akubali kuwa ule umaarufu aliokuwa
nao zamani umeporomoka sana na hakuna ubishi kuwa
itamgharimu kipindi kirefu sana kuuurejesha ndiyo atashindwa
kabisa kuurejesha.Hivyo
ni vyema yeye binafsi ajipe muda na atafakari ni wapi
amekosea hadi leo hii kila kukicha umaarufu wake unazidi
kuporoka, uadilifu wake unatiliwa shaka na chama chake na
baadhi ya wananchi.Kwanini
Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema ameamua kumtolea
uvivu bungeni na kumuumbua kuwa Zitto kuwa aliitwa kwenye
Kamati hakufika kuhojiwa na alipoitwa ofisini kwa Jaji
Werema alitoa maelezo yake chini ya kiapo kuwa hana majina
ya vigogo wala majina ya akaunti za vigogo walioficha fedha
Uswiss.Naheshimu
mchango wa Zitto katika medani ya siasa nchini ila
sipendezwi na tuhuma mbalimbali zilizomzingira Zitto kwani
wananchi walionekana kumuamini Zitto kuwa ni mwanasiasa
msafi kuliko wengine lakini ghafla baadhi ya wananchi
wanaripotiwa kwenye vyombo vya habari wakisema hawana imani
naye tena.Kwa nini hili Zitto anaruhusu litokee?Pia
namshauri Zitto hivi sasa ni vyema akajiepusha kujadili
hadharani masuala yanayohusu uadilifu wa wanasiasa wenzake ,
kwani tayari nayeye hivi sasa anaandamwa na tuhuma hizo za
ukosefu wa uadilifu.Pia
awe makini sana na hao watu wanaomshauri kwenda kwenye
vyombo vya habari kujadili masuala kadha wa kadhaa kwani hao
hao leo hii wanaojifanya kukushauri kujadili masuala kadha
wa kadhaa mbele ya adhara ndiyo hao hao mwisho wa siku
watakucheka.Kwa
wanaoifahamu jamii ya Watanzania, tunaelewa kuwa Watanzania
wengi ni kama tuna ugonjwa wa usahalifu.Tunashikia bango
jambo fulani mwisho siku tunalisahau tunadandia hoja
nyingine.Ni
sisi watanzania tulishupalia wee Dk.Steven Ulimboka ,
Absalom Kibanda, mauji ya Daud Mwangosi, Idara ya Usalama wa
Taifa livyotuhumiwa na Chadema kuiba kura katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010,mgomo wa madaktari ,shinikizo la kutaka
aliyekuwa Waziri Mkuu Edwar Lowassa, na aliyekuwa waziri
Andrew Chenge wajiudhuru na kwamba ni mafisadi, vurugu za
kugombea ujenzi wa bomba la gesi Mtwara na vurugu za kisiasa
Arusha lakini leo hii nani tena anazungumzia mambo
hayo.Hakuna.Watoto
wa mjini tunasema hivi nyimbo zinazotamba Tanzania kwa sasa
ni kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
kile kinachodaiwa ni mgogoro ndani ya Chadema na Zitto
,Zitto kuvuliwa nyadhifa zake kwa madai kuwa ni msaliti
.Kwahiyo ni vema akatulia ,watanzania watasahau tuhuma
zake.Nimalizie
kwa kumtaka Zitto Kabwe, asikubali kuingia kwenye nukuu hiyo
ya Mtume Mtume Muhamad kuwa; ' "Mnafiki akisema anasema
uongo,mnafiki akiaidi atimizi na mnafki akiaminiwa
,aaminiki'.Mungu
ibariki Tanzania0716
774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili,Desemba 15 Mwaka
2013







--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment