Saturday 29 June 2013

[wanabidii] Wanafunzi wauziwa dawa za kulevya kwenye barafu, vinywaji, vyakula

Mikate na barafu zinazouzwa kwenye shule za msingi zinadaiwa kuwekwa dawa za kulevya hali inayosababisha watoto kuathirika.

Hayo yamesemwa jana katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupinga dawa za kulevya duniani.

Lukuvi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika maadhimisho hayo yaliyofanyika hapa, alisema Serikali itaanza kufuatilia biashara hizo shuleni.

Alisema, "sasa dawa hizi zinauzwa hadi kwenye vitu ambavyo watoto wanakula katika shule za msingi, kwa mfano hivi sasa dawa hizo zinawekwa kwenye maandazi, mikate na barafu. "Ni lazima kufahamu watu gani wanauza vyakula vya aina hiyo na wana nia gani," alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, watu hao wanafanya jambo ambalo limekuwa likifanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu.

Alisema kutokana na hali hiyo, mtoto wa shule anaingia darasani akiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe, kidani chenye nyembe kifuani, wanaingia na misumari mifukoni, hawafungi lisani za suruali zao na wengine kutembea vifua wazi, jambo ambalo alisema Serikali lazima iliangalie.

Hata hivyo, Lukuvi alisema vita dhidi ya dawa za kulevya bado ni kubwa kutokana na wanaoendesha biashara hizo kuwa na fedha za kutoa rushwa na kuhonga kwa lengo la kuzuia kukamatwa au kutofikishwa katika vyombo vya Dola.

---
Sehemu ya taarifa kwenye gazeti la HabariLeo.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2XZjoUAr9

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment