Friday 28 June 2013

Re: [wanabidii] TAFAKARII

Kwa visingizio watanzania ndio wenyewe. Lakini anayeuza nyumba ya vyumba 6 Magomeni, Kariakoo, Ilala Boma yanajengwa maghorofa kisha anahamia kigogo bondeni au Ilala Mchikichini-Baghdad; Jangwani Sunna kutoka hapo magomeni mapipa alikouza ni Kigogo au mmiliki wa hiyo nyumba aliyouziwa na NHC kwa 60,000/= enzi hizo sasa ameuza kwa 1 billion? haendi Mkuranga-yupo mjini hata kama atalala njaa.

Kijiji cha mwenge kijiji cha nyumba za aina moja cha Mfano cha Mzee Nyerere pamoja na huduma zote kuwepo na maeneo mabubwa kwa nyumba-anayeweka viosk mbanano nan kuuza kukalimbikizwa majengo mbanano ni Nape Mnauwe au mmiliki binafsi ambaye mbele ya nyumba kakodisha ujenzi wa bar na garage? Surveyed and Planned area za Tangi Bovu, tegeta Sites and Services, za namna hiyo Sinza, Mbagala, Kiwalani-ni low income areas-muuzaji na mbananishaji-politician? Nyumba za NHC zenye nafasi na maeneo ya huduma-wameuziwa wapangaji. Kaangalie kilichofanyika nyuma ya ghorofa za NHC hapo ubungo nyuma ya maghorofa na NBC. Hainiingii akilini mtu unavamia na kujenga eneo la Tanz ania Zambia Road Services au unajenga vingunguti ktk bwawa la kinyesi hadi relini baada ya kuuza eneo lako kukajengwa jumba la fahari.

Wafanyabiashara mfano wa Soko la Mwenge au maduka yale ya vinyago mwenge kunakofika watalii-wanaweza wakaunda kampuni ndogo au ushirika wakalimbikiza hela miaka 3-5 hivi kisha kupata mkopo wakajenga ghorofa kubwa soko la kisasa kama kariakoo wakauza vizuri kuliko sasa. Wakakodisha wenye hotel hapo ghorofa za juu. Wale wa vinyago wakauza vyakula vya asili hapo kwenye vinyago. Ukiingia soko la Buguruni lipo wazi ndani, maji, matope, uchafu kibao nao wapo hapo kila mtu na uchafu wake. Kuna management ya soko lakini rushwa mpaka ndani ya chupi zetu.

Ni hivyo soko w za Mabibo (la vyakula kawaida na ola ndizi yapo maeneo tofauti jirani ukielekea TGNP. Ila wapo barabarani. Nenda Tandale au Tegeta-hatukai sokoni bali barabarani. Makumbusho jee soko nadhifu na zile nyumba za NHC wameuziwa waliopanga. Soko jengo poa-hatukai tupo mwenge barabara ya magari. Hii nayo? Tutembelee tuone uhalisia. Kuna kitu fulani ndani ya tabia zetu kinachotufanya tukatae ukweli na kujikanya, kujituma kiusafi na kuzingatia sheria.
 
Tingatinga liingie iwe pa mbunge, waziri au GVT kama imejenga pale pasipo ruhusiwa.  Ifike wakati kuwa GVT imshitaki yule afisa/maafisa wa kwanza (wakaguzi) aliye/waliofanya ukaguzi na kutoa taarifa au kupitisha kuwa panafaa kujengwa. Afisa wa juu anaweza kuweka sahihi kwa kudanganywa na wakaguzi wa mwanzo. Ikijulikana alishinikiza-ile kwake pia. Inatoka ktk TV kuwa mtu kauza uwanja wa wazi lakini Municipal Council haikuhusika kuutoa. hakuna kesi hapo ni kubomoa. Hati na vibali feki. Wapo watu wanafomu za bank na mihuri feki pia ya wizara halafu kesi inachukua miaka mingi na mawakili kuhusika kuwatetea. Huyo mwenye jengo anaweka mawakili ambao nao wanakuwa na utetezi usio halali kwani mtu huyo aliyejenga hapo anakata rufaa na wanamtetea. Kama sheria ni msumeno na unataka ifanyike kihaki- wakili wa kukutetea unamweka why na umekosa na jengo linaonekana na kila mtu nje ya ramani ya ruksa? wakili unatetea why? Hao nao wateteao uovu ili mradi mkono uende tumboni wafwanyeje? Ndio hapo tunajiua wenyewe.

NEMC na wapangaji mipango miji waone overload inayotiwa mfumo majitaka, uzoaji taka ngumu na Tanesco, Dawasa waone overload ktk maji na umeme. Serikali imeuza nyumba  zake Upanga, Victoria, Masaki, Msasani, St peter's, Oysterbay etc ambayo yana uwazi mkubwa ikijenga 40% ya plot huko nyuma na kuacha 60% ya huduma nyingine yakizingatia sheria zake. waliouziwa-wamejenga 100% maghorofa wanapangisha kwa $; restaurants, bar au ghorofa ya shule waitazo academic. Haya yanaongeza mahitaji ya maji, umeme, majitaka, solid waste na utata moto ukiwaka.
Wawabomolee hawa wamekiuka sheria na kuzipa mzigo mamlaka mbali mbali katika huduma. nani amfunge paka kengele na watu wanaamua kujenga bila vibali maana ploy tayari inahati. wajenzi wa TZ-wakandarasi sheria za ujenzi za TZ na international si wanasoma shule. Mbona wanachakachua na wanafanya isivyo. hata ambao maghorofa wameambiwa wabomoe hawajabomoa na soon yataua. gharama ya kubomoa itoe serikali? Na likianguka likiua? hata pamoja na kuwepo na hatari hii, utakuta mtu kapanga biashara au kapaki magari hapo penye hatari.

Ni mengi ya kujadili nchi hii mambo maovu tufanyao wenyewe na kesi mahakamani huchukua miaka kutokana na kuweka mawakili wa kisheria kuzuia ubomoaji hata kama ni mali ya mkuu au mlokole na kanisa lake. Upande wa pili-kuna  wanaotangaza ktk print media-dawa ya kushinda kesi mahakamani; ya kupasi mtihani hata kama umefeli. Yaani utashinda kesi hata kama umekosea, umeua etc.
Bongoland kiboko ya utetesi wa ujinga.
 
From: Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 28 June 2013, 23:04
Subject: Re: [wanabidii] TAFAKARII

SIUNGI MKONO HOJA KWA 100%

Pamoja na hayo yote, serikali inapaswa kuwatengea raia maeneo ya kufanyia biashara. Isiwe kwamba maeneo ya biashara yananyakuliwa na mafisadi halafu mnataka kuwatimua hao masikini. Wakafanyie wapi biashara zao? Maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya masoko yamechukuliwa na mafisadi na wamejenga mighorofa, tena kwa kiwango cha chini, na kusababisha hatari ya kuwadondokea raia. Raia hawapaswi kulaumiwa katika hili wala kuhamishwa. Waende wapi wakati nao wana njaa kama wengine?

Acheni uonevu kwa wanyonge. Kama ni kuvunja sheria, basi hizo sheria zinavunjwa na mahakama za kifisadi kwa kushindwa kuwafunga mafisadi au kwa kuwafunga vifungo laini. Mbona hatujawahi kusikia mafisadi wakiwajibishwa kwa kuuza maeneo ya kufanyia biashara? Kuna mbunge mmoja wa chama tawala kajenga hekalu karibu na mto na kuzuia maji kupita lakini NEMC wameshindwa kumbomolea--kisa kakimbilia kwenye mahakama za kifisadi! Ina maana hizo sheria zinapaswa kufuatwa na masikini tu? Ni sheria gani hizo zinazokata upande mmoja kama panga?

Kama sheria ni msumenp basi ilipaswa kukata hadi kwa mafisadi sio kukata kwa raia tu. Serikali inapaswa kualaumiwa kwa kuuza maeneo ya masoko kwa mafisadi. Lazima tukubaliane kwamba hili ni tatizo la kimfumo na linarutubiswa na SERIKALI dhaifu tuliyo nayo. Hivyo basi, dawa si kuwabomolea na kuwaharibia watu biashara zao bali ni kuufumua mfumo mzima wa serikali hii ya kifisadi. Naomba kutoa hoja.

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, June 28, 2013 10:28 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAFAKARII

Bwana Alexanda
asante sana kwa tahadhari hii. Ni kweli watanzania tumeathirika kuunga mkono au kupinga mambo ya maendeleo. Tuna hitaji miji na majiji yenye mpango na yaliyo safi. Ukitembelewa kwa wenzetu usafi unawezekana kirahisi kwa sababu ya mpango mji ulivyo.

Moto umekuwa ni janga la Taifa kwa Tanzania. Kwa umakini huduma ya zima moto haifikii jamii muda muafaka sababu ya miundombingu yetu mibovu. Kila mtu anajenga na kufanya biashara apendavyo.

Tukubali ni lazima miji na majiji yetu yawe na mpango. Ukiambiwa umejenga eneo la barabara, au karibu na nguzo ya umeme au karibu na kiwanda kinachomwaga sumu, au kwenye mkondo wa maji; tii amri ya kuondoka eneo hilo.

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, June 26, 2013 4:06 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAFAKARII

NINAUNGA MKONO HOJA

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 26 June 2013, 15:42
Subject: Re: [wanabidii] TAFAKARII

Jamani tunapaswa kuzingatia sheria, kila kipande cha ardhi ya mji kinatakiwa kitumike kama ilivyokusudiwa, hatupaswi kukubaliana na hii habari ya kila eneo la mji kuwa sehemu ya biashara. Watu wanapanga samaki, mboga-mboga sakafuni kando ya barabara na hata kwenye reserve road. Magari yetu mengi tuyatumiayo yako chini ya kiwango maana ni second car, yanatoa moshi kibao na kuathiri hata hizi bidhaa  tunazozitumia hasa vyakula? Muda mwingine tusikubali na kusuport  kila kitu kwa kisingizio cha ugumu wa miasha.

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, June 26, 2013 2:03 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAFAKARII

Nidhamu ya usafi wa miji na land use plans zake lazima uwepo na sheria izingatiwe.

Sijawahi kwenda mjini posta na maeneo ya kariakoo kwa muda mrefu. Nilipita Jumamosi last week kuelekea Buguruni. Niliona kimawazo hapa DSM kuwa- City Council na municipals zake na Mzee mkali Regional Commissioner mji umewashindwa. Hao City, Municipal Health Officers and Environmental Engineers, NEMC kulikoni nikajiuliza.

Vi nchi vidogo vinapigana vita vinakuja nyuma yetu vinatushinda. Hiyo Public, Private Partnership (PPP) katika waste collection and city cleansing activities- ni kipofu na gonjwa. Stormwater drainage system-imejaa mataka ya kila aina. watu wamepanga biashara barabarani, pembeni ya barabara pa kupita hakuna. Ninawahurumia wenye maduka kama wanafanya biashara kweli maana bidhaa zimepangwa mbele ya maduka yao hata pa kupita tabu. Hata kama kuna kuganga njaa-tugange kwa kuzingatia sheria na usafi.
Hebu fikiria gari likikosea njia au kuharibika kitu lije liingie pembeni litaua wangapi? Ni makorokoro, viosk, vibanda mitaa yote ya Manzese, kariakoo, karume, msimbazi na biashara mpaka buguruni pande 2 za barabara. Hatuna ethics za kufuata sheria si za miji tu hata vijiji, hata ya conservation.

Ni kubananisha majengo, vibanda na kuchanganya biashara. Moto ukizunga hauchagui. Pamoja na magari kutoa moshi wenye lead, upepo kutimua vumbi kupeperuka pande zote-watu wanauza chakula kikiwa wazi na mainzi yanaonekana kutua. Utaona pale matikiti kila mtu amekata vipande hayafunikwi. ukifika ubungo Mandera road landmark area-vyakula wazi, vumbi, inzi; maandazi wazi, mifereji uchafu wa kuzalisha maishi na mbu wa matende umejaa despite big size ya stormwater drainage system ya ubungo. Mitaro hiyo ipo clogged na uchafu maji yametuama.

Sehemu nyingine ukipita ni harufu ya kinyesi tu na malundo ya taka. Pia, wapo wanaochakula taka hizo bila protective gear na hapo pia kuna electronic na dispensary waste. Bado hao wafanyakazi wa makampuni wanaonyonywa na local companies kufanyishwa kazi za ufagizi na uzoaji takangumu bila ya protective gear anakula vumbi lenye usafi wa kila aina na lenye wadudu wa kila aina.

Huko manzese wanakojenga barabara-wametandaza barabarani wakati greda linafanyakazi. kampuni inakwama kujenga kwa vile watu wametandaza biashara barabarani. Jee, greda au lori likipinduka na kuua idadi kadhaa ya watu hapo barabarani atalaumiwa nani. Muda wa kampuni unakwisha kutokana na biashara barabarani na msongamano wa magari na meza za biashara. IFIKE MAHALI KIFANYIKE KITU CHA KUJENGA NIDHAMU ZA AINA ZOTE PAMOJA NA UTII WA SHERIA ZA BIASHARA, AFYA NA MAZINGIRA ILI MIJI NA TOWNSHIPS ZETU NA VIJIJI VIWE MAHALA PA KUISHI NA PA KUTAZAMIKA. Tusitete uchafu kwa visingizio vya kuganga njaa. Ganga kwa nidhamu itakiwayo ya sekta husika. Hata nyumbani-usitembee bila nguo eti kwa vile upo nyumbani kwako. Maadili hayakuruhusu, wakati wowote anaweza akatokea mtoto, mpita njia, mgeni. Ni hivyo ktk biashara na environmental, business, health ethics and laws.

TZ inakaribia kuwa kama miji mingine michafu ya Bombay/India. NGO za jamii zishirikiane na Serikali kufufua makambi ya vilema na wazee na kujenga eneo kubwa fenced. Wawape vifaa na kuwafundisha ujasiriamali, walime mazao ya bustani, waweke dukani kwao hapo mapambo hayo mikeka, majamvi, vipepeo, viti, viatu, mchicha, kabichi, machungwa, asali etc na kuwapa tender ya kupeleka mboga na matunda, asali mashuleni, hospitali kwa kutumia gari yao watakayo wanunulia ktk hicho kituo. wafufue shule za ufundi za vilema ili ziwe kama zamani kupunguza ombaomba ambao baadhi wana viungo kamilifu kabisa wanatesa watoto kuzurura juani kutwa. Kuiua social welfare dept tatizo maana ombaomba analala barabarani na watoto na tunapita tunaangalia tu.

Bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuleta maendeleo na nidhabu ya utii wa sheria, usimamiaji majukumu sawasawa katika sekta mbali mbali hata environment..
Nani anahaki ya kuuza biashara katikati ya barabara? Ifike kwamba, maeneo ya biashara ndogondogo yakijengwa halafu waondoke warudi barabarani-Pinda strategy itumike kuleta nidhamu-waondoe kwa nguvu. Maeneo ya kupita kwa mguu wakipanga biashara-ondoa; ikipita gari, pikipiki, bajaji eneo la kupita kwa mguu-kamata toza faini kubwa ili kujenga nidhamu. Tatizo ya kutekeleza sheria bongoland ni-Rushwa!! Lakini-inawezekana.
 
From: Jonas Kiwia <jonaskiwia39@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 26 June 2013, 12:51
Subject: [wanabidii] TAFAKARII

Hii ni haki jamani,nimepita hapa magomeni muda sio mrefu na kukuta wamachinga wenye vibanda vyao wakikamatwa na askari mgambo. Na vibanda vyao kuvunjwa vunjwaa.
Kulikua hamna namna mbadala ya kulishughulikia hili mpaka na maaskari wakiwa na mabomu  pia?
Mboona nguvu nyingi kwa vitu vidogo?
Nawaza
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment