Friday 28 June 2013

Re: [wanabidii] Karibu Obama nchi ya Madalali

Asante Monica kwa kuomba radhi, huo ndio uungwana. Umenifurahisha uliposema '...oooooh SIJUI KIGAMBOBI, KAMA RASLIMALI SI MZICHIMBE WENYEWE MNANGOJEA NINI?' ukanikumbusha wakati wa mgogoro wa gesi Mtwara, jamaa yangu mmoja aliniambia; "hivi hawa watu wa NTWARA walikuwa wanajua kama wana gesi miaka yote hii? Ningekuwa ni Serikali ningewaambia haya chukueni SULULU MKAICHIMBE hiyo gesi baharini kama wangeweza".

Joe

2013/6/28 Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
Sorry Emanuel kama maandishi yangu yamekuudhi key board yangu ilikuwa imejam ndio maana. now its ok
 
Date: Fri, 28 Jun 2013 08:34:25 -0400
Subject: Re: [wanabidii] Karibu Obama nchi ya Madalali
From: emuganda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Monica,
Nakuomba next time unapoandika ukumbini tumia herufi ndogo. Herufi kubwa ni kama vile una shout kwenye movie theatre.
Ni ushauri tu.
em

2013/6/28 Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
JAMANI WATANZANIA TUACHE KULAUMU KILA LINATOKEA KUAMINI KUWA LINA SABABU. UTARATIBU WA MARAISI KUTEMBELEA NCHI MBALIMBALI MBONA UPO SIKU ZOTE TANGU ENZI NA ENZI DUNIANI POTE?? KWANINI HILI LA OBAMA MMELIVALIA NJUGA? MNATAKA AJE KUGAWA HELA KWA KILA MTANZANIA? MBONA RAISI WETU AMEKWENDA NCHI KARIBU ZOTE DUNIANI MBONA HATUJASIKIA KAMA WAALIMKATAA AU KUMPIGIA MAJUNGU KAMA TUNAVYOFANYA KWA OBAMA.
TUACHE UVIVU TUFANYE KAZI SIO KUSUBIRI ooooh OBAMA KAJA KWA AJILI YA RASLIMALI oooooh SIJUI KIGAMBOBI, KAMA RASLIMALI SI MZICHIMBE WENYEWE MNANGOJEA NINI?
KARIBU OBAMA TUNAKUKARIBISHA KWA MOYO MKUNJUFU
 
Date: Fri, 28 Jun 2013 04:45:09 -0700
From: mobinsons@yahoo.com
Subject: [wanabidii] Karibu Obama nchi ya Madalali
To: wanabidii@googlegroups.com

Karibu  Obama nchi ya  Madalali

Na Mobini Sarya
OH ! Dar salaama umepambwa  ukapambika ,sawa na bibi harusi anayejiandaa  kumlaki  bwana harusi, barabara  zimesafishwa  lami zimepigwa deki, laiti kama pilika pilika hizi  zingekuwa  za siku zote  mji huu ungekuwa  tafauti  na ilivyo  sasa.
Gharama kubwa  zilizotumika kuandaa jiji hili kwa mda mfupi ni kwa,ajili ya kumlaki bwana mkubwa  Baraka Hussein Obama,rais wa Marekani mwenye asili ya afrika mashariki kutoka nchini  Kenya.
Ni nani huyo rais Obama? Baba yake Hussein  Obama wa kabila la kijaluo  kutoka  eneo la kisumu  nchini Kenya alikuwa muislam aliyesafiri  hadi nchini ,marekani na kuzaa huyo mtoto mwenye mchanganyiko wa dini na makabila tofauti.
Lakini kilichosalia ni kuwa Obama ni mwafirika mwenye asili ya Kenya ingawa ni raia wa Marekani kwa mjibu wa sheria za nchi hiyo.             
 Hivyo rais Obama alitarajiwa kuleta usawa kwenye dunia hii kwa kuwa yeye ni mkristo aliyelelewa kwenye nyumba za kiislam  katika ,maeneo na wazazi tafauti.
Rais Obama alitakiwa awe kiongozi tofauti kati ya viongozi waliowahi kuiongoza dunia kutokana na historia ya maisha yake iliyochanganyikana na jamii ,pamoja na tamaduni tofauti,lakini imekuwa kinyume na matarajio ya wengi.
Tumeambiwa kuwa rais  Obama amechagua kuja Tanzania badala ya nchi ya Mabababu zake Kenya  kwasababu eti uchumi  wetu unakua kwa kasi pamoja na kuzingatia utawala bora,kweli?
Lakini pia Rais Obama anakuja nchini ikiwa ni miezi michache imepita baada ya kuondoka  hapa mtawala wa China,taifa ,lenye  nguvu kama marekani.
imaana  Ziara ya Rais  Obama ni kama kufuta nyayo za kiongozi huyo wa china? Au ni kutokana  na ongezeko la maliasili zinazogunduliwa  kila mara katika eneo hili?      
Ewe rais Obama karibu Afrika,Karibu nchi ya madalali! Angalia wasikudanganye kuwa  hii ni nchi masikini ,sio kweli  wanataka kukuibia hao Tanzania ni tajili ila watu wake ndio masikini kutokana  na kuongozwa na viongozi masikini wa akili.
Rais Obama umasikini wa akili ni mbaya kuliko,unaweza kuwa na mali ukashindwa kuitumia ,ukabaki omba omba kwa wale ambao hawana mali kama yakona wakati mwingine unawapigia magoti wakudondoshee makabaki,aibu hii!
Rais Obama wewe unakuja na nini kwenye nchii  ya madalali wasio fanya  kazi wakisubiri  teni  pasenti  za mikataba?
Mtangulizi wako  Rais George Bush,alikuja  hapa na chandarua baada ya kuelezwa kuwa  tatizo letu kubwa ni malaria na wanaume wa hapa hawana uwezo wa kukabiliana na Jeshi la Mbu.
Oh Obama,au umekuja kumalizia  malipo ya eneo la kigamboni? nasikia Bush alistaafu akiwa bado anadaiwa  sasa wewe  umekuja  kumaalizia  deni   hilo,ndio maana nay eye Bush atakuwa mjini  Dar es saalam   wakati wa ziara yako.
Nimekuambia hii ni nchi ya  madalali angalia wasikuibie hata unapolala usiku Kampiski mikono  shikilia kwa nguvu mikononi  , mwenzako Bush alipogundua hilo,aliamua kutoa vyandarua badala ya pesa lakini nako  wakamchakachua.
Uliza  nikuambie walikwenda hadi kwenye kiwanda cha A-Z kilichopewa pesa  cha  jijini Arusha,wakaomba  asilimia yao vingenevyo vyandarua vingekataliwa , mmiliki akaona isiwe taabu tutapunguza upana wa chandarua ili kufidia   gharama ya dalali waliodai ndio wamemleta Bush Kichaka.
Leo hii pesa ya wamarekani iliyotolewa kwa ajili ya kuwanunulia watanzania chandarua  ni kama imepita  bure kwani  chandarua zilizotengenezwa utadhani ni maalumu kwa ajili ya wachina.
Kifupi ni kwamba hazitumiki raia wameamua kuzitumia kuvulia  samaki na kufugia kuku, hakuna chandarua ni mitego ya kuogea ile, utapeli mtupu lakini serikali  ikapokea   shirika la viwango (TBS)likapitisha wananchi wakagawiwa!maajabu kaabisa.
Rais Obama tunalomuuza mwenyeji wako rais Kikwete ni hili yeye akiwa anasafiri nchi mbalimbali wasaidizi wake wanatetea ziara zake kwa maelezo kuwa zina manufaa,kwani  anakwenda  kuomba misaada.
Je na wewe kuacha raaha za white house kuamua kusafiri hadi mashariki ya Afrika umekuja kufuata  nini? Umekuja kukagua mji wa kigamboni au umewambia raia wako  kuwa  ziara Tanzania ina manufaa kwa taifa la Marekani?.
Tuambie manufaa hayo kwanza ili na sisi tupime ya kwetu,kwani  haiwezikani, wewe ujio wako ulete manufaa kwetu peke  yake,yaani  rais wetu aje marekani   tuambiwe  ziara zake zina manufaa, wewe uje Tanzania bado tuambiwe ziara hiyo ina manufaa   kwetu!
Ndugu Obama ziara yako ina Ma    ........................ www.mobinday.blogspot.com
                          
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment