Wednesday 19 June 2013

[wanabidii] Vurugu za Jijiji Arusha-Zilikua lazima!!

Wadau jama nilikua jijini Arusha kikazi na wakati wa mchana kuelekea jioni nililzimika kurudi mahali milipofikia kwa ajili ya kuchukua document fulani. Kwa kuwa ilikua mjini nilijikuta katikati ya makundi yanayopingana, Upande mmoja polisi wakiwa wanarusha mabomu ya machozi kila mahali na makundi ya wananchi wakirusha mawe ovyo hususan wakiwalenga polisi.Ilifika mahali dereva wa taxi alikosa njia ya kupita maana mawe yalipangwa njiani kuzuia defenda za polisi.
Kwa kweli kwa mara ya kwanza nilihisi naweza kupoteza maisha. Namshukuru Mungu dereva yule anafahamika so tuliweza kupenya hadi tukafika salama na kurudi japo machozi yalinitoka pamoja na kufunga vioo vya gari.
Mimi najiuliza: Je zile vurugu zilikuwa na ulazima wowote? Ina maana wahusika hawawezi kutafuta njia muafaka ya kila mmoja kufikia malengo yake (yaani polisi kudumisha ulinzi na raia kuandamana kwa amani)
Is it really worthwhile kufanya yale waliyofanya? Huku ndiko tunakoipeleka nchi yetu? Nahisi bado tunazo busara za kuweza kuishi kwa kuvumiliana na kuishi kwa amani because we are very diverse but united.
Naomba wadau wote tupiganie amani despite our differences of opinion. Natamani ningekua na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa mkoa wa Arusha na wanasiasa niwashauri wajaribu amani kabla ya kupigana
Kwa kweli hali ilinitisha sana sana

--
Victor Caleb Mwita
Ministry of Livestock and Fisheries Development
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam
Tel: 0766750673, 0789142275

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment