Tuesday, 2 June 2015

[wanabidii] JINSI YA KUMTAMBUA GAIDI / MHALIFU

Wananchi wanatakiwa kuchukuwa tahadhari na kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama endapo amegundua vitu kama hivi .

MTU AMBAYE SI WA KAWAIDA
Yuko eneo ambalo hatakiwi au amepotea

Amevaa mavazi yasiyomtosha ( makubwa ) au mavazi yake hayahusiani na hali ya hewa kwa wakati huo 

Kuangalia au kufuatilia mambo sehemu bila ruhusa 

Kushangaa shangaa sehemu kama vitu vya polisi , benki , jeshi au makazi ya viongozi hii inaweza kuwa ndani ya jengo au nje 

Hawezi kuangaliana na mtu uso kwa uso na mara nyingi anaonekana mwenye haraka .

Hupiga picha , kuchukuwa video , kuchora michoro , ramani au kuchukua taarifa za maeneo yasiyotakiwa 

Anaweza kujaribu kuingia maeneo yasiyotakiwa kwa makusudi ili kujaribu kuona hali ya usalama .

Anaweza kujifanya ni muuzaji wa bidhaa Fulani na kuja hata ndani ya maeneo nyeti kwa shuguli hiyo kumbe ni mpelelezi wa magaidi .

MAGARI NA VYOMBO VINGINE VYA USAFIRI

Gari au magari yaliyoegeshwa maeneo yasiyotakiwa 

Gari inaweza kuegeshwa mbali na baiskeli au magari mengine – lengo la kufanya hivi ni kupata fursa ya kupiga picha au kukimbia kwa urahisi .

Gari inaenda mwendo mdogo lakini likionekana zito mbele au nyuma sehemu za kubeba mzigo 

Gari inaweza kuwa imepakwa rangi mpya au mchoro mpya unaopendeza 
Gari haina namba sahihi au namba zake ni bandia .

Gari inaweza kuwa imeegeshwa kwa muda mrefu bila mtu au watu kufika .

VITU VISIVYOKUWA VYA KAWAIDA

Vitu hivi inaweza kuwa havijulikani , viko sehemu isiyotakiwa au vinaweza kupelekwa kwa mtu bila taarifa kama mabeki , barua au vifaa .

Kwenye siti au karibu na siti ndani ya gari 

Kwenye sehemu ya kungoja au chooni ( msalani )

Pembeni mwa barabara

Madarasa ya kufundishia

Migahawa 

Sehemu za ibada

Kwenye maduka , mahoteli na sehemu nyingine za burudani 

JUKUMU LA UMMA – JUKUMU LAKO WEWE

Usijaribu kutingisha au kuhamisha kitu ambacho si cha kawaida

Usijaribu kufanya mazungumzo sehemu ambayo hauna mazoea nayo au hujisikii au huijui  

Ondoka sehemu hiyo mapema na toa taarifa

Kama kumetokea mlipuko ondoka eneo hilo 

WAKATI UNATOA TAARIFA UNATAKIWA UWE NA YAFUATAYO

Nani umemwona , nini umeona 

Eneo lenyewe

Muda wa tukio lenyewe

Kwanini umepata mashaka 

Kama umepata taarifa za mtu yoyote anataka kufanya vitendo vya uvujivu wa amani toa taarifa kituo cha karibu cha polisi , au polisi aliyekaribu yako au mwanausalama , viongozi wa serikali kama ni wa mtaa , kata , wilaya , mbunge au yoyote ambaye anaweza kufanyia kazi taarifa mapema zaidi .

Namba za Polisi kwa Tanzania ni +255787 66 83 06 , +255713 323 999 ,  +255754 78 55 57

YONA FARES MARO
0786 806028



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment