Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC Dodoma 1995
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995
On Saturday, November 15, 2014 1:54:04 PM UTC+3, tugutunm wrote:
Jamani sikilizeni kijana huyo anavyoongea...!
Nzweke Mussa Tugutu (Mr)
Cooler Executive Lake Zone
Nyanza Bottling Co Ltd
Nyakato Industrial Area
P.O. BOX 2086
Mwanza, Tanzania ( EA)
Mobile:+255784894535,+255754894535. On Nov 15, 2014 11:03 AM, "Fatima Husenali" <huse...@gmail.com> wrote:---Aliwahi kufukuzwa na baba yake kwa wizi wa ng'ombe wa familia ndipo akaamua kukimbilia kwenye siasa
Alikula hela aliyopewa na Mwl Nyerere kwa ajili ya kujengea ofisi ya ccm Arusha
Alifanya ufisadi mkubwa kipindi akiwa mkurugenzi wa AICC Arusha
Kaliingizia taifa hasara kubwa baada ya kuingia mkataba wa kifisadi na Richmond ambao mpaka leo unawagharimu Watanzania kwa kupanda kwa bei ya umeme.
Haitoshi kaona autafute urais kwa gharama yoyote ile, alianza kuhonga viongozi wa nec wa ccm, akaja kwa viongozi wa dini, akaendelea kwa baadhi ya mbumbumbu wa vyuo vikuu wasio jitambua, na sasa yupo kwenye vyombo vya habari na baadhi ya taasisi binafsi kama TW.....EZA.
Mbaya zaidi Kuna wapuuzi wanaojinasibu kama wasomi wamekuwa wakijaribu kumsafisha kama mtu safi kwa kisingizio eti ana maamuzi magumu lakini hawatuambii hayo maamuzi magumu yamelisaidia taifa kiasi gani zaidi ya kulitia hasara tu,
wengine wanasema deal ya richmond alitumwa na wakubwa kuifanya lakini swali la kujiuliza kama anaweza kutumwa kutekeleza uhalifu dhidi ya taifa lake na akakubali hivi tukimpa uraisi wa nchi yetu atashindwa kuliweka rehani taifa letu kwa mabepari kama anavyofanya jk?Huyu fisadi kalima ya wizi ipo kwenye damu tangu akiwa ndani ya familia yake hivi akipata urais ni kweli utakuwà mwisho wa hiyo tabia mbaya?
Na atawezaje kukomesha wizi wa mali ya umma wakati yeye mwenyewe ni mwizi aliyekubuhu?ikulu kuna deal gani mpaka akukimbilie kwa kutumia fedha nyingi sana na hizo fedha atazirudisha vipi?
Kuna wapuuzi wengine wanasema kwa sababu ana fedha basi apewe urais kwa kuwa hawezi kuiba tena, bila shaka huo ni uvivu wa kufikiri maana siku zote mwenye fedha hutaka kuwa na fedha zaidi ya zile alizonazo na ni wazi kwa hiyo hoja yao inaonesha ni jinsi gani wasivyoelewa hulka ya watu matajiri, na zaidi ya yote huyu mtu wizi upo kwenye damu kutokana na historia yake ilivyo.Nihitimishe kwa kuwaomba Watanzania tusijaribu kufanya makosa kumpa fisi atuchungie mbuzi wetu maana ipo siku tutajuta pale tutakapoona mbuzi wetu wameliwa wote.
On Thursday, September 18, 2014 10:56:23 PM UTC+3, Juma Mzuri wrote:KATIKA makala mbili nilizoandika na kuchapishwa katika gazeti hili wiki mbili zilizopita, nilijaribu kuanisha sifa za kihaiba na kikazi za mwananchi anayefaa kuwa Rais wetu wa tano.
Nashukuru kwa mrejesho niliopokea kutoka kwa wasomaji wengi na walionitia shime niendelee na makala hizi. Nawashukuru pia waandishi wenzangu wa makala, akiwemo mwandishi mahiri na mkongwe, Johnson Mbwambo, kwa kurejea maudhui ya makala yangu katika andiko lake lililochapishwa katika gazeti hili toleo Na. 370 la Septemba 10-16, 2014.
Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na hofu aliyoonyesha juu ya uwezekano wa wagombea kukidhi sifa nilizozianisha, pamoja na hitimisho lake kwamba wagombea waliokwishajitokeza hadi sasa wana ombwe kubwa la kifalsafa.
Nilisitisha kwa muda makala hizi kutokana na uzito wa maoni niliyopokea kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi waliojijengea heshima kubwa katika nchi yetu. Wengi wa waliotoa maoni walienda mbali na kunishauri niandike kitabu kuhusu wasifu wa wagombea.
Wengine waligutuka nilipohitimisha makala yangu kwa ahadi ya kuanza kuwajadili wagombea mmoja baada ya mwingine, wakidhani kwamba nitakuwa nakwenda mbali mno! Aidha, wapambe wa wagombea nao wamekuwa na wasiwasi kwamba nitawabeba baadhi ya wagombea na kuwaharibia wagombea wao.
Baadhi ya wasomaji na wapambe wa wagombea wamenishauri kwamba niache kuwajadili wagombea na niwaachie wananchi waamue wenyewe. Nimekataa ushauri wao huu wa kuwachia wananchi waamue wenyewe, na hivyo naendelea na uchambuzi wangu wa wagombea wote waliojitokeza na watakaojitokeza.
Nimeamua kujitwika jukumu hili hatarishi kama sehemu ya wajibu wangu wa kijamii katika kuchangia kuiepusha nchi kupata kiongozi atakayetushtukiza bila kumjua sawasawa kabla hajaingia madarakani. Ukimwacha Mwalimu Nyerere, marais wetu waliopita na aliyepo walitushtukiza.
Hatukumjua vizuri Mzee Mwinyi kabla hajawa Rais, na vivyo hivyo kwa Mzee Mkapa. Wote hawa walipatikana kwa mtindo unaofanana: waliibuliwa bila kujitutumua wao wenyewe kuutaka urais kwa udi na uvumba kama ilivyo kwa wagombea wa leo.
Mzee Mwinyi aliibuliwa na Kamati Kuu ya CCM, wakati Mzee Mkapa aliibuliwa na Mwalimu Nyerere pasipo kutarajiwa. Bahati nzuri waliibuliwa katika mtindo usiotia shaka sana kwa sababu ni uzao wa taasisi za kueleweka kwa wakti ule, ambazo ni Mwalimu mwenyewe na Kamati Kuu ya CCM ya wakati huo ambayo isingekuwa rahisi kuitilia shaka katika maamuzi yake.
Pengine tulimjua kidogo Rais Kikwete kabla ya kuingia madarakani kwa sababu alijinadi vya kutosha kabla hajaingia ikulu mwaka 2005. Jina la Rais Kikwete lilianza kuwika kwa upana wake kwa mara ya kwanza mwaka 1995 alipochukua na kurudisha fomu ya kugombea urais kwa mbwembwe, sambamba na swahiba wake mkuu wa wakati huo, Ndugu Edward Lowasa.
Tangu wakati huo tuliendelea kumwagiwa sifa kemkem juu ya Rais Kikwete hadi anaingia madarakani mwaka 2005. Kwa hiyo, hatukujua upande wa pili wa Rais Kikwete kwa maana ya udhaifu wake kihaiba na kiutendaji kabla hajaingia madarakani. Ndiyo kusema naye kwa kiasi fulani alitushtukiza.
Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna utamaduni wa kuwadodosa vya kutosha watu wanaotaka kuwa viongozi wetu. Maandishi mengi kuwahusu wagombea huandikwa wakati wa kampeni yakilenga kuwasifu wagombea fulani na 'kuwakandia' wagombea wengine. Hatupati uchambuzi unaotuwezesha kuwajua wagombea wote kwa ukamilifu wake katika kutusaidia kufanya maamuzi ya maana. Hili ndilo ombwe la ufahamu ambalo najaribu kuliziba katika mfululizo wa makala zangu.
Katika uchambuzi wangu nitajitahidi kuwa mkweli na kuzingatia maadili na weledi wa kitaaluma ili kuepuka kupendelea au kuonea. Hata hivyo, kama yalivyo maandishi yote katika sayansi ya jamii, sitarajii kwamba makala hizi hazitaibua hisia kali, shutuma, lawama na hata vitisho kutoka kwa miongoni mwa wapambe wa wagombea ambao wamejiaminisha kwamba wagombea wao ndio hasa wanaofaa kuongoza nchi hii na hakuna mwingine.
Niwatahadharishe wasomaji na hasa wapambe wa wagombea kwamba ninachokiandika hapa ni wasifu wa wagombea, kwa maana ya "biography" na sio wasifu kwa maana ya "hagiography". Katika kuandika hagiography, mwandishi hujikita katika kuanisha mazuri ya mtu anayemwandika huku akifumbia macho udhaifu au upungufu wake.
Katika kuandika biography mwandishi hujikita katika kuanisha pande mbili za mhusika ikiwa ni mazuri na mapungufu yake. Kimsingi hagiography huandikwa kwa ajili ya kuwatukuza na kuwasifu 'watakatifu' wanaoishi. Bahati mbaya au nzuri hatuna hata mtakatifu mmoja kati ya wagombea wetu.
Hivyo, tutachambua nguvu na mazuri yao kwa upande mmoja, na madhaifu na mapungufu yao kwa upande mwingine. Ni matumaini yangu kwamba uchambuzi huu utawasaidia wagombea na wapambe wao katika kujiimarisha kwa kukazia nguvu na mazuri yao na kuchukua hatua stahiki katika kurekebisha au kujiandaa kujibu mapigo kuhusu madhaifu na mapungufu yatakayojitokeza katika makala hizi.
Tunaanza na Ndugu Edward Ngoyai Lowasa. Huyu alipata kuwa Waziri Mkuu katika Awamu ya Kwanza ya utawala wa Rais Kikwete aliyedumu kwa takribani miaka mitatu kutoka 2005 hadi 2008.
Ndugu Lowasa ndiye mwanasiasa pekee mwenye uwezekano wa kugombea tena urais kati ya wanachama 17 wa CCM waliojitokeza kugombea urais mwaka 1995. Wengine waliobaki ama wamefariki dunia (wakiwemo Horace Kolimba, Tuntemeke Sanga, Kighoma Malima), au wamezeeka na kuishiwa nguvu za kukabiliana na mikiki ya kisiasa (wakiwemo John Malecela, Cleopa Msuya, Pius Msekwa, Joseph Warioba), au 'wamepotea' katika ulingo wa siasa (wakiwemo Rose Lugembe, Solomon Ole Saibul, Aggrey Mwasagah, Omari Mwariko na Balozi Frederick Rutakyamirwa).
Wana CCM wawili kati ya wale waliojitokeza mwaka 1995 walifanikiwa kuukwaa urais katika vipindi tofauti, ambao ni Mzee Benjamin Mkapa (1995-2005) na Rais Jakaya Kikwete (2005-2015). Jaji Mark Bomani aliyegombea pia mwaka 1995 naye bado yumo katika ulingo wa siasa lakini hajaweka wazi kama atagombea au la hadi ninapoandika makala haya, lakini kuna watu kadhaa wanamtajataja.
Edward Lowasa alijitokeza mwaka 1995 akiwa na mika 42 tu mbele kidogo ya January Makamba (miaka 40), ambaye naye amejitokeza kugombea akitembelea kete ya ujana.
Aidha, pamoja na kwamba hajawahi kutangaza rasmi na moja kwa moja, Lowasa ni mwanasiasa ambaye anatajwa kwa uhakika zaidi kwamba anautaka urais 2015, na pengine amejiandaa zaidi kisaikolojia kuwa Rais kuliko mgombea mwingine. Kwa hivyo, Lowasa ni moja ya wagombea wenye nguvu za kisiasa za kuweza kushinda uteuzi ndani ya CCM na pengine kushinda kiti cha urais.
Kikazi, Ndugu Edward Ngoyai Ngoyai Lowasa ni mwanasiasa ambaye tunaweza kumuelezea kama kiongozi anayebebwa na taswira chanya ya uchapa kazi katika sehemu mbalimbali alizofanya kazi, ikiwemo alipokuwa Waziri Mkuu. Kihaiba, Ndugu Lowasa anazungukwa na taswira hasi katika eneo la uadilifu, kutokana na kuhusishwa na tuhuma na hisia nyingi kuhusu rushwa na ufisadi hapa nchini.
Pengine, hiki ndicho kitakuwa kikwazo kikubwa zaidi katika mbio zake za urais kwa sababu uadilifu itakuwa moja ya agenda kubwa katika kampeni za 2015. Akifanikiwa kupenya uteuzi wa CCM atakuwa na kazi ya kutosha kujibu maswali mengi kuhusu tuhuma za ufisadi. Tutachambua taswira hizi pamoja na sifa zingine za Ndugu Lowasa katika makala ijayo.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/edward-ngoyai-lowassa-mchapa- kazi-mwenye-nakisi-ya-uadilifu -na-falsafa#sthash.ZHS89mtA. dpuf
On Sunday, September 14, 2014 9:06:23 AM UTC+3, Method Francis Ngonge wrote:MollelKama ni uliowataja ni wanafiki basi na Lowassa ni mnafiki maana yuko na hao wanafiki kwenye kundi moja la CCM na ndiyo maana anataka urais kupitia chama hicho hicho kilichojaa wanafiki ili akauendeleze unafiki na mabaya yote wayajuayo hao wanafiki wote2014-09-14 7:34 GMT+03:00 Hosea Ndaki <hosea...@gmail.com>:pale angekomaa nao tu wakatoka wote, siunaona pinda katoa machozi
lakini anao tu, sasa hivi tungekuwa tumepiga hatua kubwa ya maendeleo.
> Chama cha Mapinduzi.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru"..
On 9/14/14, 'lesian mollel' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com> wrote:
> ni hotuba ya mtu jasiri who see far, majungu tu ndio yalomchomoa mh si siri,
> wale walopewa kamata wote wamepewa zawadi.....hizo ni siasa chafu tu sote
> tunajua
> Ila tumejipANGA vilivyo ataingia ikulu kwa kua watanzania washagundua janja
> ya nyama......ENL is innocent,,,,wanamtaka aiingie ikulu mara mora aendeshe
> jahazi hili linaloyumba awweeeke sawa
>
>
>
> On Saturday, September 13, 2014 8:10 AM, Emma Kaaya <emma...@gmail.com>
> wrote:
>
>
>
> HEBU TUCHAMBUE MAUDHUI YA HOTUBA ILIYOTOLEWA NA Waziri mkuu mstaafishwa Mhe
> Edward Ngoyayi Lowasa (MB) Wakati wa kujiuzuru kwake......
> "Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa
> kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.
> Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati
> Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe
> zilikuwa nzuri kweli.
> Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka
> kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.
> Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha
> Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".
> Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice.
> Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita
> minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini
> mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
> Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka
> ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na
> nilikuwa tayari kufanya hivyo.
> Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite
> kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu
> ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema
> uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano
> kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond
> ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.
> Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo
> mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama
> katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri.
> Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo
> ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa
> kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa
> sana katika hili.
> Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi
> sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya
> mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini
> minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume
> imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na
> wanamsema kwa kirefu sana.
> Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi
> wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata
> moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali
> kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya
> Waziri Mkuu hakuna hata moja.
> Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema
> tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa
> hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na
> kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea
> kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?
> Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza
> hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima
> zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi
> nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani
> tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya,
> tumuondolee heshima au tumwajibishe.
> Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya
> Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.
> Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji
> lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa
> kumsingizia mtu.
> Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima
> aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.
> Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.
> Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru
> Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya
>
> On Tuesday, September 2, 2014 7:44:31 PM UTC+3, Fred Hans Kipamila wrote:
> Huyu ni Edo yupi? Edo Kumwembe au yupi?
>>------------------------------ --------------
>>On Tue, 9/2/14, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>
>> wrote:
>>
>> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 : Edward Ngoyai Lowassa
>> To: "'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii" <wana...@googlegroups.com>
>> Date: Tuesday, September 2, 2014, 7:41 PM
>>
>> Kuna siku nilisoma gazeti fulani
>> lililokuwa likizungumzia eti Ridhi One Kikwete amnyambua
>> Edo....likaendelea kunena eti asema ni mzee na
>> hafai....aisee nilisikitika sana kuwa hivi huyu kijana ni
>> kweli hajui ni kwa jinsi gani edo ameibeba serikali hii hata
>> iwepo amani na mustakabali mwema wa nchi? Nikajitia moyo kwa
>> kumsamehe lkn nikamuomba nikisema baba,ikulu hii
>> isituchagulie rais,tupe raisi sawasawa na mapenzi yako..
>> MUNGU YUPO
>>
>> 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>
>> wrote:
>>
>> >Mbunge wa Monduli tangu afe kipenzi cha watanzania
>> Edward Moringe Sokoine, nadhani ndiyo sababu anafaa kuwa
>> rais ajaye
>> >---------------------------- ----------------
>> >On Tue, 9/2/14, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>
>> wrote:
>> >
>> > Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 : Edward Ngoyai
>> Lowassa
>> > To: "'tumaini bakobi' via Wanabidii" <wana...@googlegroups.com>
>> > Date: Tuesday, September 2, 2014, 1:00 PM
>> >
>> > Tatizo la watz ni kuongea tu bila
>> > hata wakati mwingine kufikiri kwa kina....unaambiwa tz
>> ni
>> > moja ya nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi
>> > duniasi...hivyo hatujasimama,twasonga mbele...Lowasa
>> ni
>> > mmoja ya waliochangia mafanikio ya nchi kwa sehemu
>> > kubwa...na kwa sababu hiyo ndio maana anastahili
>> kupewa
>> > dhamana kubwa ya uongozi...mchango wake haujifichi kwa
>> > nyanja zote mpk kwenye nyumba ya ibada
>> unayoingia,radio
>> > unayosikiliza,maji unayokunywa,nk...ngupula
>> >
>> > 'tumaini bakobi' via Wanabidii
>> > <wana...@googlegroups.com>
>> wrote:
>> >
>> > Muda na nafasi
>> > alizoshika serikali kama akusaidia kuleta maendeleo
>> basi
>> > hataweza tena hata kama akiwa rais. Nadahani anatakiwa
>> > kung'atuka tu awaachie wengine hatakuwa na
>> > jipya.
>> >
>> > On Tuesday, 2 September 2014,
>> 12:18,
>> > 'lesian mollel' via Wanabidii
>> > <wana...@googlegroups.com>
>> wrote:
>> >
>> >
>> > magesa malizia kwa kusema anafaaa kua Rais
>> > 2015
>> >
>> >
>> > On Saturday, August 30, 2014 12:26
>> > PM, Boniface Magessa <mage...@gmail.com>
>> wrote:
>> >
>> >
>> > Mbunge wa Monduli tangu lini??imekaa
>> > sawa hii?
>> > On 30 Aug 2014 22:22,
>> > "Emma Kaaya" <emma...@gmail.com>
>> > wrote:
>> >
>> > Edward
>> > Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26
>> > Agosti 1953) ni
>> > mwanasiasa nchini Tanzania.
>> > Alichaguliwa kuwa Waziri
>> > Mkuu wa kumi wa nchi hii tarehe 30
>> > Desemba 2005 na
>> > akalazimishwa kujiuzulu tarehe 7
>> > Februari 2008 kwa
>> > kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi wa ufisadi
>> > katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond
>> kama
>> > mhusika mkuu.
>> > Lowassa ni
>> > mwenyeji na mbunge wa Monduli katika Mkoa wa
>> > Arusha. Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya
>> > tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha wanabidii+...@ googlegroups.com.
>> >
>> > For more options, visit
>> https://groups.google.com/d/ optout.
>> >
>> >
>> >--
>> >Send Emails to wana...@googlegroups.com
>> >
>> >Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> >wanabidii+...@ googlegroups.com
>> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>> >
>> >Disclaimer:
>> >Everyone posting to this Forum bears the sole
>> responsibility for any legal consequences of his or her
>> postings, and hence statements and facts must be presented
>> responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
>> and Guidelines.
>> >---
>> >You received this message because you are subscribed to
>> the Google Groups "Wanabidii" group.
>> >To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>> from it, send an email to wanabidii+...@ googlegroups.com.
>> >For more options, visit
>> https://groups.google.com/d/ optout.
>>
>> --
>> Send Emails to wana...@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+...@ googlegroups.com
>> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>> for any legal consequences of his or her postings, and hence
>> statements and facts must be presented responsibly. Your
>> continued membership signifies that you agree to this
>> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the
>> Google Groups "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>> from it, send an email to wanabidii+...@ googlegroups.com.
>> For more options, visit
>> https://groups.google.com/d/ optout.
>>
> --
> Send Emails to wana...@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+...@googlegroups.comUtapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+...@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
>
> --
> Send Emails to wana...@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+...@googlegroups.comUtapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+...@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
>
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.comUtapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment