huyu jamaa anaonekana anasoma.
Familia ya kambarage very complex ila interview nzuri
On Nov 27, 2014 1:55 PM, "Erick Maro" <rikmaro@gmail.com> wrote:
-- Mwalimu ameshaenda tuliopo tumeshindwa??
On Nov 27, 2014 2:22 PM, "Novatus Kambota" <novakambota@gmail.com> wrote:------------ Forwarded message ----------
From: Novatus Kambota <novakambota@gmail.com>
Date: Thu, 27 Nov 2014 14:20:52 +0300
Subject: Fwd: Andrew Nyerere; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi!
To:
---------- Forwarded message ----------
From: Novatus Kambota <novakambota@gmail.com>
Date: Thu, 27 Nov 2014 13:56:20 +0300
Subject: Andrew Nyerere; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi!
To:
Kuna maswala kadha wa kadha yanayoikabili Tanzania kwa hivi sasa,
miongoni mwa mambo haya ni sakata la akaunti ya Tegeta/Escrow,
mchakato wa katiba mpya na mengine mengi. Mwandishi Nova Kambota
amefanya mahojiano na Andrew Julius Nyerere ambaye ni mtoto wa kwanza
wa baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, fuatana naye katika mahojiano
haya………………
1. SWALI; Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza siku za karibuni ambayo
watu wanataka kufahamu manufaa yake kwa taifa, moja ya matukio hayo ni
ziara ya Jafar Mermo Idd Amin mtoto wa rais wa zamani wa Uganda
marehemu Idd Amin mwaka 2008, je ziara hiyo ambayo ilimkutanisha na
Madaraka Nyerere walipozuru Butiama ilikuwa na manufaa gani kwa taifa?
JIBU; Kwa familia ya Mwalimu Nyerere na familia ya marehemu Idd Amin
nadhani ilikuwa jambo zuri kuleta upatanishi, kuhusu kama taifa
lilipata faida sijui. Aliongea Jafari kuhusu kuanzisha mfuko wa hela
kuwasaidia wanajeshi walioathirika na vita vya Kagera(wa Uganda na
Tanzania), pia nchi hizi mbili zilihitaji kupatanishwa , Jenerali
Musuguri alikuwa anaongea katika redio miezi michache iliyopita,
kwamba wanajeshi wetu walikuwa na hasira sana, kabla ya kufika Kyaka
walikuwa wameshawaua watu 10,000(elfu kumi), Jenerali Musuguri yupo
hapa Butiama, natamani kwenda kumuuliza kama hao wote waliouwawa
walikuwa ni maadui kwasababu hii ilikuwa ni vita yetu ya kwanza,
inawezekana makosa yalifanyika.
2. SWALI; Una maoni gani kuhusiana na mwenendo wa CCM iliyoasisiwa na
Mwalimu Nyerere ambayo sasa baadhi ya viongozi wake wanatuhumiwa
vikali kujihusisha na ufisadi? Hudhani ni sababu tosha kwa watanzania
kuikataa CCM ikiwa inakiuka misingi ya kuundwa kwake?
JIBU; CCM iliamua kujiita Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya mapinduzi
yaliyofanyika Urusi au Uchina, kwa maana kwamba watu walio wengi
wakiwa na njaa wataleta fujo za kuiangusha serikali kama wamechochewa
au hata kama hawajachochewa. Iwapo CCM itaendeleza hayo mapinduzi
wananchi wataendelea kuichagua, inategemea tu watu wangapi bado
wanaamini inaendeleza mapinduzi, maoni yangu mimi siyo muhimu, watu
waamue, na nadhani wanaweza kugawanyika katika maamuzi.
3.SWALI; Miaka ya karibuni kumekuwa na watu wanaohoji namna baba wa
taifa Julius Nyerere alivyoaga dunia, baadhi ya wanasiasa wametilia
shaka mara kadhaa kifo chake mpaka ikampelekea Madaraka Nyerere kutoa
kauli, vipi mtazamo wako kuhusu hili? Kuhoji kifo cha Nyerere kuna
maslahi yoyote kwa taifa?
JIBU; Magige , mtoto wa Mwalimu anasema kuna chanjo moja ilikuwa
wapewe watanzania ambayo Mwalimu alikuwa ana mashaka nayo. Mwalimu
alimwambia Dr Mwakyusa kwamba yeye apewe, aijaribu halafu akiridhika
ataiidhinisha wapewe Watanzania, lakini alipopewa hiyo chanjo, Mwalimu
hali yake ilibadilika ghafla, amefariki. Niliposikia hiyo stori
nilimweleza Magige kuhusu Global 2000 Report ya Warren Christopher,
inasemekana katika miaka ya sabini viongozi wa Afrika walishauriwa na
IMF wakubali wananchi wao wachanjwe chanjo za magonjwa ili watu
wapungue ili iwe rahisi kuwasaidia; kwamba tatizo la kuwasaidia ni
tatizo la logistics tu. Inasemekana ushauri huo ulikubaliwa na
viongozi wetu. Global 2000 Report ni Top Secret ipo United Nations na
hata ukiwa kule huwezi kuipata mpaka uwe na Special Clearence. No,
nilimwambia Magige hatutapata faida yoyote tukianza kuuliza maswali
kuhusu kifo cha Mwalimu, kama kuna mtu anabisha kwamba World Health
Organization inaweza kufanya ufisadi, mtu huyo huwa anashauriwa
kufanya utafiti jinsi W.H.O ilivyoanzishwa.
4.SWALI; Unazungumziaje mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya nchini,
kutokana na matukio yanayoendelea kujitokeza kama Mzee Warioba kupigwa
na hali ya kutoelewana miongoni mwa watanzania, Je unaona wapi
tumekosea? Nini kifanyike kunusuru mchakato huu ili tupate katiba
itakayolivusha taifa letu kutoka hapa tulipo?
JIBU; Hakuna matatizo kuhusu katiba , isipokuwa kama kuna maoni
yanayoweza kuiboresha katiba , maoni mapya ambayo siyo ya UKAWA , sasa
ndiyo wakati wa kuyatoa.
5. SWALI; Unazungumziaje uongozi wa baba wa taifa hayati Mwalimu
Nyerere? Una lipi la kusema kwa kumlinganisha na viongozi wa zama
hizi?
JIBU; Sioni sababu ya kuwalinganisha viongozi wa awamu tofauti, zama
tofauti zinahitaji viongozi, kumlinganisha Nyerere na Kikwete hiyo
itakuwa sawa kumlinganisha Bismark na Angela Markel.
6.SWALI; Unazungumziaje harakati za vyama vya upinzani nchini
kupambana na ufisadi kama wa hivi karibuni wa Tegeta/Escrow? Unadhani
vyama hivi vya upinzani vina dhamira ya dhati kupambana na madudu?Je
vitafanikiwa?
JIBU; Vyama vya upinzani vina nia njema , hii kashfa inayojadiliwa
sasa hivi Bungeni imeletwa na upinzani. Hii vita ya sasa hivi ya
Bungeni wanaweza kushinda, lakini kushinda uchaguzi wa serikali za
mitaa ni jambo lingine.
7.SWALI; Kadri ulivyomwelewa hayati Nyerere, unazungumziaje kutokuwepo
kwake? Je unadhani angekuwepo angesaidia vipi kunusuru taifa kwenye
kupambana na ufisadi na kunusuru mchakato wa katiba mpya?
JIBU; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi, kuhusu katiba hakuna
tatizo kubwa au naweza kusema hakuna tatizo lolote zaidi ya fujo
inayoletwa na UKAWA.
8.SWALI; Ukipewa nafasi ya kuwashauri vijana wa sasa wa Tanzania,
ungependa wafanye nini kulisaidia taifa lao?
JIBU; Vijana wa Tanzania wafikiri sana kabla ya kuwachagua viongozi.
9.SWALI; Unapata tafsiri gani unapoona taasisi za kidini kama kanisa
katoliki likianzisha, kusimamia na kuratibu mchakato wa kumtangaza
hayati Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu?
JIBU; Kanisa katoliki ndiyo linataka Mwalimu aitwe lay saint, Mwalimu
aliishi maisha ya uadilifu lakini kama alikuwa mtakatifu hiyo ni kwa
Vatican kuamua.
10.SWALI; Unaweza kueleza nini kuhusu siku za mwisho za uhai wa
Mwalimu na namna alivyokuwa akilalamikia ubinafsishaji/uuzwaji wa
mashirika ya umma kama benki ya taifa ya biashara NBC, ukizingatia
hali ya ugonjwa wake na uzalendo wake kwa nchi, alikuwa mtu wa namna
gani? Alionekanaje nyakati zile?
JIBU; Uuzaji wa mashirika ya umma au ubinafsishaji siyo jambo baya wakati wote.
Swali; una lolote la kumalizia?
Jibu; Kwa kumalizia, nataka kusema viongozi wachaguliwe kwa uadilifu,
kwasababu ukiwachagua mafisadi, Mungu ataheshimu uteuzi wako,
hatabadili kitu chochote!
Andrew Nyerere anaweza kupatikana kwa namba 0718- 536281, ikiwa
unataka kuwasiliana na Nova Kambota mwandishi aliyefanya mahojiano
haya piga simu namba 0712-544237, barua pepe; novakambota@gmail.com au
tembelea http://novakambota.wordpress.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment