Sunday 30 November 2014

Re: [wanabidii] Go Pinda,nenda tu mzee wangu,mpe fursa JK aunde baraza jipya!

pinda komaa nao tu hamna kutoka wakikungoa ondoka na nyundo waachie jembe na shuka ya kijani, mbona hadi sasa hawajajiorodhesha wanaotaka utoke kama alivyofanya zitto wakati ule?

On Nov 25, 2014 1:41 PM, "Novatus Kambota" <novakambota@gmail.com> wrote:
Na Nova Kambota, 0712- 544237

Tofauti na wengi wanavyodhani, mzee wangu Pinda ulishaonyesha dalili
za wazi ikiwa kweli unamudu vyema nafasi ya uwaziri mkuu. Kuna mengi
tu yaliyofanya baadhi yetu tutilie shaka umahiri wako lakini hii
skandali ya Tegeta/Escrow imefunga mjadala!

Unakumbuka uliposema na wapigwe tu? Liwalo na liwe!
Wakumbuka ile kauli ya tumechoka?
Wakumbuka mgomo wa madaktari?
Je wakumbuka kauli yenye utata "anayeua albino na yeye auwawe"?
Lakini wajua namna "mchwa" katika baadhi ya halmashauri wanavyotafuna
fedha za wananchi?

Tegeta/Escrowni hitimisho la yote haya, mzee wangu Pinda mtoto wa
kulima, let it go! Jiuzulu, mpe fursa rais Kikwete aunde baraza jipya
la mawaziri, urais unaweza kutafutwa hata nje ya uwaziri mkuu!

Ukiwa mwanasheria utanielewa vizuri naposema hoja si ikiwa unahusika
au la! Hili si muhimu sana, hoja hapa ni dhamana ya uongozi kusimamia
shughuli za serikali ilishindwa kutumika kunusuru "skandali"hii.
Kiongozi waumma "kutuhumiwa" si jambo jema, tuhuma pekee zinatosha
kukufanya ubwage manyanga "resigning does not mean you are weak, but
sometimes it means you are strong enough to let it go"

Achia ofisi ya umma kwa manufaa ya walala hoi wa Tanzania, kiongozi wa
umma umetuhumiwa kutosimama kidete kuzuia uozo huu kabla, kauli za
"kila mtu atabeba msalaba wake" si za kulisaidia taifa, ni kauli
inayoashiria hamu ya mtawala asiyependa kuwajibika, anayetaka
kung'ang'ania madaraka! Haifai kabisa, busara inakutaka kuwajibika
kama mtangulizi wako Edward Ngoyai Lowassa, kumbuka "Caesar's wife
must be above suspicion''

novakambota@gmail.com , http://novakambota.wordpress.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment