Friday 28 June 2013

Re: [wanabidii] Neno La Leo: Julius Nyerere Na Ushirikina Wetu…!

Majid.
naomba kuuliza:
ushirikina ni watu kwenda kumuomba Mungu, au ni washirikina hata kama wanamuomba Mungu? Swali kama halieleweki heri nilifafanue lakini usililipue. Kwa maana nyingine huamini kuwa Mungu anaombwa na kujibu? Nataka kujua tushirikiane na nani kumsaidia nani

--- On Thu, 6/27/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Neno La Leo: Julius Nyerere Na Ushirikina Wetu…!
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, June 27, 2013, 12:21 PM

Ndugu zangu,

 Asubuhi ya leo hapa Iringa nilishangaa kuona makundi ya watu yakitokea maeneo ya Kihesa kuelekea katikati ya mji.

 Nilipouliza nikaambiwa wanakwenda kwenye maombi. Ndio, Alhamisi asubuhi, watu wanafunga safari kwenda kwenye maombi. Nimeambiwa maombi hayo ni ya siku kadhaa. Ni siku kadhaa za watu kutokufanya kazi.

 Na wengi ni watu wazima, na zaidi wanawake. Kwa kuwaangalia, kuna wenye kwenda kuombewa kwa hofu ya kuwa wamerogwa, au wanahofia wasije wakarogwa.  Ni hofu ya ushirikina. Na wengi wanaumwa kisaikolojia. Kuna wenye kujihisi wamerogwa, ama , wanaishi na wachawi kama majirani. Hawa wako gizani kwenye wengine tunachokiona ni nuru.

 Inanikumbusha kisa cha Julius Nyerere na mwandishi wa Kimagharibi. Miezi ya mwanzo kabisa ya Tanganyika huru, mwaka 1961,  Julius Nyerere alitembelewa na mwandishi wa habari kijana wa Kimagharibi. Mwandishi yule alimwuliza Julius Nyerere, Rais kijana kwenye nchi changa  swali lifuatalo;

 " Mheshimiwa Rais, unadhani kwa sasa ni kitu gani kimetawala fikra za watu unaowaongoza kwa maana ya Watanganyika ?"

 Julius Nyerere alitulia kidogo, kisha akajibu;

 " Kwa kweli kilicho mbele kabisa kwenye fikra za watu wangu ni ushirikina. WaTanganyika wengi wanafikiri sana juu ya mambo ya kishirikina, hasa zaidi watu wa vijijini".

 Miaka mingi ikapita, na kabla ya Julius Nyerere hajang'atuka uongozi, mwandishi yule alirudi tena Tanzania. Akakutana na Julius Nyerere. Akamwuliza swali lile lile la mwaka 1961, akitaka kujua Watanzania wa sasa ni kitu gani kilicho mbele kwenye fikra zao.

 Julius Nyerere hakuchukua muda mrefu kutoa jibu. Alisema;" Ooh! Kwa sasa hali ni mbaya zaidi. Watanzania wa sasa  wanafikiri zaidi mambo ya ushirikina, na sasa si vijijini tu, hata watu wa mijini nao wanatanguliza sana mambo ya ushirikina kwenye fikra zao!"

 Ndio, msafara ule niliowaona leo asubuhi wakitokea Kihesa na kwingineko ni WaTanzania wa mijini!

 Ni Neno La Leo.

 Maggid Mjengwa,

Iringa.

http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment