Friday 28 June 2013

[wanabidii] Msimamo Mkali Wa Vijana Wa Mlimani ( V)- Mkapa Alikuwa ' Profesa' Wa Ujamaa...!



Na Born Again Pagan

Katika makala yaliyopita, tuliona matukio kumi na moja yaliyochangia kikamilifu katika kujenga mkitadha wa msimamo mkali wa baadhi ya vijana waliokuwa wakisoma hapo Mlimani (1960 hadi 1970). Hii haina maana ya kwamba hao ndio walikuwa vijana tu wa msimamo mkali waliopata kuelemishwa hapo Mlimani. La, hasha!

Na wala haina maana ya kutamati kuwa matukio hayo yalitokea kuwafanya wawe na msimamo kama huo. Ilikuwa ni dhamira au busara (prudence) ya vijana hao wachache kuyaona matukio hayo yakitoa changamoto; wakapata fursa (opportune) kuyatafsiri ili yawe na maana maishani.

Makala haya yanaendelea kuelezea matukio mengineyo sawa na yaliyopita, kama ifuatavyo:

Kumi na nne, Tanzania Bara: Kushindwa kwa siasa na sera za ki-Bepari, chini ya Mpango wa Taifa ya Maendeleo wa Miaka Mitatu-Mitatu (ulioishia mwaka 1965). Mipango hii ilizalisha matabaka ya akina "ma-naiza" na "ma-kabwela" (mithili ya hali ilivyo sasa nchini kwetu) Ikumbukwe kwamba mfumo wa mipango hiyo ulitungwa na Mashirika ya Kimataifa ya Fedha (Benki Kuu ya Dunia na Mfuko wa Fedha).

Kujengeka kwa matabaka hayo ya "ma-naiza" na "ma-kabwela" kulichangia sana kuelekea kwenye..... Soma zaidi...http://www.mjengwablog.com/siasa/item/3579-msimamo-mkali-wa-vijana-wa-mlimani-v-mkapa-alikuwa-profesa-wa-ujamaa.html#.Uc2K1JyNCAg

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment