Friday 28 June 2013

[wanabidii] FIKRA BUTU!

Ni heri tuendelee kumea
kama fikra pevu kuliko
kukubali kudhoofishwa
na wenye fikra dhaifu.
Nape Nnauye ni bora
ukae kimya watu
wakudhanie ni mjinga
kuliko ukisema halafu
ukathibitisha kuwa
kweli wewe ni mjinga!
WanaChadema warushe bomu
kwenye mkutano wao
wa kampeni
kuwaogopesha ,kuwajeruhi
na kuwauwa watu wake
wale wale
wanaoombwa kura, ni
kauli inayoweza
kukubaliwa na mazuzu
wenzako lakini si kwa
wapembuzi wa mambo. Ni
dhihaka za kitoto.
Kama ulijua njama hizo
za Chadema kwa nini
hukuiarifu polisi?
Kama hukuiarifu kwa
nini hukuombwa kupeleka
ushahidi?
Tunajua wanaogopa
kukukamata kwani
taarifa zako zingeweza
kuepusha maafa
yaliyotokea.
Kwa kauli yako, pamoja
na ya Lukuvi, ni wazi
kuwa mna ufinyu wa
akili kwani Lukuvi
anapodai kuwa polisi
walikuwa wanajihami je,
wananchi walikuwa
wana silaha gani
zilizowalazimu askari
kutumia risasi za moto
dhidi yao?
Kama askari walikuwa
wakijitetea
inawezekanaje wajitetee
dhidi ya raia wasio na
silaha?
Kulikuwa na haja gani
ya kutumia risasi za
moto badala ya risasi za
mpira (rubber bullets)?
Serikali ilitoa tamko
kuwa milipuko ya
kanisani na ile ya Chadema
inafanana mbona safari
hii hamkuwaita FBI kama
mlivyofanya mara ya
kwanza?
Huyu ndiye Nape Nnauye,
katibu mwenezi ambaye
ametumwa na chama
chake kutoa tamko hilo.
Leo Nape anaposema ni
chadema waliohusika
wapo wanaohoji na lile
la kanisani je nayo ni
Chadema?
Kiongozi asiyejua la
kusema mbele ya umma na
nyuma ya pazia lazima
ima awe ameishiwa au
amekuwa kiongozi kwa
bahati mbaya.
 

0 comments:

Post a Comment