Monday 24 June 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Mwigulu, Msigwa Na Hamu Ya Vurugu Mechi!

Duh Maggid ngoja nikupe nukuu ya Msigwa baada ya kurushiana maneno na Mwigulu " achana na yule mnafiki (Mwigulu), mimi siwezi kuzungumza na mtu mnafiki, mkatili na yeye ndiye alihusika na mipango mibaya dhidi ya Chadema hata mlipuko wa Arusha hivyo kutesa watu wa Chadema"

Kweli hapo chai inayweka kati ya Mwigulu na Msigwa?

Lakini pia soma pata hii "....Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno...". Na hapo chai inanyweka Maggid?

Nikirejea kwenye hoja yako inawezekana kabisa ina msingi na ukweli ndani yake, lakini mfano ulioutoa unaipunguza nguvu.

Suala la pili, wewe unaamini wabunge wana jipya kuhusu Ukimwi? Uwaonavyo bungeni, wanavyochangia bajeti kutwa wakijua kwamba wanaonekana kwenye luninga ndo wanakua vile, je wakiwa nje ya hapo hali huwaje?

Tatu na mwisho, habari ina sifa zake. Tatizo tulilonalo kwenye media zetu leo ni kudhani kwamba kila asemacho mbunge, waziri au rais ni habari. Tunajivuta kutoka huko, hatutamani vyombo vyetu kugeuka tena 'leaders' diaries'
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Date: Mon, 24 Jun 2013 09:17:20 +0300
To: mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Mwigulu, Msigwa Na Hamu Ya Vurugu Mechi!

Ndugu zangu,


Leo jijini Dar wanakutana wanahabari na wadau wa habari zaidi ya 150. Watajadili maadili na wajibu wa wanahabari kwenye hali ya migogoro. Watachambua pia hatari ya lugha za chuki, udini na mengineyo. Wataangalia pia namna njema ya kukabiliana na hali hizo.

Ni hatua njema kabisa na imekuja wakati muafaka. Na hapa nawasifu MCT kwa kufanikiwa kuwakutanisha wanahabari katika hili. Kila la kheri.

Na kwenye hili la wanahabari na migogoro tunaweza kuona mfano wa moja ya habari kubwa jana Jumapili; Iliwahusu Wabunge Mwigulu Nchemba ( CCM) na Peter Msigwa ( CHADEMA)

Hakika niliamka nikisikia vichwa vya habari vya uhasama vikitamkwa redioni. Kisha nikajionea mwenyewe nilipoyanunua magazeti kadhaa ya jana.

Naam; " Mwigulu na Msigwa nusura wazichape!". Mengi ya magazeti yalibeba habari hiyo katika staili ya kufanana- Waheshimiwa nusura wachapane! Na picha kubwa ya waheshimiwa hao ikawekwa mbele kwenye magazeti hayo.

Kabla hata sijaisoma habari yenyewe, nilipoangalia picha tu, nikajiuliza; hivi walio kwenye nusura ya kuchapana makonde ndio hawa?!

Picha tu ilijieleza, kuwa Msigwa na Mwigulu ni watu wenye kufahamiana na pengine hukutana kunywa kahawa pamoja. Kwamba pale, na kwa mujibu wa habari yenyewe, walikuwa kwenye mabishano ya hoja. Ni kawaida. Maana, sikuona hata mahali wametukanana.

Masikini Msigwa na Mwigulu, hawa ni watu wazima na familia zao. Fikiri mtoto wa mheshimiwa anaambiwa na mwenzake shuleni; " Eeh, nimesikia baba yako anataka kuzichapa na mwenzake huko bungeni!" Ni mambo ya kudhalilisha kwa kweli, si kwa familia tu. Hata kwa Mheshimiwa kwa wapiga kura wake. Naam, Waheshimiwa wakianza kuchapana makonde hadharani badala ya kuzungumza wanaacha kuwa waheshimiwa. Wanabaki kuwa wahuni tu, kama wale wa mitaani.

Na hapa ndipo tunauona udhaifu wetu wanahabari, kuwa tunapenda sana kushabikia 'vurugu mechi'. Maana, utotoni tulipokuwa tukenda viwanjani, moja ya burudani tuliyoona ni ya kufurahisha ni pale ilipotokea ' vurugu mechi!' Kwamba hapo rafu mtindo mmoja na kinachofuatia refa kukimbia mwenyewe au kukimbizwa kwa fito.

Naziona dalili za media yetu kuanza hulka ya kushabikia ' vurugu mechi' badala ya mambo ya msingi. Ona jana, wabunge wale wapambanaji wa UKIMWI waliudhuria semina ya UKIMWI. Lakini, kilichoongewa na wabunge hao kuhusu UKIMWI hatukukisikia hata kimoja!

Hivyo, wakati wanahabari wakikusanyika hii leo pale Dar kujadili maadili ya kazi zao na wajibu wao kwenye migogoro waiangalie pia mifano kama ya jana kwenye media. Maana, badala ya media kuchangia kwenye kupunguza tension na migogoro, inaweza kuchangia kwenye kuichochea! Na hilo si jukumu la media yenye kuwajibika na kuzingatia uzalendo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment