Thursday, 27 November 2014

Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Tunaofuattilia mjadala Bungeni HATUDANGANYIKI. Tunabaini pumba na mchele. Ukweli  wenye vithibitisho wa ukweli  na  uongo wenye vithibitisho vya kuchonga. Tuendelee kufuatilia tuone mwisho utakuwaje lakini tusitoe visingizio vya Urais, Ubunge wala Udiwani.
 
On Thursday, November 27, 2014 8:43 PM, 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

mmmmh,lowasa na pinda mmmmh pinda hana ubavu bana, mkulima na mfugaji mmmm mkulima lazima atashindwa
 
From: 'john mushi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 11:21 AM
Subject: Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Hivi wewe Emma unayejaribu kulijua sakata na kumsifu Muhongo na majibu yake unaelewa kweli nchi iliko?Hivi ramani nzima unaiona na kuielewa?THINK BEFORE YOU .....PESA HIZO HATA KAMA NI ZAKO WEWE  BINAFSI  ZILIVYOTOLEWA TOLEWA  USINGESHTUKA? KWA HALI HIYO UTAENDELEA KUCHANGIA MAABARA NA MADAWATI NA MUHIMBILI UTAENDELEA KUWACHUKUA MAREHEMU WAKO MPAKA UTAKAPOZINDUKA! MUNGU AKUBARIKI EMMA NA WENGINE WOTE WA STAILI YAKO.

From: 'jabir yunus' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 9:43 PM
Subject: Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Emma unabakia na msimamo wako huo hata baada ya mchango wa Tundu Lissu, David Kafulila na Freeman Mbowe?

Utakuwa mtu wa ajabu sana.

Haya.

J

From: Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 7:08 PM
Subject: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Kwa aliyefatilia majibu ya waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo leo bungeni akijibu hoja za kamati ya PAC atakubali kuwa kamati ya ZITTO KABWE imewadanganya watanzania. Muhongo ambaye amejibu hoja moja baada ya nyingine kwa kutoa ushahidi wa viambatanisho muhimu amedhihirishia bunge kuwa kamati ya bunge imetoa taarifa ya uongo. 

Katika majibu yake, profesa Muhongo amedhihirisha kwa ushahidi kuwa pesa za ESCROW hazikua za serikali. Pesa hizo ni za IPTL na kwamba serikali bado inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 94 na IPTL kama malipo ya kufua umeme. 
Aidha, Muhongo amemlipua mwanasheria Mkono ambaye aliingia mkataba na TANESCO wa kuwa mwanasheria wao na alidai na kulipwa kiasi cha bilioni 62 (robo ya pesa za ESCROW) kama malipo ya uanasheria. Mkataba huu ulivunjwa na TANESCO chini ya uongozi wa waziri Muhongo. 

Majibu haya ya Muhongo yameivua nguo kamati ya PAC na kuzua maswali mengi yasiyo na majibu. 
Kwanini PAC ilidanganya bunge? 
Kwanini PAC haikuonesha vielelezo hivyo? 
Nani yako nyuma ya PAC? 
Kwanini PAC haikutaja ufisadi huu wa Mkono? 
Taarifa kuwa wasaka Urais wa CCM ndio waliopika uongo huu tuziamini? 

Kwa muda sasa tangu sakata hili lianze, yako majina ya watu ambayo yamekua yakitajwa kuwa wana maslahi yao binafsi na sakata hili la escrow.
Hawa ni wafuatao:-

REGINALD MENGI:
Huyu alikua anatajwa kutaka kulipa kisasi cha ugomvi wake na Muhongo na Maswi kufuatia kunyimwa vitalu vya gesi na kutajwa na Muhongo kuwa ni dalali na si mfanyabiashara. Taarifa ya PAC imelitumia neno dalali sana, lakini si kwa Mengi safari hii. Bali kwa Prof Muhongo. Hatujui kama ndio kisasi cha Mengi au la. 

NIMROD MKONO:
Huyu ni mwanasheria maarufu ambaye aliingia mkataba wa kuwa mwanasheria wa TANESCO ambao ulivunjwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi . Mkono hadi mkataba ulivunjwa alikua ameigharimu TANESCO kiasi cha bilioni 62, sawa na robo ya pesa za ESCROW. Akiwa nchini Uingereza Mkono alizusha uvumi wa kulishwa sumu, lakini mjumbe mwenzie wa kamati Halima Mdee alitilia shaka taarifa hiyo kwakuwa alikua na Mkono Uingereza. 
EDWARD LOWASSA :
Hawa walitajwa kuwa na mipango kwa wakati tofauti ya kumchafua waziri mkuu Pinda kila mmoja akilenga kupendekeza njia ya Urais. Lowassa anatajwa kumuona Membe kuwa si tishio (threat) tena katika mbio zake za u Rais. Badala yake anamtazama Pinda kama kikwako kikuu au mshindani mkuu kwa sasa. Lowassa anatajwa kutumia karata ya ESCROW ili kummaliza Pinda kisiasa kwa kumbana ajiuzulu. Katika kufanikisha haya, mpambe wa Lowassa ambaye pia ni mbunge Peter Serukamba anatajwa kusimamia bungeni mara kadhaa kutaka kamati teule iundwe kuchunguza sakata hili, kama karata ya kummaliza Pinda. Aidha Lowassa anatajwa kuwashawishi wabunge wa upinzani kwa mlungula ili waishabikie hoja hiyo. 

BERNARD MEMBE
Waziri huyu wa mambo ya nje yeye anaamini kuwa hadi miezi mitatu iliyopita kabla ya ujio wa Pinda kwenye mbio za urais, mpinzani wake mkubwa alikua mbunge wa Monduli na waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa. Membe alibweteka akiamini kuwa Lowassa jina lake litakatwa na kamati kuu na lake kupita . Lakini baada ya ujio wa Pinda kwenye mchakato wa Urais, Membe alitikiswa sana. Akafikia hatua ya kulalamika kwenye magazeti juu ya harakati za Pinda. Alijua kuwa hesabu zake zimevurugika. Utafiti wa TWAWEZA ukamuumiza zaidi pale ulipoonesha kuwa Mizengo Pinda ndiye anayemfuatia Lowassa kwa karibu, huku Membe akizidiwa na Lipumba na Dr Slaa. Kama kawaida yake akalalamika kwenye vyombo vya habari. Karata pekee ambayo Membe aliiona ni kutumia ESCROW kummaliza Pinda na ikiwezekana kuiangusha serikali kwa maana ya baraza zima la mawaziri. Membe anaamini (sijui kama ni kweli) kuwa Jakaya anamtaka awe Rais baada yake. Hivyo kwa vyovyote angerudi kwenye nafasi yake. Katika kufanikisha hili, Membe anatajwa kuwatumia wabunge wa Upinzani kwa kuwashawishi na kuwahonga pesa kuipitia yeye Membe na wapambe wake. Wabunge hao walichukua pesa lakini walivujisha siri. Membe pia anadaiwa kuvujisha siri za sakata la ESCROW na kupika uongo kwa kupitia waandishi wa habari. Hapa anatajwa mwandishi wa gazeti moja la kiingereza (jina tunahifadhi) la hapa nchini. Pia Membe anatajwa kuwatumia marafiki zake wengine walioko ndani ya vyama vya Upinzani kuvujisha siri za vikao vya mienendo ya kujadili ESCROW. Baadhi yao ni vijana waliokuwa wanarusha mtandaoni habari hizo moja kwa moja wakati vikao vya CAUCUS YA CCM vikiendelea. Mmoja wa wapambe hawa anaeshukiwa ni Yeriko Nyerere ambae ni member mzuri wa jamii forums (rejea post za Yeriko Nyerere). 

Wananchi tulipuuza tukajua huu ni uongo, lakini leo hii baada ya majibu ya Muhongo tunashawishika kuamini kuwa ESCROW imetengenezwa na wachache kwa maslahi ya wachache huku wengi tukitumiwa kama daraja. Prof Muhongo kawaumbua PAC
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment