Thursday, 27 November 2014

[wanabidii] MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA

MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA  YAKO NA CHAMA


Mheshimiwa Bi.Anna Tibaijuka (Mb) Waziri wa Ardhi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la Tageta ESCROW,kwani kiongozi huyu amekili wazi kuwa amepokea fedha Billion 1.6 kutoka kwa mmiliki
wa kampuni ya VIP Engineering Bw.James Rugimalira,tena si fedha ndogo.

Si jambo jema kumuhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka,lakini sio vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili,basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.

Msomi yoyote yule anapofikia ukiitwa Professor na tena waziri mwenye kushika
dhamana ya nchi na wananchi yaani Ardhi na makazi, ardhi ndio kila kitu kwa
watanzania,harafu akafikia sehem ya kukubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa
Shiling Billion 1.6 kutoka kwa mfanyi biashara ! naye Mhe.Anna Tibaijuka bila ya
kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana
na dhamana ya cheo chake ? hapa kwa mtanzania yoyote haingii akilini.
Litakuwa jambo bora kwa Mhe.Anna Tibaijuka kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora
kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine watafuata nyao.

Tunajua mtu apoitwa Professor sio msomi wa kawaida bali msomi aliefikia daraja
la juu kabisa,ndio maana tunaona msomi kama kiongozi wetu huyu ambaye anajua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa mawaziri wachache ambao wizara zao
zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii anakubali kununuliwa kiurahisi pia kufanya biashara akiwa katika madara mazito,kama atandelea kututumikia wananchi katika
wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi,tuna mashaka nae.

Watanzania tunajiuliza hivi Mhe.Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena katika wizara muhimu na huku akiwa mkurugenzi wa mashirika au shule na miradi binafsi au? ndio kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio
dhmana ya biashara zake ?
Hivi kuna hosptali ngapi hapa nchini azina dawa? je wakina mama wangapi wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule ngapi ? za serikali ambazo hazina madawati?
Leo Mheshimiwa ambaye tena ni Professor amepokea fedha Tsh.Billion 1.6
na kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu,watanzania tunamashaka nae.

Professor Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya 
viongozi wa umma " (Sheria namba13 ya mwaka 1993) ambayo inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa".

Sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii na juhudi za kiongozi wetu mhe.
Rais DKT.Jakaya Kikwete (mungu amuongezee afya njema),hautuwezi
kabisa kukubali au kuona kiongozi tena msomi Professor,anavunja dhamana
ya wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alikuteuwa.

Litakuwa jambo la busara sana Mhe.Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima
yako kama msomi Professor,pia kulinda heshima serikali na Chama tawala.
Uwezi kutumikia ofisi mbili utumishi wa umma na biashara.

Wanachi tunasikitika sana  kuona katika sakata la fedha za umma mpaka
baadhi watumishi wa mungu ambao ni viongozi wa kanisa nao wausika
na bila ya uwoga wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu mzidishie afya njema kiongozi wetu raisi 
Dkt.J.K



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment