Sunday 30 June 2013

[wanabidii] Simulizi Za Mzee Madiba; Mandela Alipomshangaza Dereva Wa Mheshimiwa!



Ndugu zangu,

Kama tulivyoona huko nyuma, Mzee wetu Madiba hana makuu. Kuna simulizi pale Mzee Mandela akiwa Ikulu alimwalika Mheshimiwa mmoja kwa chai ya saa nne asubuhi. Mgeni wa Mandela akaingia Ikulu. Baada ya kusalimiana, na kabla ya kukaa chini kunywa chai na kuzungumza, Mandela alimuuliza Mheshimiwa yule;

" E bwana, nimeona ukiingia ukiwa na dereva akikuendesha, mbona hukuja nae, si dereva wako wa siku zote?"

" Ndio Mheshimiwa Rais!" Alijibu mgeni wa Mandela.

Naye Mandela akasema; " Basi, kama ni hivyo, ngoja nimtume mtu aende akamwite, naye aje tunywe nae chai!"

Dereva yule wa mheshimiwa hakuamini masikio yake alipoambiwa kuwa anaitwa aende akanywe chai meza moja na Nelson Mandela!

Naam, huyo ndio Mzee wetu, Nelson Mandela! Mtu wa watu wa dunia nzima, masikini na matajiri!

Maggid,

Iringa.
http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment