Saturday 29 June 2013

Re: [wanabidii] Wanafunzi wauziwa dawa za kulevya kwenye barafu, vinywaji, vyakula

No research, no right to speak. Hizi ni ndoto za Ali Nacha. Kama Lukuvi anafahamu hilo (kwa utafiti aliofanya) kwanini hadi sasa hajawachukulia hatua hao wauza maandazi? Mama ntilie aweke dawa kwenye maandalizi ili iweje na ataweka dawa kiasi gani mpaka ikolee kwa maandazi yote? Hapo ndipo uwezo wa kufikiri wa viongozi wa serikali hii ulipokomea! Wanafikiri kwa kutumia masaburi. Nashangaa kwa nini hao wahalifu kama wapo wasiPIGWE TU kama mkuu alivyoamrisha. Kama  ni kupiga, basi hivyo vipigo vilipaswa kuanzia kwa hawa 'wahalifu' wa kufikirika. Hii research ni mpya na ni kali sana. Lukuvi kaifanyia mkoa gani vila na alihusisha shule ngapi? Shame upon Lukuvi!

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, June 29, 2013 8:03 PM
Subject: Re: [wanabidii] Wanafunzi wauziwa dawa za kulevya kwenye barafu, vinywaji, vyakula

Felix yawezekana faida yake sio moja kwa moja kwa maandazi hayo. Anaweka humo watoto wawe adicted. Baada ya hapo wataitahuta na watabugia. Hii ni namna ya kufanya advatisement.

--- On Sat, 6/29/13, Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com> wrote:

From: Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Wanafunzi wauziwa dawa za kulevya kwenye barafu, vinywaji, vyakula
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, June 29, 2013, 2:22 AM

Kwakweli utumiaji wa dawa za kulevya sio mzuri, unapashwa kukemewa; ila nashangazwa na:
  1. Ina maana mfanya biashara ambaye anatarajia apate "mkate wake wa kila siku" anaweka madawa ya kulevya kwenye maandazi ya watoto wa shule? Ili iweje? Fikiria kama anatengeneza maandazi mia 5, ataweka dawa za kulevya kiasi gani kwa andazi la kuuzwa sh 100? Yaani maandazi mia 5 kwa @sh 100 apate shs 50,000/= ? Dose-response ya hizo dawa zikoje?
  2. Ina maana watu hao wanawalenga watoto wa shule za msingi na sekondari tu?
  3. Hao wafanyabiashara ambao "maandazi" yao yamekutwa na madawa "wamechukuliwa hatua gani" ?
Ni jambo la busara kama tungepatiwa takwimu "halisi" kwamba katika shule fulani, utafiti umefanyika juu ya maandazi yanayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya. Majibu yanaweza kuwa: katika sampuli ya maandazi "X" (ya wafanyabiashara kadhaa) maandazi "Y" yamekutwa na mabaki ya madawa ya kulevya.
 
Pia, sampuli damu za wanafunzi (mchanganyiko) kwa maana ya kwamba kuwe na uwiano wa wanafunzi yaani std 1, 3, 7. Pia kuwe na uwiano wa umri (kuna wanaokula maandazi na kuna wasiokula maandazi), pia uwiano wa kijinsia - wasichana na wavulana. Sampuli damu zao zifanyiwe uchunguzi na "wahusika" watoe majibu "juu ya mabaki ya dawa za kulevya".
 
Vikifanyika hivi, basi hitimisho zuri litapatikana kwamba mabaki ya dawa za kulevya ambayo chanzo chake ni maandazi yamekutwa kwenye sampuli damu za wanafunzi na kuwe na uwiano.
 
Ni mtazamo tu!
 
2013/6/29 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
 
Mikate na barafu zinazouzwa kwenye shule za msingi zinadaiwa kuwekwa dawa za kulevya hali inayosababisha watoto kuathirika.
 
Hayo yamesemwa jana katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupinga dawa za kulevya duniani.
 
Lukuvi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika maadhimisho hayo yaliyofanyika hapa, alisema Serikali itaanza kufuatilia biashara hizo shuleni.
 
Alisema, "sasa dawa hizi zinauzwa hadi kwenye vitu ambavyo watoto wanakula katika shule za msingi, kwa mfano hivi sasa dawa hizo zinawekwa kwenye maandazi, mikate na barafu. "Ni lazima kufahamu watu gani wanauza vyakula vya aina hiyo na wana nia gani," alisema Lukuvi.
 
Kwa mujibu wa Lukuvi, watu hao wanafanya jambo ambalo limekuwa likifanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu.
 
Alisema kutokana na hali hiyo, mtoto wa shule anaingia darasani akiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe, kidani chenye nyembe kifuani, wanaingia na misumari mifukoni, hawafungi lisani za suruali zao na wengine kutembea vifua wazi, jambo ambalo alisema Serikali lazima iliangalie.
 
Hata hivyo, Lukuvi alisema vita dhidi ya dawa za kulevya bado ni kubwa kutokana na wanaoendesha biashara hizo kuwa na fedha za kutoa rushwa na kuhonga kwa lengo la kuzuia kukamatwa au kutofikishwa katika vyombo vya Dola.
 
---
Sehemu ya taarifa kwenye gazeti la HabariLeo.
 
--
  
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
  
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
  
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment