Friday 28 November 2014

[wanabidii] Lamudi Tanzania kutangaza huduma za madalali bure

Lamudi Tanzania kutangaza huduma za madalali bure

[caption id="attachment_53532" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/11/Meneja-Huduma-kwa-Wateja-wa-Lamudi-Tanzania-Godwin-Lemma-akizungumza-na-waandishi-wa-habari-hawapo-pichani-leo-jijini-Dar-es-Salaam..jpg" alt="Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam." width="640" height="414" class="size-full wp-image-53532" /> Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.[/caption]
<strong>KAMPUNI</strong> ya Lamudi Tanzania, imetambulisha huduma yake ya kuwawezesha madalali mbalimbali wanaofanya kazi ya kuwatafutia nyumba, viwanja na magari wateja wao ili kuweza kutangaza huduma wanazotoa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma amesema kwa sasa madalali wanaweza kutangaza nyumba, viwanja na magari yaliyoko sokoni kupitia mtandao wa kampuni hiyo bila malipo yoyote.

Akifafanua zaidi Lemma alisema dalali anayependa kupata huduma hiyo anatakiwa kufika katika ofisi za Lamudi Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar  es Salaam (Garden Road) na kujaza fomu ambayo itaelezea huduma yake na kuanza kuitangaza kwenye tovuti www.lamudi.co.tz bila malipo yoyote.

"…Kimsingi huduma hii inawasaidia sana madalali kutangaza kazi walizonazo, bei zao na hata eneo ilipo. Mfano kama ni nyumba au kiwanja baada ya dalali kutoa taarifa za kutosha sisi tunamtangazia bure kazi hiyo kupitia tovuti yetu (www.lamudi.co.tz)," alisema Lemma.
[caption id="attachment_53533" align="aligncenter" width="486"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/11/Meneja-Huduma-kwa-Wateja-wa-Lamudi-Tanzania-Godwin-Lemma-akizungumza-na-waandishi-wa-habari-hawapo-pichani-leo-jijini-Dar-es-Salaam...jpg" alt="Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam." width="486" height="480" class="size-full wp-image-53533" /> Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.[/caption]
Alisema mbali ya kuwasaidia madalali kutangaza bidhaa zao wameanza kutoa pia mafunzo ya kuwajengea uwezo madalali kuweza kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi ili kujenga heshima ya kazi zao.

"Wakati mwingine tumekuwa tukifanya kazi ya kuchukua baadhi ya madalali na kuwajengea uwezo, kuwapa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi na masuala mengine ya msingi katika shughuli zao," alifafanua Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.

Pamoja na hao alisema kwa sasa kampuni ya Lamudi Tanzania  imezinduwa huduma mpya ya kumwezesha mteja kupata taarifa za uuzaji au ukodishaji nyumba ama viwanja kupitia simu za mkononi hivyo kumrahisishia kupata taarifa kwa wakati.
<strong>*Imeandaliwa na www.thehabari.com</strong>


________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment