Sunday 30 June 2013

Re: [wanabidii] Kumbe jiji la DSM linapendeza likifanyiwa usafi!

Pale watakapoondoa (na itaanza soon kuwa wana siasa asiwe mwajiriwa ktk GVT) kuacha kuchanganya siasa na utendaji serikalini. Itasaidia ikiwa-asiyetekeleza majukumu akiwa GVT staff-afukuzwe kazi au kushushwa cheo ndio hii ya wapiga kura wetu wasisumbuliwe itaisha.

Hata kama chama chako kitashinda kuongoza nchi, hutowaruhusu wananchi wakate miti hovyo, wafuge na kulima mpaka vyanzo vya maji. Fikiria mtu kwao usukumani analima kila kona mchele anauza ZNZ na Kenya ila mifugo analeta Kilosa na Rufiji huko anachapa watu bakora na mpunga auzao Mwanza huku pwani mpunga ni malisho ya ng'ombe zinalishwa mashambani. Amezitawanya ng'ombe mia zipo Mwanza, Mia Rufiji, Mia Kilosa na mbuzi kibao. Akilima Loliondo au Naitolia mahindi si majani anazungushia mti wa miba wa mgunga (Acacia nilotica). Ruvu, Chalinze, Kilosa, Mkuranga mahindi shambani ni majani ya mifugo-mapigano, vita, kuuana na kutiana vilema.
Soko lipo Buguruni, Makumbusho, Mabibo-wapo barabarani kati kati ya njia na vumbi chakula kinauzwa-wasisumbuliwe wanaganga njaa. Mitaro ambayo mkandarasi anachimba kujenga pembezoni mwa barabara-usiku wanakuja kutupa magunia ya takataka. Asubuhi mkandarasi kwanza azoe taka. Hii inawatesa na ni Tanzania pekee duniani wakandarasi kufanyiwa hivi (tunasikia wakilalamika).

Barabara ya Dar-Bagamoyo inasikitisha hayo malundo ya taka daily mitaroni. Wakati huo huo under PPP mitaa ina mfumo wa kukusanya na kulipia uzoaji taka ambapo hatutaki kulipia kiasi kwamba mtaa unashindwa kumlipa mkandarasi wa kuzoa taka. Kila mtu anatupa usiku ili asilipie. Magunia ya taka yapo katikati ya barabara ya Ubungo Manzese, Ubungo-Mwenge mchana yanaonekana. Na mwingine anafuga ng'ombe daraja la ubungo kinyesi kinaoshwa na mvua unakiona kimetiririka mto ubongo kimetuama kinazalisha mbu culex wa matende. wanapisa maofisa mazingira, afya, mtaa wanaona ila wamekula jiwe.

Uchafu unaonekana Jon Mushi ila-mfuate kumshitaki au kumkataza huyo mfuga ng'ombe umwagiwe tindikali. Hata kama ukipeleka suala ofisi ya kata/polisi ukiomba wasikutaje, mshitakiwa atatoa senti kuwapa wamtajie watakutaja. Kisha anakuja kukukomesha kidomodomo!!

From:
john mushi <mushijohn@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, 30 June 2013, 12:27
Subject: Re: [wanabidii] Kumbe jiji la DSM linapendeza likifanyiwa usafi!

Nyie mnafikiri huo uchafu hauonekani? tatizo ni kwamba wanaochafua ni "wapiga kura wetu".Kwa hali hiyo uchafu utadumu milele hapa Dar, Labda Obama ajitolee kuja kwetu kila mwaka!ili JiJi lisafishwe na "wapiga kura" waelekezwe maeneo ya kufanyia shughuli zao kwa sababu hata hizi barabara mnazojenga za mabasi ya kasi zitageuka magulio.Pita manzese uone.

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, June 30, 2013 7:53 AM
Subject: Re: [wanabidii] Kumbe jiji la DSM linapendeza likifanyiwa usafi!

Wewe ulie tu. Subiri Obama aondoke utaona watapanga mpaka ndani mifereji ya majitaka na kunuka kwake maji ya kinyesi watapanga tu na utakuta mtu kavaa nadhifu hapo anakula ngisi pamoja na mainzi na harufu zote hizo..

Kama mtu anaona barabara inajengwa na malori, greda zinapita na vichimbio vinachimba na kutimua fumbi na bado yupo-ni akili hiyo kweli? Hatari anaiona kuwa wakati wowote lori linaweza likakosea njia likamkanyaga akawa kilema atajuta au atafurahi? Amepanga biashara tena ya chakula pembeni mwa barabara au katikati ya barabara mbili zinazojengwa na kupitisha magari wakati huohuo.

Daraja la manzese limejengwa ili kuepusha ajali watu wapite juu-ndio kumepangwa biashara na viosk vya biashara. Hakuna nidhamu hata kidogo. Tusijali kukusanya ushuru na kuachia biashara kishaa sheria kukiukwa ndio tunayalea. 

Wameambiwa boboa na walilipwa kuanzia 1994- (Mfano wa Ubungo mataa hadi kimara temboni)-Hawajabomoa. Hata ile karakana ambayo tuliambiwa itaepukwa kupunguza gharama-ukipita unaona kaongeza chumba kwa sasa kaingia barabarani zaidi. Wanaona waliokaidi kubomoa Victoria-makumbusho na barabara nyingine na wanavyolalamika katika T jinsi tingatinga linavyolamba mali zao. bado wanaudanganya umma kuwa-Tunaonewa kubomolewa. Wachache sana wanasema ukweli kuwa-uzembe wetu. Miaka imepita wamepewa taarifa na wamezidisha wenyewe kuipita nondo ya survey.

Ukiangalia NHC zilipojengwa-mbali na barabara kuzingatia nondo za alama ya pima ardhi. Hata hospitali ya magomeni angalia ukipita kuta zake ziko umbali gani na barabara au  kituo cha police magomeni na NHC houses za maghorofa, nyumba 6 na zile ndogo ndogo-zinakuonyesha jinzi GVT ilivyozingatia alama za pima ardhi, kuta zipo mbali na barabara. Wao wananchi maghorofa yametokeza mpaka barabarani na kuopngeza ukuta nje zaidi.

Pia ukiangalia waliopanga NHC-wamebadili design na kujenga maduka, bar, restaurant kinyume na utaratibu. hawa nao itakuja kula kwao pindi wampate muona mbali. Maana hata njia kati ya ghorofa na ghorofa ndogo, watoto hawana pa kucheza kama zamani. Ninakupangisha kama mpangaji-unaibadili nyumba yangu utakavyo? Hii ndio bongoland!!

Kwa nini yule wa 1994 wa ubungo mataa-kimara temboni asijifunze kuwa naye litamfika la kupoteza mali zake bila fidia? Yupo amekaa anaangalia! Na kila siku anafuta maandishi ya bomoa kwa rangi nyeupe. Licha ya GVt kukubali uzembe wake kwa kuwaachia wajenge hivyo kuwalipa, lakini bado hajaondoka. Hivyo, uone akili zetu zilivyo. Watarudi, na wakiondolewa watapiga askari na mgambo nondo. ukienda soko zilizojengwa hapo jirani-zipo wazi ndani. hivyo baadhi ya watu wameitumia nafasi wamejenga vyumba vya biashara. Na soko kama makumbusho lenye nafasi kubwa-watu watajenga na kuchukua nafasi ile kujenga baa, maduka kwa kuhonga wahusika.Ni bongoland ya ubongofinyu.

From: Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com>
To: Mailing Lists <wanabidii@googlegroups.com>; Mailing Lists <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Mailing Lists <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Saturday, 29 June 2013, 11:28
Subject: [wanabidii] Kumbe jiji la DSM linapendeza likifanyiwa usafi!

Kutokana na ujio wa Mhe. Raisi wa Marekani Barack Obama...sehemu kubwa ya jiji zimefanyiwa usafi mpaka raha...
 
Changamoto: Je, hali ya usafi itaendelea kuwa hivi pindi ziara itakapokwisha?
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment